Ni kipi ambacho alikuwa nacho Mkapa na Kikwete hana?

aise hawa ni watu wawili tofauti sn....huyu kwere hana lolote kichwani ambae hajui kwanini nchi yake ni maskini......
 
Mmoja anaita lebeshi -lebeshi; mwingine aniata lebeshi -kijiko!
Mmoja akipewa hela, mchanga, cement ya kujenga nyumba basi atajenga nyumba tena nzuri tu lakini atajikatia hapo 5% yako kama 'motivativation' - Huyo mwingine, yeye atachukuwa hela, mchanga na cement na kupeleka kusikojulikana huku mkibakia kusimulia 'bwana hapa ilikuwa ijengwe nyumba'!
 
mimi tofauti kubwa ninayo iona mmoja ni msanii na the former ni Serious na alikuwa anajua anachokifanya na alikuwa mzalendo tuache ubinadamu ambayo ni mapungufu ya kila anayeitwa binadamu, bado tunamkumbuka the real Presedent
 
kwa kuongezea:

1.Mkapa alifanya biashara akiwa pahala patakatifu yaani ikulu(kumbuka ANBEM)...Kikwete akawafanya wafanyabiashara kuwa maswahiba wake wakuu

2. Mkapa alitutukana tuliokuwa na fikra tofauti naye kwa kutuita wavivu wa kufikiri na spika wake Msekwa akawaita baadhi yetu wana wivu wa kike...Kikwete ametupuuza kwa kusema kelele za mbu hazimzuii mwenye nyumba kupata usingizi

3. Mkapa alimruhusu waziri wake kutufananisha na ng'ombe, punda nk kwamba tuko tayari kula majani ili Mkapa anunuliwe gulf stream (ndege ya rais)...Kikwete anafaidi kwa matanuzi ya safari za nje kwa ndege hiyo

4. Mkapa & Co waliruhusu mtandao uibe pesa BOT(EPA scandal) ili chama chao kishinde...ushindi wa kishindo huo ndiyo umetuletea Kikwete

ukisoma hizo points hapo juu..utaona mmoja alianzisha na mwingine ameendeleza na hapo ndiyo tunafikia hitimisho kuwa shida ni mfumo na siyo watu...watu ndiyo kwa kuwa ndiyo waanzilishi wa mfumo lakini kwa nini basi wasaidiane..lengo ni kulinda mfumo maana mwisho unawanufaisha wote.

Nawakilisha!

5.Mkapa alikuwa dikteta(kumbuka yaliyowakuta akina Ulimwengu, hakielimu, jaji Kisanga n.k) na Kikwete ni Laissez-faire
 
Mkapa alikuja kipindi kizuri akauza mashirika (kama NBC, n.k) ,akauza na nyumba za serikali kwa bei chee wakazinunua vigogo. Akaja kikwete masikini ya mungu hamna cha kuuza na mrahaba wa madini umekaa vibaya sasa , hapo ndio tofauti kubwa. Pamoja na pesa nyingi alitengeneza mheshimiwa Mkapa lakini hakuweza kufanya makubwa sana mimi haraka haraka nakumbuka uwanja mpya wa Taifa tu ambao wachina walisaidia.
 
Mkapa pamoja na madudu yake alikuwa na UDHUBUTU pia aliogopwa na baadhi ya watendaji.
JK gharasha tupu.
 
Akili, maarifa, busara, hekima?

1. Mkapa alikua ana uwezo wa kusimamia anachokiamini hata kama ni kibaya --- Kikwete uwezo huo hana.
2. Mkapa alikua na usawa katika dini zote --- Kiwete hana usawa katika dini.

Alicho nacho Jk Mkapa hana
1. Kwa kuongezea Mkapa alikua hana visasi wakati Jk ana visasi sana

Wanachofanania
1. Wote MAGAMBA tuu
 
zote ulizotaja hapo juu JK hana hata moja. Ila kuna ki2 mkapa alikuwa hana na JK anacho nayo ni UDINI

Kwakuwa shutuma ulizotoa ni nzito basi lete ushahidi japo mdogo tumpeleke mheshimiwa mahakamani akajibu tuhuma za ubaguzi.
 
Kwakuwa shutuma ulizotoa ni nzito basi lete ushahidi japo mdogo tumpeleke mheshimiwa mahakamani akajibu tuhuma za ubaguzi.
Kwa sheria ipi? Na wewe utoe kifungu cha sheria ambacho unafikiri kimevunjwa. Au mnaenda mahakamani kusalimia?
 
Upo utofauti mkubwa sana kati ya Mkapa na Kikwete. Mkapa alikuwa na maamuzi kama Rais, kwa mfano licha ya waTZ kupiga kelele wakisaidiwa na Tonny Blair kuhusu ununuzi wa rada, Mkapa aliweka msimamo hadi rada ikanunuliwa japo kwa ufisadi!

JK hana maamuzi kama Mkapa, kwa mfano: Alipoitisha Kamati Kuu ya CCM kuhusu malipo ya Dowans, yeye akiwa Mwenyekiti kikao kiliazimia kuwa Dowans walipwe yale mabilioni! Lakini siku ya sherehe ya CCM mwaka huu, JK aliutangazia umma kuwa, hata yeye hakubaliani kuwalipa Dowans!
Swali hapa ni kwamba, kwa nini Kamati kuu ya CCM ilipitisha azimio la kuwalipa Dowans?, alishindwa nini kuweka msimamo wa mkuu wa nchi katika kamati hiyo kwamba Dowans wasilipwe?
 
Back
Top Bottom