Ni kama nyuso za Watanzania zimefunguka!

Ni kama nyuso za Watanzania zimefunguka!

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,509
Reaction score
45,126
Nimefanya uchunguzi wangu binafsi nimeona na kujiridhisha pasi na shaka kwamba nyuso za watanzania zimefunguka!! Kuna ki faraja fulani ndani yao. Vijiwe vingi sasa vinaanza kuongea mambo ya matumaini.

Ni kama nchi imepata uhuru vile! Kuna kitu kwa kweli kimo ndani ya hawa watanzania.

Nafikiri hata na nyie wenzangu mmeona wenyewe hali ya nchi ilivyo kwa hizi siku tatu nne.

Watalaam wa saikologia ya binadamu pia wataniunga mkono.
 
Kama Mungu yupo kweli basi anaipenda sana Tanzania kuliko watu wanavyofikiri!! Na Watanzania kama hatutajifunza kwenye hili hata Malaika watakasirika na ghadhabu tutaiona
Ni kitu cha ajabu sana hiki...watanzania kuanza kuwa na nyuso hizi za matumaini wakati mifukoni mwao bado hawana kitu ni jambo la ajabu saana!!
 
Mi kitu nilichojifunza ni "heri kumfadhili mbuzi,utakunywa hata mchuzi..lakini si kumfadhili binadamu,binadamu si mtu mzuri" hili nimejifunza,na nitaitumia ktk maisha yangu kama kanuni,kuanzia juzi simuamini binadamu yoyote aisee
 
Kwa kweli tumepata uhuru. Hata kwenye makundi ya WhatsApp unaona waliokuwa wanaogopa kabisa kuchangia chochote kwenye mijadala, sasa wanafunguka.

Mpaka wabunge pale mjengoni nao wamepata uhuru.....tukianza na Mh 'Supika'.

JPM alituweza kweli!
 
Una maana ipi kaka? Wewe si mmoja wa watanzania ambao wanaoangalia mwangaza kwa mbaali? Unaona namna akina Sabaya walivyojigeuza wao kuwa mapolice, wao mahakama na wao hao hao kutoa hukumu?

Huwezi kujua watanzania hawa kwa nini sasa nyuso zao sasa zina furaha.
 
Mi kitu nilichojifunza ni "heri kumfadhili mbuzi,utakunywa hata mchuzi..lakini si kumfadhili binadamu,binadamu si mtu mzuri" hili nimejifunza,na nitaitumia ktk maisha yangu kama kanuni,kuanzia juzi simuamini binadamu yoyote aisee
Pia jifunze kusema ukweli muda wote katika maisha yako!
Maama unaweza danganya watu kwa miaka sita ila nusu mwezi tu wakigundua
Ulikuwa muongo na mwizi watakuona mtu mbaya sana kuliko chatu mla watu!
 
Kwa kweli tumepata uhuru. Hata kwenye makundi ya WhatsApp unaona waliokuwa wanaogopa kabisa kuchangia chochote kwenye mijadala, sasa wanafunguka.

Mpaka wabunge pale mjengoni nao wamepata uhuru.....tukianza na Mh 'Supika'.

JPM alituweza kweli!
Wanaogopa tu kuandamana ila wana furaha ya ajabu.....ni kweli kabisa!!

Taifa ni kama limekombolewa!!
 
Kwa kweli tumepata uhuru. Hata kwenye makundi ya WhatsApp unaona waliokuwa wanaogopa kabisa kuchangia chochote kwenye mijadala, sasa wanafunguka.

Mpaka wabunge pale mjengoni nao wamepata uhuru.....tukianza na Mh 'Supika'.

JPM alituweza kweli!
Adi spika kasema jamani semeni ukweli ili msaidie serikali kufanya mipango yake kwa ufanisi Msiogope msiogope!!
Nikagundua kumbe mwazo walikuwa wana ogopa!
 
Walioko huku kwetu wamepoteza matumaini. Yaani wanahisi wametelekezwa baharini katika boat isiyo na injini
 
Anayebisha basi hayuko sawa..jamani tulitishwa mnooo khaaa
Kaka hata kuongea kuhusu mwenendo wa nchi yako ilikuwa shidah, huyu mjinga mjinga Msiba ni wa kuwatukana kina Kikwete na kinana kweli? Hapo ndipo mwendazake alipokuwa katufikisha.
Kweli nchi ni kama imepata uhuru!!

Mi pia nakubaliana na wengine kwamba tusimwage sifa kwa Samia - hatujamwaga bado ila tuwaache watanzania washangilie Uhuru wao!! Freedom is back!!
 
Nimefanya uchunguzi wangu binafsi nimeona na kujiridhisha pasi na shaka kwamba nyuso za watanzania zimefunguka!! Kuna ki faraja fulani ndani yao. Vijiwe vingi sasa vinaanza kuongea mambo ya matumaini...

Ni kama nchi imepata uhuru vile !! Kuna kitu kwa kweli kimo ndani ya hawa watanzania.

Nafikiri hata na nyie wenzangu mmeona wenyewe hali ya nchi ilivyo kwa hizi siku tatu nne....

Watalaam wa saikologia ya binadamu pia wataniunga mkono....

Bar nyingi zilizokuwa hazina watu kwasasa naona watu/wanywaji wanaongezeka.

Ila kiukweli JIWE alikuwa muoga sana ,sector zote za uchumi alikuwa anazilimit sana kufanya mambo yao kwa uhuru hivyo kupelekea baadhi ya wawekezaji kurudi nyuma na kutilia shaka ku_invest mzigo....JIWE alikuwa anaona kama atapinduliwa.
 
Back
Top Bottom