Ni kama nchi imesimama, hakuna kinachoendelea

Major

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2007
Posts
1,865
Reaction score
2,453
Binafsi nahisi ni kama Tanzania kwa sasa hivi tuna wakati mgumu kuliko kipindi chochote cha uhai wa nchi hii kilichopita.

Sasa hivi wataalamu wote wa nchi hii wanakwazwa na wanasiasa ambao 100% hawana utaalam wowote. Doctor msomi na mzoefu kazini anaweza kufukuzwa kazi na mkuu wa wilaya! Ambaye hata kusoma na kuandika hajui vizuri. Ni hatari sana.

Hatari kubwa zaidi ni viongozi kujaribu kuyatumia majeshi yetu kisiasa. Hii ni hatari kubwa kuliko wao wanavyofikiri. Kama hali itaendelea hivi, basi kuna Siku haya haya majeshi yetu na yenyewe yatatamani kutawala. Hakuna atakayeweza kuyazuia.

Nchi imekosa dira kabisa. Wananchi hawajui wafanye nini! Kwa mfano. Mwaka huu wakulima wamelima nyanya na mazao ya mboga mboga kwa wingi sana. Wengi walihamasika baada ya kiongozi wetu kuwaahidi kuwa ni Tanzania ya viwanda. Matokeo yake kila mkulima analia. Nyanya hazina bei na hakuna hata kiwanda kimoja cha kusindika nyanya. Zinaozea mashambani.

Wakulima wa nyanya ni kilio kila kona ya nchi hii. Sasa hivi tenga moja la nyanya ambalo lina wastani wa kilo 30 bei yake ni Tsh elfu tatu (3000) hakuna juhudi zozote za kuwaokoa hawa wakulima. Waziri anayehusika na viwanda hawezi kufanya lolote la dharura ili kuwaokoa hawa wakulima kwa sababu anaogopa bila sababu. Sasa kama hatuwezi kuhifadhi hata mazao yetu tunayolima, je ni viwanda gani tunafikiri tunaweza kumiliki?

Kila kiongozi mwenye taaluma anaogopa kufanya maamuzi kwasababu nyuma yake kuna anayemsimamia ambaye ni mwanasiasa asiye na taaluma yoyote. Yeye taaluma yake ni kutafuta sifa tu, madhara yake ni makubwa kuliko tunavyofikiri. Tusipobadilika mapema, tutakwama sana na tunastahili kukwama.
 
Bora wewe umeliona hilooo....wengine wako bize na tar 1 Sept....utasikia
1-ukuta
2-ukum
3-siku ya usafi kwa majeshi
4- siku ya kupatwa jua
5-.........
6-.......
Natamani nirudi shule nikuchukuwe masters na PhD n dani ya miaka mitano inji ukiwa imesimama mie niwe nimegain education.
Sitaki kusimama na nchi iliyoamua yenyewe kuisimamisha.
 
Mkuu ni hatari sana. Tena bora mara Mia uende shule kuliko kupoteza Muda. Other ways unaweza ukasimama na nchi
 
Wakuu wa Wilaya na mikoa, wakuu wa Polisi, wote wanahisi kuwa jukumu lao kubwa la kikazi ni kuhangaika na wapinzani. Kwa bahati mbaya hakuna hata tofali moja la kiwanda linalotengenezeka kwa kudhibiti upinzani.

Tunatumia gharama kubwa ikiwa ni pamoja na muda mwingi kuhangaika na vitu vya kijinga, vitu ambavyo haviwezi kulisogeza Taifa hili hata hatua moja mbele, huku kuna mambo mengi ambayo tungehangaika nayo, wote kwa pamoja kama Taifa, yangeweza kusogeza mbele Taifa letu.

Watawala ni muhimu wakatambua kuwa hakuna hata siku moja ambapo watu wote watakuwa na fikra za aina moja, yaani wote wakakuunga mkono kwa kila jambo na kwa wakati wote, ukilazimisha utawapoteza hata wale ambao walikuwa wakikuunga mkono.
 
Hongera kwa kutambua mkuu. Ila Mimi sasa hivi najipanga ili nihamie Kenya, baada ya miaka 5 nitarudi. Siwezi kukubali kupoteza muda wangu hapa wakati kila dalili za hali ngumu ya maisha zinaonekana. Na watawala wetu wametia pamba masikioni.
 
Wengine tunawaona siku ya usafi tu,pamoja na hilo hakuna changamoto wanazojiongeza kwenye usafi huo kama kupata hata hela za kununua skips za kuwekea taka.
 
Na pia ukichukulia tishio la watoa maoni kwenye mitandao basi hata yale mawazo ambayo outwardly hudahiwa ni ya kijinga lakini ndio yanawasaidia wenye PhD zao kufikiri kwa usahihi yamesimama!
 
Mkuu nchi haijasimama. Watu wanachapa kazi na maisha yanasonga. Maisha hayajawahi kuwa rahisi. Ni kweli changamoto ni nyingi lakini Kikubwa...wewe pambana kwenye nafasi yako uliyonayo. Usaidie familia yako na wategemezi wako (ikiwa ni pamoja na kulipa kodi stahiki za jamhuri). Hayo mengine waachie wenyewe.

Tanzania ya viwanda haitaletwa na serikali. Ukiona nyanya zinaozea shambani..hebu fikiria ni namna gani unaweza kutumia fursa ya kuzisindika. ni wewe na mimi kuona fursa zilizopo na kuzitumia. Ukisubiri kwamba serikali ifanye hili au lile..utasubiri bila majibu.

Mimi nadhani wananchi wengi hatujui wajibu wa serikali. We expect too much from it. Yet the truth is our expectations are in most cases misplaced!

Lets stop complaining! Do something. Hata akitoka Magufuli atakuja mwingine na yeye atakuja na wimbo wake. Mwisho wa siku ni wewe unayeumia na kukosa ufumbuzi wa matatizo yako na jamii inayokuzunguka.
 
Nchi haiko katika wakati mgumu sema ww ndo uko katika wakati mgumu.Tatizo lenu mlizoea vya kunyongwa vya kuchinjwa hamviwezi.Hakuna wakati nchi imetulia kama sahizi asikudanganye mtu mapato ya serikali sahizi yanatumika ipasavyo na kwa taarifa yako pesa iko yakutosha hakuna matumizi ya ovyo sahizi.
Kwani nyanya kuwa elf3 ni mwaka huu tu? au unaleta umbeya? Tatizo unaunganisha matatizo yako kufanya serikali ichukiwe hayo maswala ya bei ya mazao ni historia sio nyanya tu toka enzi matatizo ya hivyo yapo ww unataka kuaminisha watu kisa awamu ya tano ndo hali iko hivo.

Pia kiwanda mjomba hakijengwi siku 1 subira yavuta Kheri hiyo ni mikakati sio ya mwaka mmoja au miwili. Mtaweweseka sana mwaka huu shughuli ndo kwanza inaanza mjomba.
 
Maendeleo hakuna, misuguano inazidi mpaka watu wanashangilia vivo vya walinzi wa Amani yao. Na kuonyesha kuwa hawa wanasiasa wa Leo hawatumii hekima badala ya hali hiyo kuiondoa kwa kurejesha upendo wanamwagia tena petrol kwa kusema tutawasaka ndani na nje. Hivi ukiwakamata ndio utakuwa umeondoa chuki kati ya polisi na raia? Badala ya kujenga daraja wao wanajenga ngome ya kuwatenganisha zaidi
 
Binafsi nahisi ni kama Tanzania kwa sasa hivi tuna wakati mgumu kuliko kipindi chochote cha uhai wa nchi hii kilichopita.

Sasa hivi wataalamu wote wa nchi hii wanakwazwa na wanasiasa ambao 100% hawana utaalam wowote. Doctor msomi na mzoefu kazini anaweza kufukuzwa kazi na mkuu wa wilaya! Ambaye hata kusoma na kuandika hajui vizuri. Ni hatari sana.

Hatari kubwa zaidi ni viongozi kujaribu kuyatumia majeshi yetu kisiasa. Hii ni hatari kubwa kuliko wao wanavyofikiri. Kama hali itaendelea hivi, basi kuna Siku haya haya majeshi yetu na yenyewe yatatamani kutawala. Hakuna atakayeweza kuyazuia.

Nchi imekosa dira kabisa. Wananchi hawajui wafanye nini! Kwa mfano. Mwaka huu wakulima wamelima nyanya na mazao ya mboga mboga kwa wingi sana. Wengi walihamasika baada ya kiongozi wetu kuwaahidi kuwa ni Tanzania ya viwanda. Matokeo yake kila mkulima analia. Nyanya hazina bei na hakuna hata kiwanda kimoja cha kusindika nyanya. Zinaozea mashambani.

Wakulima wa nyanya ni kilio kila kona ya nchi hii. Sasa hivi tenga moja la nyanya ambalo lina wastani wa kilo 30 bei yake ni Tsh elfu tatu (3000) hakuna juhudi zozote za kuwaokoa hawa wakulima. Waziri anayehusika na viwanda hawezi kufanya lolote la dharura ili kuwaokoa hawa wakulima kwa sababu anaogopa bila sababu. Sasa kama hatuwezi kuhifadhi hata mazao yetu tunayolima, je ni viwanda gani tunafikiri tunaweza kumiliki?

Kila kiongozi mwenye taaluma anaogopa kufanya maamuzi kwasababu nyuma yake kuna anayemsimamia ambaye ni mwanasiasa asiye na taaluma yoyote. Yeye taaluma yake ni kutafuta sifa tu, madhara yake ni makubwa kuliko tunavyofikiri. Tusipobadilika mapema, tutakwama sana na tunastahili kukwama.
Hali ngumu ikiwa kwako usifikiri na kwa wengine ni hivyo hivyo. Binafsi naona mambo murua kuliko kipindi kingine chochote.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Inauma sana, tena inakera sana. Juzi nimeona mkuu wa wilaya flani anamfukuza Afisa mifugo uku anafoka na kutajataja huu ni awamu ya tano siyo ya nne. Niliumia sana, sijui ndo njia ya kufanyia kazi matatizo ya wakulima na wafugaji?
 
Na pia ukichukulia tishio la watoa maoni kwenye mitandao basi hata yale mawazo ambayo outwardly hudahiwa ni ya kijinga lakini ndio yanawasaidia wenye PhD zao kufikiri kwa usahihi yamesimama!
Viongozi wetu ni Kama wamechomwa sindano waka paralaizi. Hakuna wa kumstua mwingine. Wao bado wanafikiri wako kwenye kampeni wakati tayari tulishawachagua. Nasikitika sana.
 
Hali ngumu ikiwa kwako usifikiri na kwa wengine ni hivyo hivyo. Binafsi naona mambo murua kuliko kipindi kingine chochote.

Hongera ndugu yangu, mimi nilikua na kibanda nilikua nauza 80,000/ kwa siku ila juzijuzi nimefunga kibanda kwani nilianza kuuza 3,000/ kwa siku.
 
Jiongeze, Ongeza ubunifu, challenge ni kawaida pambana nazo.
 
Back
Top Bottom