Ni kazi gani uliyowahi kufanya ambayo unafikiri hautoweza kuisahau kamwe?

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,941
24,816
Taja hapa kazi uliyofanya ambayo unafikiri hautoweza kuisahau kamwe?
Ama kwa ugumu wa kazi yenyewe au hadhi yako katika jamii.

Mimi binafsi kazi ambayo nimefanya na sitokaa niisahau ni kazi ya ukonda wa daladala niliifanya kipindi nimemaliza kidato cha nne kama gape la kusubiri matokeo ya mwisho
Asikwambie mtu hii kazi ni ngumu sana hasa ukikutana na abiria wenye vichwa vigumu.
Yaani wao wanaona ugomvi ni kama suluhisho lao.

Hakika sitokaa niisahau hiyo kazi .
Na wewe je mwanaJF mwenzangu taja kazi yako.

87670d8c4efec3ff0b9574b80faca40e.jpg

ZERO IQ.!
 
Hiyo ya kujenga tiles ndiyo ilikua ishu, nilikutana na wadada wawili huku nimebeba mashine ya kukatia tiles, wale wadada tulikua darasa moja. Ngoma imenikuta Magomeni hospitali hakuna pa kuingia pale.
Hiyo ilikuwa noma kweli
 
Nikiwa kidato cha sita Mimi na jamaa yangu mmoja mzee wa kuhangaika tulipata dili la kuchapia choo cha shule ya serikali.Tena kilikuwa cha shimo...tulizoea kusema cha kulenga...sio hivi vya kisasa vya ku flash. Bwana wee harufu ya mavi ilikuwa mbaya(utadhani kuna wakati mavi hutoa harufu nzuri)!.Tulikomaa siku nzima,huku tukiipuuzia harufu ya mavi na baadaye kuizoea.Tukajiambia kumbe si mbaya,ni nzuri tu...na hasa jua lilivopiga kwenye bati...mavi yakatokota shimoni mvuke mzuri ajabu ukamea taratibu na kutoa mlio wa pyuu...harufu nzuri ajabu.Masela wakatuletea nguna,tukaisokomeza vinywani mwetu huku macho tumeyafumba kwa utamu wa haja.Harufu nzuri ya mavi yatokotayo iliusindikiza vema mlo wa ugalu kwa maharagwe.Sh.Elufu(elfu) nne nilizozipata kama malipo zioitumika mwezi mzima!
 
Gepu la kusubiri kujiunga UDSM baada ya kumaliza FTC Mbeya Tech enzi izo... nilikuwa nabeba samaki toka ziwa nyasa na kuwauza Songea mjini pale soko la Lizaboni na jeshini chabruma. zile safari kwenye TOYOTA STOUT ya Konda Madebe siwezi sahau na kukamatwa na wanajeshi nikatetewa na wamama...
 
Gepu la kusubiri kujiunga UDSM baada ya kumaliza FTC Mbeya Tech enzi izo... nilikuwa nabeba samaki toka ziwa nyasa na kuwauza Songea mjini pale soko la Lizaboni na jeshini chabruma. zile safari kwenye TOYOTA STOUT ya Konda Madebe siwezi sahau na kukamatwa na wanajeshi nikatetewa na wamama...
Mkuu samahani, hua naangalia username yako na kuhisi kama vile haujui maana yake. Lakini leo umetaja una background ya Mbeya nadhani utakua unajua kua username yako pia maana yake nyingine ni "bado/ mbona kasichana".
 
Mimi baada ya kumaliza form four nilikua nikimsaidia mama kwenda kuuza vitumbua gengeni asubuhi na jioni kwa wasio elewa maisha walikua wakiona kitu cha ajabu sana lakini kidume nilikomaa kwan ndivyo vilivyo tuweka mjini
umenikumbusha mimi nilikua nauza Ice cream kwenye shule fulani Dah.. Boyfriend wangu wa kipindi hiko aliwahi kuniambia one of the thing kilimvutia kwake ni hiko aliniona fighter maana nilikua nasimamia shoo mwanzo mwisho...
 
umenikumbusha mimi nilikua nauza Ice cream kwenye shule fulani Dah.. Boyfriend wangu wa kipindi hiko aliwahi kuniambia one of the thing kilimvutia kwake ni hiko aliniona fighter maana nilikua nasimamia shoo mwanzo mwisho...

Ebwanaee...mimwenyewe vitumbua vilinifanya nitokekimaisha kwani kunakibosile mmoja alinikuta nikiwa gengeni nauza vitumbua akiwa hanijui namimi simjui akavutiwa nanilichokua nikikifanya akaamua kunisaidia mpaka leo nimekua mtu ktk watu nakubakiza story na mfano wakuigwa mtaani
 
Back
Top Bottom