Ni kipi kimeikumba Dunia yetu?

KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
8,024
16,490
Wana JF,

Wenzangu yawezekana tupo tunaendelea na maisha yetu ya kawaida ila kwa jinsi mimi nionavyo kuna tatizo zito kwenye uchumi wa Dunia na kwa hatua tatizo hili lilipofikia kuna uwezekano wa mifumo ya fedha iliyopo ikashindwa kabisa kufanya kazi hali ambayo itazusha taharuki Dunia nzima.

Nimeona Federal reserve kule Marekani wameongeza interest rate kidogo sana lakini matokea yake hisa za makampuni mengi zimeporomoka,indexes zimeporomoka,crypto kama bitcoin imeshuka thamani mpaka kuwa chini ya $30000 na investors Dunia nzima wako katika panic kubwa na wanaonekana hawajui cha kufanya.

Kwa hali iliyopo sasa nadhani nchi nyingi kwa pamoja zinakwenda kudefault madeni yao tena kwa kufuatana hali ambayo itakwenda kuzalisha mamilion ya maskini Dunia nzima.

Kwa sasa tukae tayari mifumo iliyopo ya kifedha iliyojengwa kwa mtindo wa kumunipulate imefika mwisho tuweni tayari kwa mifumo mpya ambayo utakuja kwa masharti lukuki.
 
Hakuna haja ya kupaniki. Mitikisiko katika mifumo ya uchumi wa dunia siyo jambo geni. Wewe unapaniki lakini wenye mifumo yao na wanaojua kinachoedelea ndiyo wanapiga hela.

Lakini pia hali ya sasa kidogo inatia wasiwasi kwa sababu ya mambo yanayoendelea duniani. Uchumi wa dunia ndiyo huo ulikuwa umeanza kupumua baada ya mbanano wa Covid na sasa tena umeingia kwenye athari za vita vya Ukraine ambavyo vimeathiri sekta ya mafuta, nafaka pamoja na saikolojia ya masoko. Inflation imekuwa kubwa mno na matokeo yake ni kilio kila kona kila kitu kimepanda. Hata hiyo Marekani kupandisha interest kidogo ni katika juhudi za kujaribu kupambana na Inflation ambayo ni kubwa na haijawahi kutokea.

Ni vyema kujiandaa na mitikisiko hii japo kwa Mtanzania wa kawaida hata sijui anajiandaaje yaani.

Wewe unashauri tufanyeje katika hali hii?
 
Bubble inakaribia kulipuka na recession inakaribia kutokea. Serikali ya Biden inajaribu kuthibiti mfumuko wa bei niliona kuwa measure ya kuongeza interest ililenga kufanya hilo, lakini huenda ikawa tofauti.
 
Hakuna economic boom period inayodumu...lazima recession ziwepo ili regulation zakifedha and so on zifanyike in a sustainable manner. Ila kuna muda financial regulators wanashindwa kucontrol haya mambo kutokana na unforeseeable events. Ila ni vipindi vya mpito..cha muhimu vuta suruali yako juu jiandae kuchafuka na matope😄😄
 
"Welcome to 2030. You will own nothing and be happy" (Klaus Schwab, 2020) Welcome to the #Great Reset! Worldwide poverty!! World economic forum says, you will own nothing and be happy. They also want a reduction in world population by 2030. They are the enemy!!!

IMG_6886.jpg
 
Back
Top Bottom