Ni Kipi Kivumiliwe Kwenye Mahusiano?

Baby M

JF-Expert Member
Apr 18, 2012
1,037
415
mmeshindaje wana JF.

kwani kwenye mahusiano ya kimapenzi unatakiwa uvumilie mangapi jaman na kama hakuna kipimo kipi ukifanye tofauti kukabiliana na hali zenye utata?

nina rafiki yangu nilisoma nae chuo, tumekua marafiki wa karibu sana ananijua na mimi namjua,
wakati tupo chuo boy friend wake alimpa mimba akaikataa kwa sababu alihisi si yake as alikua akijua story kwamba dem wake alikua ana wanaume wengine jamaa alivyokua nje ya nchi, na ni kweli alikua aki date wakati jamaa akiwa nje(those cheat chart na nyegez) ila jamaa ake akirudi she keep it strictly uhusiano wake na jamaa ham`mix,.

well akajifungua mtoto likatokea copy paste na jamaa, baada ya mwaka boifrend akaamua rudi baada ya kushauriwa kwamba kweli toto ni lake bila hiyana akakubali kwa hiari yake wakasameheana akaamua muoa shosti yangu.

after ndoa ndani ya ka mwezi na nusu hapo shost ana mimba ya miez saba ya jamaa coz walirudiana kabla ya kuhalalisha ndoa kanisani, waligombana jamaa akambonda vizuri sana mkewe, aling`oa rasta kichwani ngumi za kushosha skio moja liliacha kusikia kwa muda makofi ya kutosha, aliumwa na kuugua wiki mbili,, alishauriwa avumilie ndito maisha ya ndoa, kwani yeye alitaka kuondoka kwa huyo mme.

sasa bidada hivi karibuni anakua analalamika tuu kuhusu ndoa, mara hana hela, stress and upweke wamsumbua, mara ataniambia nimtafutie namba za ma x wake labda na yeye atapata faraja, kwa sasa yupo kwao anahisi mumewe ana toka nje ya njia kuu.
mara ataniambia huyu mwanaume aliye nioa simjui tena sio yule aliye kuwa boifrend m`sweet, wakati mwingine mimi naweza mkuta jamaa yake kwenye kumbi za starehe usiku mnene na ataniambia nisimwambie mkewe kama nimemuona hapo na wanakaa nyumba moja.

yeye shost yangu siku hizi hunishauri mimi ambaye sijaolewa kwamba niwe mwangalifu kumjua mwanaume wangu sababu yeye anayopitia ni mazito, na ana miaka 25 sasa with two kids, chuo hakueza maliza mwaka wa tatu hadi sasa hana cheti anapata wakati mgumu kuomba ajira tho anajituma na biashara zake za hapa na pale.

leo kaamka asubuh ananiambia nimsaidie tafuta nyumba ya kukaa na watoto wake sababu alishaondoka kwa mmewe ako kwao, alikua akiniambia mda mrefu nikajua utani nikiamini atarud kwa mzazi mwenzie. hao ni watu wenye ndoa ya mwaka 1 na miez 4 tuu.

now najiuliza sababu roho inaniuma kuona rafiki yangu ndoa yake ipo matatani japo naamini siku kitaeleweka warudiane, je ndoa za siku hizi zinatengana ndani ya mda mfupi je ni wanandoa kukosa uvumilivu or kitu gani jaman, sababu natishika hata mimi kuolewa naona sijui ni kipi nijipange kuvumiliana humo ndani ya ndoa. ukizingatia kila mtu anamapungufu yake.

mawazo na uzoefu wenu pliz.
 
kwa wewe usiogope yatokanayo....japo wengi wanalalamika na ndoa ila pia wapo wanaofurahia ndoa zao..Just pray Mwombe Mungu akupe mume ambaye mtafurahia ndoa na sio matatizo....

Huyo rafiki yako kama anadhani kumpenda mume ni kuzaa mwambie akazane....
 
Kipindi ana chit chart na nyegezi mpenz wake akiwa nje ulikuwa haumshauri kutulia,saizi mambo yamekuwa magumu anakuomba umtafutie namba za ma x wake,huyo mwanamke si mzima na aliingia ndoani kichwa kichwa na kwa miguu yote,badala ya kufikir namna gani atayakabili hayo yanayomsibu na kuhangaika na watoto wake yeye anawaza ma x wake ndo wafanyeje sasa? hata ukimpa namba za ma x nani atakubali saizi mtu ana watoto wawili?
 
Rafiki yako na bwana wake wote ni mental case...utajichosha na kutuchosha kujadili....go get your life together..

The Boss wa kipindi hiki ni tofauti na niliyekua namsoma kipindi cha nyuma kabla sijiunga na JF,wasikuizi amekua harsh,hana huruma ushauri wake niwahapo kwa hapo
 
Last edited by a moderator:
Kipindi ana chit chart na nyegezi mpenz wake akiwa nje ulikuwa haumshauri kutulia,saizi mambo yamekuwa magumu anakuomba umtafutie namba za ma x wake,huyo mwanamke si mzima na aliingia ndoani kichwa kichwa na kwa miguu yote,badala ya kufikir namna gani atayakabili hayo yanayomsibu na kuhangaika na watoto wake yeye anawaza ma x wake ndo wafanyeje sasa? hata ukimpa namba za ma x nani atakubali saizi mtu ana watoto wawili?

Hivo tukiwa na watoto tukiachwa ndio basi teeeenaaa eeehhh? pole ya sisi jamani tujenge nyumba zetu japo wakati mwingine ata uweke zege wabomoaji wengi
 
The Boss wa kipindi hiki ni tofauti na niliyekua namsoma kipindi cha nyuma kabla sijiunga na JF,wasikuizi amekua harsh,hana huruma ushauri wake niwahapo kwa hapo

Naunga mkono hoja, The boss rudia hali ile ilikuwa inakupendeza sana na inafanana na Avatar
 
Hivo tukiwa na watoto tukiachwa ndio basi teeeenaaa eeehhh? pole ya sisi jamani tujenge nyumba zetu japo wakati mwingine ata uweke zege wabomoaji wengi
Hilo linajulikana wazi kuwa mwanamke akizaa ule mvuto wa mwanzo unapungua sasa yeye badala ya kuhangaika na hao watoto wake ambao kimsingi yeye ndiye aliyesababisha hiyo hali bado anaulizia ma x hivi kuna x atatamani kuwa naye tena? kwanza status aliyonayo tayari ni kicheche na mume wake alimrudia baada ya kugundua ana mtoto wake
 
Yale ni maisha yao,wewe una maisha yako,usiogope,cha kufanya uwe mtu mwema utapata wa kufanana nawe,kama nawe si mwema taraji kupata kama wa rafiki yako.
 
Ndo shida ya kuolewa na mtu asiyekupenda. Inaonekana Mwanaume alimuoa kwa sababu tu alimzalisha.
 
Back
Top Bottom