Tetesi: Ni kosa makampuni ya minada kufunga gari kwa "Wrong Parking"

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,045
20,408
Tabia ya kufunga funga Magari na kudai Tshs 50,000 hii hapa, jisomee.

Kwa wapenzi wa sheria, kuna kesi tamu hapa ya Vigu Trading Co. Ltd dhidi ya TANROADS, Yono, Inland Transporters Ltd (breakdown) na Mwanasheria Mkuu (kwa sababu ni kesi ya serikali)

Mshtaki lori lake liliharibika mbele kidogo ya Chalinze akiwa katoka Lusaka anarudi Dar.

Wazee wa Yono wakamkamata wrong parking, wakamvuta na break down na kumtaka alipe Tshs. 166,000/-

Ilikuwa 29/11/2013 hiyo. Mwenye lori akawasusia na kuwashtaki.

Kesi ameshinda 16/12/2019 na ikaamriwa alipwe Tshs. 150,000,000/-, na gari lake arudishiwe.

Miaka sita ya kutafuta haki, sio mchezo. Ndo hapo watu sheria inapowashindaga.

Kidokezo muhimu ni picha za eneo la tukio alipiga kwa simu, halafu simu akapoteza. Mahakama ikazikataa picha zake alizoprint maana ilitakiwa aambatanishe na simu iliyotumika kupiga, au aambatanishe na loss report.

Na katika madai yake ya pesa hakuambatanisha na risiti au ankara zozote kwa hiyo madai ya fidia mahususi yakapigwa chini. Hiyo fidia ya milioni 150 amepewa kama fidia ya jumla.

Kilichompa ushindi ni kwamba:

Naombeni msome hiyo kesi nliyoweka hapo japo ipo kwa lugha ya Mabeberu ila mtaelewa, tu, huyo jamaa gari yake ilikamatwa ikiwa imepaki chalinze, wakalivuta na kumpiga faini, akagoma na kufungua kesi, amelipwa milioni 150 ila angelipwa hata bilioni sema alipiga picha gari lilipofungwa na kuvutwa, na simu na picha zikapotea sasa alishindwa kutoa ushahidi mahakamani.

1. Sheria ya TANROADS (Roads Act, 2007) haina kosa la wrong parking

2. Sheria ya Usalama Barabarani inaruhusu wrong parking ukipata dharura (ambayo iko nje ya control ya dereva).

3. Mkataba wa Yono na TANROADS unamtaka Yono asivute gari ambalo liko wrong parking kabla masaa sita hayajaisha (kwa maeneo ya mjini) na masaa 24 kwa maeneo ya kijijini. Yeye alilivuta kabla masaa sita hayajaisha.

4. Mkataba wa Yono na TANROADS haumruhusu Yono kuuza kazi ya kuvuta gari ambalo liko wrong parking kwa kampuni au mtu mwingine.
 

Attachments

  • Wrong_Parking_against_TANROADS,_Plaintiff_awarded_Tshs_150M_.pdf
    245 KB · Views: 31
Ila hawa jamaa wakikukamata hawana maelewano wao ni kudai hela tu,nilishuhudia siku moja dada moja na IST yake ile amepaki sehemu anakusakusanya kusanya pochi zake ili ashuke jamaa huku wanafunga tairi,ile kushuka jamaa tayari wanamkomalia yuko wrong parking ,nikaacha ule mtanange siju uliishaje.
 
Ila hawa jamaa wakikukamata hawana maelewano wao ni kudai hela tu,nilishuhudia siku moja dada moja na IST yake ile amepaki sehemu anakusakusanya kusanya pochi zake ili ashuke jamaa huku wanafunga tairi,ile kushuka jamaa tayari wanamkomalia yuko wrong parking ,nikaacha ule mtanange siju uliishaje...
Nchi isiyofuata Sheria, kwenye kituo cha Daldala sheria inataka ukae mita 5 toka sehemu inapopaki Daladala, kwa uhalisoa, hizo mita 5 unakuta bodaboda zimejaa na Wamachinga wamepanga bidhaa, utapaki wapi kama si kwenue daladala, hii nchi imekuwa ya kishamba sana, nafikir sehemu pekee ambayo machinga hawajapanga bidhaa ni kwenye vyoo tu, ila hata wakipanga huko tulivyo wajinga tunanunua
 
Kuna wale TARURA na Noah yao hapa Dar. Wasubiri tu.
Usihofu, hakikisha toka wanafunga gari yako, unapica picha, matukio yote then rusha kwa group ya wasap, tafuta wakili, fungua kesi, utakula hela sawa na Okwi alokuwa anakula pale Msimbazi
 
Back
Top Bottom