Ni kwanini Jeshi la Polisi halijamkamata Mwita Waitara kuhusiana na sakata la Tundu Lissu?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,920
2,000
Kuna clip ambayo imeendelea kusambaa mtandaoni, ambayo bila shaka yoyote, sauti inayosikika humo ni ya Mbunge wa Ukonga na waziri mdogo wa TAMISEMI Mwita Waitara

Katika clip hiyo amesikika mbunge huyo akitamka kuwa kwenye vita ya uchumi, mnapoona kuna mtu anawakwamisha kwenye vita hiyo hamna budi KUMTANGULIZA mtu huyo!

Ni maneno ya hatari sana kwa usalama wa nchi yetu, kutamkwa na mwanasiasa, mwenye wadhifa mkubwa wa ubunge, ambapo anatoa hukumu kuwa mtu wa aina hiyo hana budi kuuawa!

Ni maneno ya hatari mno kutamkwa kwa kuwa tunavyojua ni chombo kimoja pekee kilichopewa dhamana ya kutoa hukumu hapa nchini, ambapo chombo hicho ni mahakama

Vile vile ni maneno ya hatari mno kwa kuwa hadi sasa ni zaidi ya mwaka mmoja na nusu, hakuna mtuhumiwa hata mmoja aliyekamatwa na kufanyiwa "interrogation" kuhusiana na tukio lile la kumiminiwa risasi zaidi ya 30 kwenye gari lake, kwa nia ya kumwua Tundu Lissu, ambapo hadi sasa anaendelea kuuguza majeraha katika hospitali nje ya nchi.

Ndipo hapo ninapojiuliza, je Jeshi la Polisi linasubiri nini kumkamata Mwita Waitara, kwa mahojiano ili limfikishe mahakamani kutokana na maneno yake ya UCHOCHEZI??

Kama Jeshi la Polisi halitamkamata Mwita Waitara, tutajua kuwa limepewa "maagizo" toka juu ili lisifanye hivyo!

Kwa kufanya hivyo ndipo Jeshi hilo linatengeneza visasi vya hali ya juu ndani ya Jamii ya watanzania, kwa kuwa itakuwa inafahamika wazi kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya CCM, wanaweza kuongea vitu vya hatari sana kwa nchi hii, lakini vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi haviwezi kuwakamata, kwa kuwa kundi hilo la watu ni UNTOUCHABLES!
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,920
2,000
Wenyewe walishasema mapema,faili la upelelezi limefungwa

Lakini kila kukicha wanamtaka dreva na Lissu mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kweli Jeshi letu la Polisi linafanyia kazi taarifa za kiintelejensia, basi ni lazima limkamate Mwita Waitara......

Kutomkamata huyo mtu tutajua kuwa Jeshi hilo linapewa "maagizo" toka juu ya namna ya kutekeleza majukumu yake, na siyo kuwa wanatimiza majukumu yao kwa weledi

Refer kauli ya Mkuu wa nchi ya "I WISH I COULD BE IGP"
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Kuna clip ambayo imeendelea kusambaa mtandaoni, ambayo bila shaka yoyote, sauti inayosikika humo ni ya Mbunge wa Ukonga na waziri mdogo wa TAMISEMI Mwita Waitara

Katika clip hiyo amesikika mbunge huyo akitamka kuwa kwenye vita ya uchumi, mnapoona kuna mtu anawakwamisha kwenye vita hiyo hamna budi KUMTANGULIZA mtu huyo!

Ni maneno ya hatari sana kwa usalama wa nchi yetu, kutamkwa na mwanasiasa, mwenye wadhifa mkubwa wa ubunge, ambapo anatoa hukumu kuwa mtu wa aina hiyo hana budi kuuawa!

Ni maneno ya hatari mno kutamkwa kwa kuwa tunavyojua ni chombo kimoja pekee kilichopewa dhamana ya kutoa hukumu hapa nchini, ambapo chombo hicho ni mahakama

Vile vile ni maneno ya hatari mno kwa kuwa hadi sasa ni zaidi ya mwaka mmoja na nusu, hakuna mtuhumiwa hata mmoja aliyekamatwa na kufanyiwa "interrogation" kuhusiana na tukio lile la kumiminiwa risasi zaidi ya 30 kwenye gari lake, kwa nia ya kumwua Tundu Lissu, ambapo hadi sasa anaendelea kuuguza majeraha katika hospitali nje ya nchi.

Ndipo hapo ninapojiuliza, je Jeshi la Polisi linasubiri nini kumkamata Mwita Waitara, kwa mahojiano ili limfikishe mahakamani kutokana na maneno yake ya UCHOCHEZI??

Kama Jeshi la Polisi halitamkamata Mwita Waitara, tutajua kuwa limepewa "maagizo" toka juu ili lisifanye hivyo!

Kwa kufanya hivyo ndipo Jeshi hilo linatengeneza visasi vya hali ya juu ndani ya Jamii ya watanzania, kwa kuwa itakuwa inafahamika wazi kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya CCM, wanaweza kuongea vitu vya hatari sana kwa nchi hii, lakini vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi haviwezi kuwakamata, kwa kuwa kundi hilo la watu ni UNTOUCHABLES!
Unafurahisha kweli yaani imkamate Ccm?
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Inafaa Jeshi la Polisi limkamate Mwita Waitara kwa mahojiano na aeleze alikuwa ana maana gani ya kusema kwenye vita ya uchumi mtu mtakayeona mnatofautiana naye hamna budi KUMTANGULIZA??

Hio ni ndoto sawa na kusema wamkamate Mollel,Mkurya wa dar alipewa teuzi kama fadhila ya kumtukana Mbowe na upinzani, ndo akamatwe na policcm.
 
Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
1,895
2,000
Halafu unasikia mijitu inafurahia maneno ya waitara.
Wanachotakiwa sahivi intelijensia ya chadema ni kukusanya kila aina ya ushahidi,kila chembe ya viashiria ili vitumike siku moja kuwahoji hawa mafedhuli.

Isije ikawa wanaishia tu kucheka na kuendeleza mijadala mitandaoni wakati hakuna hatua yeyote inachukuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,370
2,000
Inafaa Jeshi la Polisi limkamate Mwita Waitara kwa mahojiano na aeleze alikuwa ana maana gani ya kusema kwenye vita ya uchumi mtu mtakayeona mnatofautiana naye hamna budi KUMTANGULIZA??
Neno 'kumtanguliza' lina maana zaidi ya moja unaweza kumtanguliza mtu akawa mbele ya mapambano,kumtanguliza kama chambo kumtanguliza kama mtu anayeaminiwa zaidi etc.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,920
2,000
Hili ni suala nyeti lakini kama kawaida litaishia hewani tu.Litakufa lenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Najaribu kuimagine kama kauli hiyo ingetollewa na mpinzani, sijui ingekuwaje....

Naamini hao Polisi wangeshamkamata mpinzani huyo na kumburuza "fasta" mahakamani

Katika nchi moja ni jambo la hatari sana kuweka matabaka ya watu wanaoweza chukuliwa hatua na wengine kupewa "impunity" ya kutoweza shitakiwa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom