Mungu tu ndio hazomewi..
Nimewasikia wajumbe mbalimbali wa CCM akiwemo pia Mwenyekiti Samwel Sita wakijitahidi kutoa tahadhari zenye sura za vitisho kwa wajumbe wanaowahisi watamzomea Mh Rais JK atakapohutubia bunge siku ya ijumaa. Sita kadai kuna kamera zaidi ya 13 ndani ya bunge kwa ajili ya kuwanasa wajumbe watakaofanya fujo na kwamba wataangalia uwezekano wa kuwatoa kwenye public media.
Baada ya hoja zilizoshiba za Mh Warioba, inaonekana CCM wanajua JK hatakuwa na hoja yeyote ya maana kumpinga Warioba na tume yake, na kwa sababu hiyo wameshikwa na hofu kuwa akijifanya kukosoa tume tu anaweza kuambulia aibu ya kuzomewa. sasa wanajipanga kuwatisha wajumbe wasiexpress hisia zao zidi ya mipasho badala ya kujibu hoja zitakapoanza dhidi ya tume ya warioba.
Tunamsihi Mh Rais kama ijumaa atapenda kumjibu Warioba na tume yake, basi ajikite kwenye hoja alizozitoa Mh Jaji Warioba.
TBC sasa hivi asubuhi wako na Lipumba na Mzanzibar na wanazungumzia kuhusu serikali 2 au 3 kwa nini wanashindwa kusema vipi tuwe na serikali ya zanzibar na tusiwe na serikali ya tanganyika? kuna ulazima gani wa kuwa na serikali ya Zanzibar wakati tuna serikali ya muungano? hilo ndilo tatizo kubwa, na kama hilo sio suala la msingi kupita yote kwa nini ccm wameliwekea msimamo?mbona hawajawekea msimamo hayo masuala mengine wanayosema ni ya msingi kama Ardhi, elimu,na mshikamano. kiukweli la msingi kupita zote ni hili la haina ya muundo wa serikaliNimewasikia wajumbe mbalimbali wa CCM akiwemo pia Mwenyekiti Samwel Sita wakijitahidi kutoa tahadhari zenye sura za vitisho kwa wajumbe wanaowahisi watamzomea Mh Rais JK atakapohutubia bunge siku ya ijumaa. Sita kadai kuna kamera zaidi ya 13 ndani ya bunge kwa ajili ya kuwanasa wajumbe watakaofanya fujo na kwamba wataangalia uwezekano wa kuwatoa kwenye public media.