Ni kwanini Jeshi la Polisi halijamkamata Mwita Waitara kuhusiana na sakata la Tundu Lissu?

Kwa nchi ya Marekani mtu yeyote yule awe ndani au nje ya nchi anayetaka kuhatarisha nchi ya Marekani na raia wake huyo anatangazwa ni adui wa taifa na adhabu yake ni kuwawa yeye na kazazi chake
Rejea tukio la kuwawa kwa sadam hussein na kazazi chake hussein na Hassan
Tayari sadam alikuwa ni adui wa Marekani

Nchi jirani hapa wamefagia masheikh wote wana harakati pale mombasa kwa kauli tu za kichochezi na hakuna cha kesi wala maini
Kifupi hata ukisoma vitabu vya Mungu akitokea mtu mmoja anahatarisha maisha ya watu wengi kwa kauli za kichochezi auwawe ili taifa libaki salama..

Sent using Jamii Forums mobile app
Wajinga nao lazima muwepo hata uende peponi utawakuta.
 
Kuna clip ambayo imeendelea kusambaa mtandaoni, ambayo bila shaka yoyote, sauti inayosikika humo ni ya Mbunge wa Ukonga na waziri mdogo wa TAMISEMI Mwita Waitara

Katika clip hiyo amesikika mbunge huyo akitamka kuwa kwenye vita ya uchumi, mnapoona kuna mtu anawakwamisha kwenye vita hiyo hamna budi KUMTANGULIZA mtu huyo!

Ni maneno ya hatari sana kwa usalama wa nchi yetu, kutamkwa na mwanasiasa, mwenye wadhifa mkubwa wa ubunge, ambapo anatoa hukumu kuwa mtu wa aina hiyo hana budi kuuawa!

Ni maneno ya hatari mno kutamkwa kwa kuwa tunavyojua ni chombo kimoja pekee kilichopewa dhamana ya kutoa hukumu hapa nchini, ambapo chombo hicho ni mahakama

Vile vile ni maneno ya hatari mno kwa kuwa hadi sasa ni zaidi ya mwaka mmoja na nusu, hakuna mtuhumiwa hata mmoja aliyekamatwa na kufanyiwa "interrogation" kuhusiana na tukio lile la kumiminiwa risasi zaidi ya 30 kwenye gari lake, kwa nia ya kumwua Tundu Lissu, ambapo hadi sasa anaendelea kuuguza majeraha katika hospitali nje ya nchi.

Ndipo hapo ninapojiuliza, je Jeshi la Polisi linasubiri nini kumkamata Mwita Waitara, kwa mahojiano ili limfikishe mahakamani kutokana na maneno yake ya UCHOCHEZI??

Kama Jeshi la Polisi halitamkamata Mwita Waitara, tutajua kuwa limepewa "maagizo" toka juu ili lisifanye hivyo!

Kwa kufanya hivyo ndipo Jeshi hilo linatengeneza visasi vya hali ya juu ndani ya Jamii ya watanzania, kwa kuwa itakuwa inafahamika wazi kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya CCM, wanaweza kuongea vitu vya hatari sana kwa nchi hii, lakini vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi haviwezi kuwakamata, kwa kuwa kundi hilo la watu ni UNTOUCHABLES!
Kumtanguliza wapi?

..waitara kasema huyo mwenye kuwakwaza kwenye mapambano mnamuweka mstari wa mbele. Hajasema lolote tofauti. Kwenye vita kuna kufa au kupona kushinda au kushindwa..a luta continua a vitoria é certa..vinceremos
 
Nami nauliza, hawa wastaafu ninaowalipia pensheni zao kwa kodi na.jasho langu wanajisikiaje umoja na mshikamano walioujenga kwa miaka kumi kila mmoja kisha wao wanakaa kimya tu, wanayafurahia haya matamko?
Au wamesahau kuwa nao waliwahi kuwa raia namba moja? Waseme neno basi juu ya kauli hizi za kuchochea uvunjaji wa amani waliyoilinda kwa miaka yao kumi ya ulinzi wa amani!
Tena waseme kwa sauti na kwa umoja wao na siyo kwa kutegeana kwani nao ni raia wa kawaida lakini wenye sehemu ya heshima waliyobakishiwa. Semeni neno kwani kauli ya naibu waziri ni kauli ya serikali.
IMG-20170117-WA0003.jpg
 
Yeye kasema: "Kwenye vita ya uchumi, mtu akiwa anawasaliti ni kutumia njia ya jeshi la wapiganaji wa kivita, MSALITI anatangulizwa mbele ya haki"

Sasa tuje,
Nani anayepigana vita ya uchumi?
Wapiganaji wake ni akina nani?
Kamanda anaye ongoza kikosi ni nani?

Ila kuna mtu ameshawahi kujipambanua na kikosi chake kwamba anapigana VITA YA UCHUMI!

Sasa tumalize hivi:

Msaliti anajulikana na yuko kule ughaibuni anafanya mazoezi ya miguu!

Wanaopigana vita nao tunawajua sasa!

Conclusion:

Waliom-pyu-pyu-pyu TAL tushawajua.

Wamejitajaaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...Usicheze na njaa. jamaa huyo keshajitoa ufahamu . Nadhani wakati anaropoka hayo, alikuwa chupa kama kawaida yake.
 
Yeye kasema: "Kwenye vita ya uchumi, mtu akiwa anawasaliti ni kutumia njia ya jeshi la wapiganaji wa kivita, MSALITI anatangulizwa mbele ya haki"

Sasa tuje,
Nani anayepigana vita ya uchumi?
Wapiganaji wake ni akina nani?
Kamanda anaye ongoza kikosi ni nani?

Ila kuna mtu ameshawahi kujipambanua na kikosi chake kwamba anapigana VITA YA UCHUMI!

Sasa tumalize hivi:

Msaliti anajulikana na yuko kule ughaibuni anafanya mazoezi ya miguu!

Wanaopigana vita nao tunawajua sasa!

Conclusion:

Waliom-pyu-pyu-pyu TAL tushawajua.

Wamejitajaaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly Mkuu Malo Robi

Watu wasiojulikana sasa tushawajua!
 
Back
Top Bottom