Ni kosa kuharibu alama za mipaka (beacons)

Obuzeva_Og

New Member
Sep 23, 2020
2
0
Kwa mujibu wa Sheria ya Upimaji na Ramani Sura Na. 324 ya Mwaka 1957 na kama ilivyorekebishwa Mwaka 1997, ni kosa la jinai kwa kuharibu au kusogeza alama za mipaka. Chini ya Sheria hii Vifungu Na.11 na Na.12 vinatoa adhabu ya Faini au kifungo au Vyote kwa pamoja na kugharamia alama iliyoondolewa pamoja na kazi ya Upimaji itakayofanywa kurudishia alama hiyo ya Mpaka iliyosogezwa.

Msimamo wa Sheria kuhusu Uharibifu Wa Alama za Mipaka Ya Viwanja na Mashamba

1. Mtu yeyote ambaye kwa matashi yake mwenyewe bila kuidhinishwa na Sheria (Jambo ambalo litambidi athibitishe yeye Binafsi) ataondoa, ataharibu au atahamisha au atasababisha Uondoshaji, uharibifu au uhamisho au akibadili makao ya, au akiumbua, akitengua, akifuata au kuvunja au akitimiza Uumbushaji,Utengo, Ufutaji au Uvunjaji wa Alama yeyote, atakuwa na hatia chini ya Sheria hii, na anastahili adhabu ya Fedha za Kitanzania Shilingi laki saba na Ishirini Elfu (720,000/=) au kifungo kisichozidi miaka miwili au adhabu zote hizo mbili, na baraza linaweza kumwamuru kulipa gharama ya kurudisha alama hiyo pamoja na gharama ya Upimaji utakao andamana na Urudishaji huo.

2. Hakuna chochote katika kifungu hiki kitakachoeleweka kama kitamuacha mtu yeyote asishtakiwe au asihukumiwe chini ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) au chini ya Sheria yeyote kuhusu kitendo chochote au ukosefu wa kutenda kama ilivyoelekezwa katika sehemu hii.

3. Si ruhusa kwa Mtu kufanya kazi yeyote ambayo huenda ikaharibu alama za maboya (Trigonometric Station) au alama kuu za kina cha urefu uliolinganishwa na usawa wa Bahari (Fundamental Bench Marks) au kutenda kazi karibu na alama hizo muhimu itakayohatarisha vitu hivyo vilivyotajwa.

Mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha masharti ya kifungu hiki cha Sheria atakuwa amevunja sheria hii na anastahili faini ya Fedha za Kitanzania Shilingi zisizozidi miaka miwili au kuhukumiwa adhabu zote mbili.

Manufaa Ya Kutunza Alama za Mipaka Ya Viwanja au Mashamba.

Alama za Mipaka zikitunzwa wakati wote miliki inapodumu zitaepusha migogoro ya Mipaka/Ardhi.

Kuepuka Mashauri mahakamani; kwa sababu kama mtu atasema umezidisha Kiwanja chako au Shamba utaweza Tumia hati yako kama shahidi.

Alama hizo ni Chanzo ca Upimaji Mwingine Mpya au wa kurudishia alama zilizoharibika.

Ili kuepusha Usumbufu wa kupelekana Mahakamani ningependa kukushauri Mtumiaji Ardhi tumia Ardhikama vile Ulivyoelekezwa na mamlaka husika kwa maana madhara ya kupuuzia maagizo haya yanaweza kusababisha mabo mengi kutokea kama vile chuki kati ya Mtu na mtu na pia kulipa kiasi kikubwa cha Faini pamoja na Kufungwa Gerezani kitu kinachoweza kusababisha ukarudisha Nyuma Maendeleo yako, Familia, pamoja na Taifa kwa Ujumla.
 
Back
Top Bottom