Sababu Kumi Kwanini Sitaki Watoto
10)Hivi kwani lazima uniulize Kwanini? Mbona watu wakiongelea mipango ya watoto hawaulizwi Kwanini...
9)KIFO
Hivi wazazi tukasafiri tukafa huko watoto wangu itakuwaje? Yani ndugu wachukue watoto wangu wawalee wanavyojua wao? Wawapeleke kwenye ibada zao? Wafunge akili za wanangu? Wawafundishe ujinga? Aisee hapana...
8)Naogopa nitakuwa dissapointed. Nitakuwa na expectations mwanangu aweje lakini atakuwa tofauti... . Eg. Sitegemei mwanangu atumie uhuru wake kupractice bestiality. Imagine namwona mwanangu kwenye TV anaandamana apate haki ya hiyo kitu. Uwiii... Ndo tunaelekea huko jamani
7)Naogopa dunia si sehemu salama/atateseka/ataumia. Vipi akapata accident akaparalyse mwili mzima? Vipi akapatwa gonjwa la ajabu nikamzika? Vipi akauawa na wenye wivu? Vipi akafia kwenye earth quake? Au vita ya tatu ya dunia?
6)Naogopa hatokuwa na furaha. Naogopa nitakuwa confident kuwa nampa kila kitu, kama wazazi wengi wanavyodhani, lakini kumbe Kuna vitu nakosea. Naogopa nitamuathiri kisaikolojia bila kujua...
5)jamii ina mategemeo mengi mno. Naogopa anaweza akawa mtu wa ajabu. Naogopa atatengwa au kuchukiwa na watu. Naogopa watu watamuathiri na kumtesa mwanangu...
4)Mimi ni MVIVU mno. Sitaki majukumu. Hivi housegirl akinikimbia nitaishije? Sipendi kazi za nyumbani. Naweza nisile nikakaa nascroll tu. Si wanangu watapata kitapia mlo?
3)Mimi ni mama tayari. Wazazi wengi ni wazazi Jina tu. Watoto wao wanakua peke yao. Hawawajui watoto wao. Najali wote wanaoniambiaga shida zao wanazoshindwa kuwaambia wazazi wao..Saa nyingine nahisi nawawazaga Hawa watoto kuliko wazazi wao.
2)Watoto wengi wanahitaji mama. Mayatima kibao. Utabeba watoto wazuri kibao hadi utachoka. Wote wanahitaji kutunzwa na attention. Umama tosha.
1)Kusema ukweli sababu kubwa ni kuwa Sina uwezo. Mwanangu asikie shida kwenye radio tu. Nataka kuzaa kumpa kiumbe experience ya maisha. AiEnjoy. That's what life is all about. Sio kuzaa ili tuone na wewe una mbegu. Me ilikuwaga nizaliwe kwenye familia ya kifalme sijui ikawaje. Lakini kosa hilo lisijirudie kwa mwanangu
***) lakini bwana, huyu mwanaume akisema tu, mayai yangu hayatosubiri siku za hatari. Yatatoka Saa hiyo hiyo tayari kupandikizwa. Nahitaji tu mtu atakayenihakikishia maisha. Mengi nayoyaona sio maisha ni chemical reactions tu.