Ni kitu gani kimekusukuma kufanya ujenzi?

baby zu

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
544
1,000
Sasa wakikutana na muhaya wangu ,vinaumana,dharau,kujikweza,shombo zote mdomoni zipo,
Mwisho wa siku mwenye nyumba anachemka utasikia, " kodi yenu ikiisha muhame, sipokei tena kodi kutoka kwenu"
Hahahaha mimi pia niliwahi kupigwa notice miez mitatu kabla nkamwambia wala usingeangaika kunipa maana nilikua siezi kuendelea kukaa hapa na nkiondoka kuacha kodi utaina nimekuogopa nilikaa niakahama saa tano usiku ya tar ya mwisho wa mkataba.

Nadhan siku hyo alikua ana hamu kesho yake inikute kwake akawa haoni kama nahama nikaondoka zangu usiku mwingi. Mzaramo yule yani sijawahi tibuana na mtu maisha yangu lkn yule mama mikono juu
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,082
2,000
Habari za majukumu mabibi na mabwana!

Katika harakati hizi za maisha watu hupitia mengi sana, Kuna kipindi pesa inakubali, Kuna kipindi unachapika mpaka unajuta kuzaliwa. Anyways twende kwenye jambo la msingi...
Binafsi nimepanga kwa miaka lukuki na nimekuwa nilibadilisha maeneo mengi jijini, nimeishi Sinza, Magomeni, K'nyama, Ilala na Kinyerezi. Kwasasa ndiyo nimeanza ujenzi na nipo katika hatua ya kupaua, ni nyumba yangu ya kwanza.
Bado hujavunja record yangu
 

baby zu

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
544
1,000
Binafsi nimepanga kwa miaka lukuki na nimekuwa nilibadilisha maeneo mengi jijini, nimeishi Sinza, Magomeni, K'nyama, Ilala na Kinyerezi. Kwasasa ndiyo nimeanza ujenzi na nipo katika hatua ya kupaua, ni nyumba yangu ya kwanza.
Bado hujavunja record yangu
Hahahahahahah ntamani kujua record yako
 

keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,658
2,000
Habari za majukumu mabibi na mabwana!

Katika harakati hizi za maisha watu hupitia mengi sana, Kuna kipindi pesa inakubali, Kuna kipindi unachapika mpaka unajuta kuzaliwa...
Swali lako halina tofauti eti ni Nini kilisukuma uwe unakula vizuri ama nimekosea.
 

Fibanochi

JF-Expert Member
Jun 28, 2018
416
1,000
Bonyokwa 1
Kibo3
Kibangu1
Kwa Azizi Ali 2
Temeke1
Sweet corner 1
Kino 3
Tabata 2
Manzese, mburahati...yaani acha tu
Duuuh we mzee umekaa maeneo hatarishi ya kutosha, inaonekana kash kash za uswahilini unazijua mwanzo mwisho! Sweet corner, Temeke, Manzese, Mburahati sehemu hatari sana hizo, umebakiza mwananyamala tu.
 

Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
5,990
2,000
Kitendo cha kuwa na amani unapopata mahali pa kudumu kimaisha. Choo chako na familia, labda wageni wangu watatumia choo chetu. Vyoo katika nyumba za kuganga ni shida.
 

Fibanochi

JF-Expert Member
Jun 28, 2018
416
1,000
Swali lako halina tofauti eti ni Nini kilisukuma uwe unakula vizuri ama nimekosea.
Hapana kula vizuri ni suala la mtu binafsi sana linalotegemea na uelewa wa mtu juu wa umuhimu wa suala hilo, halina msukumo sana tofauti na suala la kujenga.

Unaweza ukawa na pesa za kutosha lakini ukala hovyo na kula vizuri hapa hapa ni tafsiri ya mtu mmoja mmoja, kula chips kuku broiler pembeni ukiwa na soda kwako inaweza kuwa ni kula vizuri lakini kwa mwingine kula vizuri ni kula dona kiasi na spinach pembeni kukiwa na parachichi.

Kula vizuri kunaweza kusihitaji gharama kubwa, lakini obvious ujenzi wa nyumba tutahitaji gharama za kutosha.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,082
2,000
Duuuh we mzee umekaa maeneo hatarishi ya kutosha, inaonekana kash kash za uswahilini unazijua mwanzo mwisho! Sweet corner, Temeke, Manzese, Mburahati sehemu hatari sana hizo, umebakiza mwananyamala tu.
Mwananyamala tena hapo ndio nimekaa miaka 10


Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,082
2,000
Ulikua unafukuzwa ulozi au?
nilikuwa kwenye utafiti

 

Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,726
2,000
Madogo walikuwa na dharau sana!! niliamua tu nikajenga kila MKoa nyumba tena kwa haisra mbaya!! nikapangisha zote!! na kazi nikaacha sasa najenga south!! nimewakomesha!!
 

Kyokola

JF-Expert Member
Sep 5, 2014
1,409
2,000
Mke wangu ana gubu, na dharau,anatunishiana misuli na wenye nyumba,yaani kila nyumba tukipanga ile kodi ya kuigilia ndio huwa ya mwisho.

Tukaona tujenge ya kwetu/ zetu.sasa hivi nae ni land lord na upole umekuja ghafla.
Nae eti anachukia wapangaji wakorofi.

malipo ni hapa hapa duniani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom