Ni kawaida binti wa miaka 13 kuvunja ungo?

89357763_3461700717178651_8616117253802295296_n.jpg
 
Ni kawaida kabisa hasa kwa mabinti wenye miili mikubwa, binti yangu alivunja ungo akiwa na miaka 11 darasa la tano. Huu ndo muda wa kuongea nae kweli kweli tena kwa kutumia mafundisho ya dini. Kama ni mkristo mwambie mwili wake ni hekaalu la Roho Mtakatifu. Pia tumia maandiko kutoka 1Wakorinto 6: 18-20.
Hakikisha anamuogopa Mungu kuliko anavyowaogopa nyie wazazi
Nakutakia kila la heri mkuu
'Mbwa mwitu' watakula nae sahani moja tu no matter what!
 
Mzigo ushaiva huo. Hongera kwa kutuzalia demu wetu mkuu.
Au sio baba mkwe😂😂😂😂😂
 
Hivyohivyo na wa kiume ukiona sauti inaanza kukwaruza inahama kutoka sauti ya kwanza inaelekea kuwa ya tatu na nusu jua tayari anaweza kusababisha maafa kwa majirani. Kwa nini wa kiume huwa hatuwakalishi chini kuwaeleza kwamba wamekua?
 
Nijuavyo ni kuwa kuvunja ungo (Menarche) ni miaka miwili baada ya kuanza balehe (Puberty), hivyo tukio la kuvunja ungo huwa halitokei pasi na dalili za utangulizi ambazo ni balehe

Bila shaka mtoa mada umekwishaona mabadiliko ya upili ya ukuaji wa mwili wa binti yako kama vile ngozi kunawiri, sauti kuwa nyororo, kutanuka nyonga, kuota vinyweleo, matiti kukua n.k....

Kama umeyashuhudia yote hayo basi hili la kuvunja ungo si la kushangaza. Zamani balehe ilikuwa inaanza na miaka 13 hadi 15 kwa watoto wa kike ila zama hizi ni kuanzia miaka 9 aisee...

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
shukrani kwa somo. ulichoongea nimekishuhudia!
 
Hivyohivyo na wa kiume ukiona sauti inaanza kukwaruza inahama kutoka sauti ya kwanza inaelekea kuwa ya tatu na nusu jua tayari anaweza kusababisha maafa kwa majirani. Kwa nini wa kiume huwa hatuwakalishi chini kuwaeleza kwamba wamekua?
mkuu kuharibiwa mtoto wa kike inakera zaidi. katika jamii zetu hizi za mfumo dume mtoto wa kiume akiharibu kwa jirani huko hata huumii sana (zaidi utakuwa na hisia za kufurahisha za 'udume' tu wa mtoto wako akilini)
 
Anza kuweka ulinzi mzee kuanzia wa kijinsia kwake, aijue dunia na ubaya wake mkalishe chini kupitia mkeo mapema laa sivyo wahuni watampitia kimasihara. Vzr umetambua naamini utamudu kumjenga na kumuepusha mambo mabaya kwa sasa
nitajitahidi mkuu
 
Back
Top Bottom