Ni kama muujiza, kwa vituko vya CCM sikutegemea ishinde.

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,344
Uchaguzi umekwisha, walioshinda wameshinda na walioshindwa wameshindwa, ninachojaribu kufanya sasa ni kuonyesha uwiano wa kile kilichotarajiwa na wengi kabla ya uchaguzi na matokeo ya matarajio hayo baada ya uchaguzi.

Kusema kweli, nikiwa mwanachama wa CCM tangu enzi za TANU, ni katika uchaguzi wa mwaka huu pekee kati ya chaguzi zote zilizowahi kufanywa nilikuwa na wasi wasi wa CCM kushindwa ama kutoa matokeo ambayo yangekaribiana sana na vyama vya upinzani.

Mtazamo wangu huu ulitokana na udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na serikali ya Rais Kikwete katika vipindi vyote viwili vya utawala wake alivyokaa madarakani.

Watanzania wamenishangaza sana kiasi ninashindwa kuelewa ni vigezo gani hasa tunavyotumia kukipa kura chama cha siasa wakati wa uchaguzi.

Sikutegemea, kwa madudu yaliyokuwa yamefanywa na serikali ya Kikwete kama CCM ingeweza kupata ushindi huu wa 58% dhidi ya 40%.

Ebu jaribu kurejea kashfa kama za EPA, Richmond, Escrow, Kuzuia Katiba mpya, utoroshaji wanyama wetu kwenda nje, mateso, unyanyasaji na mauaji ya kinyama ya raia kutoka vyombo vya dola (Ulimboka, Mwangosi n.k), dhuruma na utesaji wa raia wakati wa oparesheni Tokomeza na mengine mengi lakini eti tayari watanzania wameishayasahau yote hayo wakaamua kuirundikia CCM kura.

Safari hii wapinzani walikuwa na turufu nzuri sana ya kuitumia dhidi ya CCM lakini kwa tamaa za kipumbavu za viongozi wao hawakukumbuka hayo, wote wakageuzia fahamu, macho na akili zao kwa akina Lowassa, Sumaye na Kingunge ambao hawakuwa na mamlaka yoyote ndani ya Ukawa, wakaachiwa majukwaa ya kampeni, matokeo yake CCM ikajikuta imeachiwa mwanya wa kupenya hadi kwenye mstari wa ushindi bila kikwazo.

Nina imani Magufuli akiutumia vizuri mwanya huu uliopatikana, ambao sasa wapinzani hawana agenda madhubuti watakayoisimamia mbele ya wananchi, akafanya vizuri ktk miaka hii mitano ya kwanza ana uwezo wa kuisambaratisha kabisa Ukawa.
 
UKAWA imeshakufa. Tangu walipowabeza na kuwadhalilisha mashujaa waliounda UKAWA kisha kuwaacha wende zao, wakakaribisha makapi yaliyowafanya wao UKAWA wakubalike kwa kuyasema maovu yao. Magufuri anajua walipokosea UKAWA na ndio maana ktk kampeni neno MABADILIKO na MAFISADI hakuliacha
 
kiujumla mtaji mkubwa wa ccm ni ujinga na umasikini. hivo hivo vimetamalaki sana kwa mikoa ya pembezoni na katikati ya taifa letu. hivo huo ndo ulikuwa mtaji mkuu wa ccm kushinda uchaguzi...
 
maramia,

..mimi sikutegemea kama Lowassa will be that weak on the campaign trail.

..tukubali kwamba Lowassa tuliyemtegemea, siye yule tuliyempata ktk kampeni hizi.

..ukawa bado wana nafasi ya kuibua upya kashfa zilizotokea ktk awamu ya JK.

..sasa watakuwa wanam-challenge Magufuli kuzishughulikia manaake aliahidi mahakama maalum ya mafisadi.

..suala lingine litakalowapa uhai ukawa ni KATIBA MPYA, MUUNGANO, na TUME HURU YA UCHAGUZI.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom