Ni kipindi gani ulitamani dunia ipasuke uingie

Ni kipindi gani ulitamani dunia ipasuke uingie

Elly255

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2017
Posts
883
Reaction score
1,432
Kwa upande wangu nakumbuka ilikuwa 2003 kama sikosei niko primary. Siku moja jioni kwenye saa 12 jioni naenda zangu kuchota maji bombani karibu na mto, si nikaingiwa na tamaa ya kula muwa. Ikabidi nivamie shamba moja kuiba, aise kumbe mlinzi aliwepo akanikamata na kunifunga kamba.

Hapo niliwaza mzee alivokuwa mkatili anapiga nusu kuua kwakweli nilitamani dunia iishe. Nilipelekwa home mida ya saa 3 usiku nilipigwa sana na mzee sitasahau. Bado kesho yake nilichelewa kuwahi namba shule nikapigwa tena dah!

Vipi kwa upande wako inaweza kuwa mahusiano, pengine uliachwa au ulifumaniwa au uliiba kama mimi [emoji16][emoji16][emoji16].

Karibu ufunguke
 
Kipindi ambacho timu yangu kipenzi YANGA ilipofungwa bao tano kwa bila na Simba hiki ni kipindi ambacho nilitamani dunia ipasuke nizame maana nilijigamba sana mtaani
 
Siku nilikuwa sijaandaa lesson plan na scheme of work nafundisha nikiwa field mara paap assessor akaja bila ya Mimi kufahamu sipendi kukumbuka ila nilihisi mstari wa Moto umepita tumboni
Hahahahaha noma sana hiyo
 
Siku nilikuwa sijaandaa lesson plan na scheme of work nafundisha nikiwa field mara paap assessor akaja bila ya Mimi kufahamu sipendi kukumbuka ila nilihisi mstari wa Moto umepita tumboni
Pole sana mkuu, i hope haikuleta athari kwenye kibarua chako
 
Za kitoto zote hizo
Siongei kwa kirefu ila kipindi kigumu nilichopitia ni kufumaniwa na mke wa mtu. Full stop, unaweza kunywa sumu ufe
Ndo tafsiri halisi ya kusema mke wa mtu sumu. Dont try at home or wherever.
 
Nilikaita kaje ghetto kaniage vizuri kesho nasafiri, Kakazingua. Nikaamua nimuite mwenzie, akakubali. Tupo ndani dak mbili nyingi cm inaita "njoo ulipe bodaboda nipo nje APA".
Stor yako inaelekea ni tamu lakini hujaimalizia
 
Kuna likizo nilienda kumtembelea sister nikiwa form three hivi nikamtongoza mtoto wa jirani

Ile saa mbili usiku muda wa kula tupo mezani familia yote pmj na shem.

Mara ghafla mlango unagongwa kufunguliwa akaingia yule binti ameambatana na mama ake na baba ake binti aliulizwa ni yupi anayekusumbua akaninyoshea mkono mimi....nilichambwa sister anajua kuchamba asee nilishambuliwa kila aina ya maneno mabaya.
Iyo siku niltamani nipae angani
 
Siku nilikuwa sijaandaa lesson plan na scheme of work nafundisha nikiwa field mara paap assessor akaja bila ya Mimi kufahamu sipendi kukumbuka ila nilihisi mstari wa Moto umepita tumboni
Hahahaaaaa. Ilikuwaje mkuu. Afu jina lako mkuu we muhaya au.
 
Nilikaita kaje ghetto kaniage vizuri kesho nasafiri, Kakazingua. Nikaamua nimuite mwenzie, akakubali. Tupo ndani dak mbili nyingi cm inaita "njoo ulipe bodaboda nipo nje APA".
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom