My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,930
- 13,335
Naikumbuka vyema Sana hiyo siku, niliwasili Dodoma majira ya saa tisa alasiri na kisha mimi na dereva wangu tukapaki ktk hoteli moja maarufu sana kwa kuchoma nyama ya mbuzi.
Tulikuwa tunatoka Dar tukisafiri kwenda kanda ya ziwa, ndani ya gari kulikuwa na pikipiki za biashara za mitumba( Tulikuwa na Fuso).
Tukiwa tunakula kando yetu walikaa wazee watatu na kijana mmoja wakiongea kwa huzuni sana. "Haiwezekani bwana, huyu kaonewa tu." Mwingine akasema,"hapa imeshakula kwetu tayari"
Baadae tuliona makundi mengi ya watu yakiwa yamejaa huzuni, hakuna aliyekuwa na furaha. Tulianza safari saa 12 jioni na bado tuliendelea kuona makundi ya watu barabarani yakiwa na huzuni.
Hadi leo huwa najiuliza ni tukio gani lilitokea Dodoma siku ile?