Mkuu nchi haijasimama. Watu wanachapa kazi na maisha yanasonga. Maisha hayajawahi kuwa rahisi. Ni kweli changamoto ni nyingi lakini Kikubwa...wewe pambana kwenye nafasi yako uliyonayo. Usaidie familia yako na wategemezi wako (ikiwa ni pamoja na kulipa kodi stahiki za jamhuri). Hayo mengine waachie wenyewe.
Tanzania ya viwanda haitaletwa na serikali. Ukiona nyanya zinaozea shambani..hebu fikiria ni namna gani unaweza kutumia fursa ya kuzisindika. ni wewe na mimi kuona fursa zilizopo na kuzitumia. Ukisubiri kwamba serikali ifanye hili au lile..utasubiri bila majibu.
Mimi nadhani wananchi wengi hatujui wajibu wa serikali. We expect too much from it. Yet the truth is our expectations are in most cases misplaced!
Lets stop complaining! Do something. Hata akitoka Magufuli atakuja mwingine na yeye atakuja na wimbo wake. Mwisho wa siku ni wewe unayeumia na kukosa ufumbuzi wa matatizo yako na jamii inayokuzunguka.