Kama kweli Jeshi letu la Polisi linafanyia kazi taarifa za kiintelejensia, basi ni lazima limkamate Mwita Waitara......Wenyewe walishasema mapema,faili la upelelezi limefungwa
Lakini kila kukicha wanamtaka dreva na Lissu mwenyewe
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna clip ambayo imeendelea kusambaa mtandaoni, ambayo bila shaka yoyote, sauti inayosikika humo ni ya Mbunge wa Ukonga na waziri mdogo wa TAMISEMI Mwita Waitara
Katika clip hiyo amesikika mbunge huyo akitamka kuwa kwenye vita ya uchumi, mnapoona kuna mtu anawakwamisha kwenye vita hiyo hamna budi KUMTANGULIZA mtu huyo!
Ni maneno ya hatari sana kwa usalama wa nchi yetu, kutamkwa na mwanasiasa, mwenye wadhifa mkubwa wa ubunge, ambapo anatoa hukumu kuwa mtu wa aina hiyo hana budi kuuawa!
Ni maneno ya hatari mno kutamkwa kwa kuwa tunavyojua ni chombo kimoja pekee kilichopewa dhamana ya kutoa hukumu hapa nchini, ambapo chombo hicho ni mahakama
Vile vile ni maneno ya hatari mno kwa kuwa hadi sasa ni zaidi ya mwaka mmoja na nusu, hakuna mtuhumiwa hata mmoja aliyekamatwa na kufanyiwa "interrogation" kuhusiana na tukio lile la kumiminiwa risasi zaidi ya 30 kwenye gari lake, kwa nia ya kumwua Tundu Lissu, ambapo hadi sasa anaendelea kuuguza majeraha katika hospitali nje ya nchi.
Ndipo hapo ninapojiuliza, je Jeshi la Polisi linasubiri nini kumkamata Mwita Waitara, kwa mahojiano ili limfikishe mahakamani kutokana na maneno yake ya UCHOCHEZI??
Kama Jeshi la Polisi halitamkamata Mwita Waitara, tutajua kuwa limepewa "maagizo" toka juu ili lisifanye hivyo!
Kwa kufanya hivyo ndipo Jeshi hilo linatengeneza visasi vya hali ya juu ndani ya Jamii ya watanzania, kwa kuwa itakuwa inafahamika wazi kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya CCM, wanaweza kuongea vitu vya hatari sana kwa nchi hii, lakini vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi haviwezi kuwakamata, kwa kuwa kundi hilo la watu ni UNTOUCHABLES!
Inafaa Jeshi la Polisi limkamate Mwita Waitara kwa mahojiano na aeleze alikuwa ana maana gani ya kusema kwenye vita ya uchumi mtu mtakayeona mnatofautiana naye hamna budi KUMTANGULIZA??
Hivi wananchi wenye uchungu na ndugu zao nao wangekuwa wanalipa visasi na kuwaua wanasiasa waropokaji wa aina hii kama walivyofanya MUNGIKI huu uropokaji ungeendelea?Hawawezi kujikamata
Kamu Mungu muumba wa mbingu na nchi aishivivyo huyu atatangulia tena kwa mateso makali,Mungu hadhihakiwi.Inafaa Jeshi la Polisi limkamate Mwita Waitara kwa mahojiano na aeleze alikuwa ana maana gani ya kusema kwenye vita ya uchumi mtu mtakayeona mnatofautiana naye hamna budi KUMTANGULIZA??
Halafu unasikia mijitu inafurahia maneno ya waitara.Mwita ile kauli kaicopy na kuipaste toka kwa bosi wake.
Sasa polisi wakimkamata mwita,bosi wake anaponaje.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanachotakiwa sahivi intelijensia ya chadema ni kukusanya kila aina ya ushahidi,kila chembe ya viashiria ili vitumike siku moja kuwahoji hawa mafedhuli.Halafu unasikia mijitu inafurahia maneno ya waitara.
Neno 'kumtanguliza' lina maana zaidi ya moja unaweza kumtanguliza mtu akawa mbele ya mapambano,kumtanguliza kama chambo kumtanguliza kama mtu anayeaminiwa zaidi etc.Inafaa Jeshi la Polisi limkamate Mwita Waitara kwa mahojiano na aeleze alikuwa ana maana gani ya kusema kwenye vita ya uchumi mtu mtakayeona mnatofautiana naye hamna budi KUMTANGULIZA??
Najaribu kuimagine kama kauli hiyo ingetollewa na mpinzani, sijui ingekuwaje....Hili ni suala nyeti lakini kama kawaida litaishia hewani tu.Litakufa lenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Najaribu kuimagine kama kauli hiyo ingetollewa na mpinzani, sijui ingekuwaje....
Naamini hao Polisi wangeshamkamata mpinzani huyo na kumburuza "fasta" mahakamani
Mwita ile kauli kaicopy na kuipaste toka kwa bosi wake.
Sasa polisi wakimkamata mwita,bosi wake anaponaje.
Sent using Jamii Forums mobile app