John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 110
- 210
Ni kwa vipi Yesu Kristo anaombea wanadamu mbinguni
Ni wapi maandiko yanasema Yesu anaombea wanadamu
Katika maandiko, Warumi 8:34, yanasema,
“Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea”.
Pia, 1Yohana 2:1, inasema, “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye mwombezi kwa Baba.
Hivyo, ni kweli Neno la Mungu linasema kuwa Bwana wetu Yesu Kristo anatuombea.
Ni vizuri kuzijua lugha za kiroho na namna ya kuzitafsiri, vinginevyo itatuwia vigumu
kuielewa biblia, na hata wakati mwingine kujikuta tunaabudu sanamu kwa kushindwa kuzipambanua lugha za kiroho.
Maandiko yanasema KRISTO ameketi kutuombea, hata tufanyapo dhambi.
Kwa mfano kuna mahali Bwana YESU alisema mtu asipoula mwili wangu, na kuinywa damu yangu hana uzima ndani yake (Yohana 6:53).
Tukiuchukua huo mstari kama ulivyo na kwenda kutafuta mwili wa Bwana kama nyama, na damu yake kama ilivyo na kuinywa, tutakuwa tumeshindwa kutafsiri vyema lugha ya biblia, na hivyo tutakuwa tumefanana na waganga na wachawi walao nyama na kunywa damu.
Lakini kama tukiweza kuelewa maana ya mwili wake Bwana Yesu na damu yake kuwa ni ule mkate na kile kikombe, sawasawa na (Mathayo 26:26-27), tutakuwa tumeenda sawa sawa na Neno la Mungu.
Kwa msingi huo, tuwe tayari kujifunza ni kwa namna gani Kristo anatuombea kwa Baba.
Katika kitabu cha Warumi 8:34, tulisoma kuwa KRISTO ndiye anayetuombea.
Hebu twende kwenye: Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO MWENYEWE HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA. 27 Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu”.
Katika ule mstari wa 34 tumesoma kuwa ni BWANA YESU ndiye anayetuombea, lakini katika mstari wa 26, ndani ya sura hiyo hiyo, tunasoma kuwa ni ROHO MTAKATIFU ndiye anayetuombea.
Hapa, swali ni: yupi kati ya hawa wawili anayetuombea kwa Baba, ni Roho Mtakatifu au ni Bwana YESU?
Hebu tuangalie katika kitabu cha 2Wakorintho 3:17: “Basi Bwana ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru”.
Hapo anasema lakini “Bwana” (yaani YESU) ndiye “Roho” (yaani Roho Mtakatifu). Kumbuka hapo Roho imeanza kwa herufi kubwa kuwakilisha Roho Mtakatifu.
Hivyo, kulingana na hayo maandiko, ni sahihi kabisa kusema BWANA YESU ndiye ROHO MTAKATIFU, na Roho mtakatifu ndiye Bwana YESU.
Kwa hiyo mahali popote asemapo Roho Mtakatifu, ni Bwana YESU ndiye amesema.
Ndiyo maana utaona katika kitabu cha Ufunuo, Mlango wa 2 na wa 3, katika ujumbe kwa yale makanisa saba, utaona ujumbe unaanza na YESU ANASEMA, na unamaliza na ROHO AYAAMBIA MAKANISA, ikiwa na maana kuwa, Roho ndiye huyo huyo Bwana. Hivyo, Roho Mtakatifu akiomba ni Bwana ameomba.
Kama Bwana YESU ndiye Roho Mtakatifu, je huyo Roho Mtakatifu anatuombeaje sawa sawa na Warumi 8:26?
Roho Mtakatifu (ambaye ndiye Bwana mwenyewe) hatuombei kama sisi tunavyoombeana. La hasha. Yeye anaomba ndani yetu. Maana yake ni kwamba, pale sisi tunapoomba, yale maombi yetu anayachukua na kuyapeleka mbele za Baba, katika lugha nzuri zaidi, na katika maelezo mazuri zaidi.
Lakini si kwamba tumelala au tunacheza, tunatenda dhambi, au tunafanya mambo yetu mengine, basi wakati huo huo yeye kule anatuombea, Hapana, sivyo. Hiyo si tafsiri yake kabisa.
Kwa ujumla, ni kwamba jinsi Bwana YESU anavyotuombea ni kwa jinsi ya Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu anachukua yale maombi yetu na kuyapeleka kwa Baba kwa lugha kamilifu zaidi.
Hivyo, kamwe mtu asiwaze kuwa Bwana YESU yupo mbinguni mbele za Baba, akisali kwa ajili yetu, hata tukitenda dhambi. Bali, ni kwa njia ya Roho wake mtakatifu ndani yetu, na kupitia maombi yetu wenyewe, ndipo anapotuombea.
Kwa hiyo, OMBA, ILI MAOMBI YAKO YAPELEKWE MBINGUNI.
Kwa nini tunajifunza haya
Hii ni kwa sababu zipo imani zilizoanzishwa na ibilisi zisemazo kuwa “hatuna haja ya kuomba, kwa sababu Bwana YESU yupo mbinguni anatuombea usiku na mchana”.
Kamwe usidanganyike na hayo mafundisho kwani ni mafundisho ya adui, ibilisi. Tusipoomba, na Roho Mtakatifu hawezi kuomba, na Roho Mtakatifu asipoomba, ni Bwana hajaomba.
Lakini tuombapo, Roho Mtakatifu ni kipaza sauti chetu kwa Baba. Kwa hiyo maombi ni lazima.
Tuelewe vizuri kuhusu maombi
Kimsingi, hakuna mtakatifu yoyote aliyekufa au aliyenyakuliwa anayetuombea. NI YESU TU PEKE YAKE, kwa NJIA YA ROHO WAKE MTAKATIFU, ndiye anayetuombea. Hivyo, Mariamu hawezi kutuombea, wala Eliya, wala Musa, wala Henoko, wala mtu mwingine yoyote aliye hai, wala aliyekufa. Mungu wetu si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai (Marko 12:27)
Kwa hiyo lililo kubwa na la msingi sana, ni kutafuta Roho Mtakatifu kwa sababu ni kwa kupitia huyo, ndiyo maombi yetu yatafika na kukubaliwa.
Tukumbuke pia kuwa, kulingana na biblia (Warumi 8:9), mtu asiyekuwa na Roho Mtakatifu, huyo si wake. Hivyo, okoka, ili uwe na Roho Mtakatifu ndani yako.
Roho Mtakatifu, ndiye Yesu mwenyewe, hatuombei kama sisi tunavyoombeana. Yeye anaomba ndani yetu. Maana yake ni kwamba, pale sisi tunapoomba, yale maombi yetu anayachukua na kuyapeleka mbele za Baba, katika lugha nzuri zaidi, na katika maelezo mazuri zaidi.
Hivyo basi, omba, ili Yesu apeleke maombi yako mbinguni.