Ni kiongozi gani wa kisiasa ana hotuba kali za kumbadilisha mtu?

Dr Slaa ninamkubali sana ni Kiongozi mzuri wa Kizazi hiki ila kwa mambo Hotuba sidhani kama anamfikia Chairman wake F.A.Mbowe.

mkuu, mbowe yuko fiti kwa hotuba anajua kuliteka jukwaa! Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
Mbowe kila mahali akisimama kuhutubia anatiririka vizuri sana,Nimemsikia kwenye Bunge la Katiba ameongea mambo ya muhimu sana.
 
Adolf Hitler was an emotional speaker who had a mesmerizing effect to those who listened....

Huyu jamaa alikuwa na uwezo wa kukushawishi ujitundike kwenye kitanzi mwenyewe kwa hotuba zake Tu..

Bongo bado Sana,wanaobalishwa Ni vilaza Tu wasiojitambua!!!
 
Kwangu Mimi wako wengi lakini hakuna hata mmoja wa kutoka CCM samahanini sana wanaCCM.. Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Zitto Kabwe (Nje ya Usaliti wake), JJ Mnyika, Halima Mdee, Pro. Lipumba, Field Marshal Godbless Lema, Kamanda alphonce Mawazo (Hapa ni kwa msisitizo)... Kwa Mbaali ndani ya CCM ni Harison Mwakyembe lakini sasa huwa anaongea mambo ya kiCCM hayana mvuto kwa watu.

kuna kijana mmoja nilimuona mnazi mmoja na kariakoo akihutubu mhadhara JOHN HECHE(BAVICHA )nae nilimkubali au wewe wamuonaje?
 
Kati ya mwaka 2008 hadi 2010 niliwahi kumsikia Mh.Mbowe akihutubia Uwanja wa Mkendo Manispaa ya Musoma.

Alizungumzia mambo mengi ila alipoanza kulizungumzia suala Ufisadi wa EPA ndani ya BOT.

Nakumbuka siku ile watu walikuwa wengi sana walihudhuria wakiwemo wanachama na wapambe wa CHADEMA,CCM,CUF na wengi wasiokuwa wanachama wa chama chochote kile.

Kijana aliyeonekana kavalia Tisheti ya njano ikiwa inaashiria yeye ni mwana ccm aliyekunywa mpaka maji ya Bendera kama kiapo cha kutokukiuka masharti ya chama hicho.(kama wasemavyo watu)


Kijana huyo alionekana kumfuatilia Mbowe kwa makini wakati akiongea,Kijana aliyeaminiwa na ccm kuwa kamwe haitatokea akikane na kukiacha CHAMA CHA MAPINDUZI,ailiposikia fedha zile zikipangwa moja moja kutokea TZ zitafika Cairo Misri alipiga Yowe la nguvu UUWIIIII!!! HUKU AKICHANA ILE TISHITI ALIYOKUWA AMEIVAA MBELE YA HADHARA YOTE AKABAKIA KIFUA WAZI.

Kwa tukio hilo kutokea yamkini ilituthibitishia kwamba Hotuba ya Mbowe ilibeba ujumbe mzito mpaka kijana akaona haina maana ya kuendelea kuvaa Tisheti ya CCM huku akizidi kuwa masikini na Wakati huo huo Wengine wakiyala mema ya Nchi kwa kuifisidi Nchi kaa Mchwa anayatafuna Nyasi.

Wewe unaonaje? Mh. Mbowe aweza kuwa kiongozi wa Kisiasa mwenye Hotuba kali kiasi cha kuwabadili wengi na kuacha vyama vyao na kujiunga na CHADEMA?

Nawasilisha kwenu Wanajamii.

kaka dr slaa anaushawishi mkubwa sana na tungepata watu angalu 10 tu kama yeye Tanzania isingefikia hapa leo , including our late prez. Nyerere
 
kwa kujenga Hoja slaa,zito na mnyika wanatisha ila kwa hotuba za hatari Mbowe,lema,msigwa na mawazo ni balaa
 
Mheshimiwa Getrude Lwakatare ni nomaaaa, kuanzia sauti mpaka mpangilio wa mada
 
Mchungaji Mtikila, ndiye gwiji pekee wa hotuba. Kila neno analotamka limepimwa, natamani angekuwa rais 2015.
 
Mie na utaalamu wangu wa kiingereza sijakupata kabisa mkuu. Hebu andika kwa lugha nyingine huenda ukaeleweka.
 
Back
Top Bottom