mwanasaikologia
Member
- May 23, 2013
- 76
- 17
Mwanasaikolo "GIA"
Mie hotuba za Sophia Simba napenda kumsikiliza huwa anaongea uhalisia wa mambo hivi ulishawahi kumsikiliza hotuba zake vzr?bila ushabiki?
Adolf Hitler was an emotional speaker who had a mesmerizing effect to those who listened....
Huyu jamaa alikuwa na uwezo wa kukushawishi ujitundike kwenye kitanzi mwenyewe kwa hotuba zake Tu..
Bongo bado Sana,wanaobalishwa Ni vilaza Tu wasiojitambua!!!
Kumbe hitra alikuwa bado anahutubia 2008-2010? Wonders never end!
Kati ya mwaka 2008 hadi 2010 niliwahi kumsikia Mh.Mbowe akihutubia Uwanja wa Mkendo Manispaa ya Musoma.
Alizungumzia mambo mengi ila alipoanza kulizungumzia suala Ufisadi wa EPA ndani ya BOT.
Nakumbuka siku ile watu walikuwa wengi sana walihudhuria wakiwemo wanachama na wapambe wa CHADEMA,CCM,CUF na wengi wasiokuwa wanachama wa chama chochote kile.
Kijana aliyeonekana kavalia Tisheti ya njano ikiwa inaashiria yeye ni mwana ccm aliyekunywa mpaka maji ya Bendera kama kiapo cha kutokukiuka masharti ya chama hicho.(kama wasemavyo watu)
Kijana huyo alionekana kumfuatilia Mbowe kwa makini wakati akiongea,Kijana aliyeaminiwa na ccm kuwa kamwe haitatokea akikane na kukiacha CHAMA CHA MAPINDUZI,ailiposikia fedha zile zikipangwa moja moja kutokea TZ zitafika Cairo Misri alipiga Yowe la nguvu UUWIIIII!!! HUKU AKICHANA ILE TISHITI ALIYOKUWA AMEIVAA MBELE YA HADHARA YOTE AKABAKIA KIFUA WAZI.
Kwa tukio hilo kutokea yamkini ilituthibitishia kwamba Hotuba ya Mbowe ilibeba ujumbe mzito mpaka kijana akaona haina maana ya kuendelea kuvaa Tisheti ya CCM huku akizidi kuwa masikini na Wakati huo huo Wengine wakiyala mema ya Nchi kwa kuifisidi Nchi kaa Mchwa anayatafuna Nyasi.
Wewe unaonaje? Mh. Mbowe aweza kuwa kiongozi wa Kisiasa mwenye Hotuba kali kiasi cha kuwabadili wengi na kuacha vyama vyao na kujiunga na CHADEMA?
Nawasilisha kwenu Wanajamii.
Khaa!! Style ya kuongelea kooni ambayo Lema, Mnyika na vijibwa vingine hutumia??Mbowe ana style yake ya kuvutia watu akiwa anahutubia, but Mwl Nyerere ni wisho wa reli ktk hotuba zake, huwa nasikiliza hotuba zake za miaka ya sitini, utadhani zimeandaliwa juzi, jamani ile ilikuwa mashine hakuna tena!
JK Nyerere ni Noma shida hakuna mrithi anayefanana naye iwe kwa Hotuba au Uadilifu.
Mbowe anatisha
Lipumba???
Miaka nenda rudi ni M/Kiti wa CUF na Amesimama kugombea Urais;Badala ya CUF kuongeza idadi ya wanachama ndio hao wanazidi kupungua.