Ni Kama ilipangwa na Mungu uchaguzi huu Bunge liwe la CCM tu

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Tunafahamu kwa kiasi kikubwa sarakasi zilivyotumika katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Kura ziliibwa, wasimamizi walipiga kura nyingi hadi zikapitiliza idadi ya wapiga kura waliojiandikisha

Mabegi yalijazwa kura zilizopigwa saa 12 asubuhi.

Yote hii ilifanyika kuhakikisha CCM inabaki madarakani na Rais afurahi kwa kupita kwa asilimia kubwa

Viongozi wa dini wanatufundisha kuwa Mungu huruhusu jambo litokee ili makusudi fulani itimie

Intelijensia ya CHADEMA isingeshindwa kujua kwamba walimu na wasimamizi wengine walipangwa mapema kabisa kupiga kura nyingi kadili wawezavyo maana Kuna baadhi ya Walimu walikuwa wafuasi wa CHADEMA.... Lakini waliliacha likapita

Hayo yote yaliwezekana ili Mungu ajidhihirishe.

Kwanza waelewe Mungu hapangiwi na hata uwe mwamba vipi akikuhitaji lazima utaondoka tu . Ukifanya ukatili sio kwamba utaishi milele

Pili alitaka kuwaumbua wabunge wa CCM ili wale pumba tuwajue na wale mchele tuwajue

Tangu bunge la bajeti linaanza imekuwa ni vituko vituka kila siku

Kama Wapinzani wangekuwepo Bungeni, wangezodolewa kwamba wanamsema marehemu na usingesikia mbunge wa CCM anamsema vibaya hayati.

Lakini hali ni tofauti. Wale waliokuwa wanawasemea ajenda nzito nzito huku wao wakijificha nyuma yao hawapo kwasababu waliwaibia uchaguzi wakidhani ni ujanja.

Nina hakika Kuna baadhi ya wabunge wanatamani kambi rasmi ya upinzani ingekuwepo bungeni! Kuna wanaoogopa kuonekana wasaliti lakini mioyoni mwao wana fundo zito wanashindwa kulitoa

Ni lazima wagawane, either kambi Magufuri au Kambi Samia

Awamu hii wameumbuka na wataendelea kuumbuka
 
Back
Top Bottom