Ni John Okelo au Amri Abeid: mapinduzi

Ni John Okelo au Amri Abeid: mapinduzi

hasason

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
1,648
Reaction score
1,542
Kama nilivyojifunza kwa makini History of Colonialism and Nationalism Zanzibar aliemobilize na kukamilisha mapinduzi kamili ya Zanzibar ni mganda John Okelo na sio Amri Abeid sasa inakuwaje hata kumtambua hatajwi wala kuthaminiwa kama Icon ya Nationalism kwa Zanzibar.
 
Joni ukelu si mganda ni Mkenya kama sikosei ,na hakuwa kitu chochote isipokuwa alivishwa kilemba cha ukoka na kutomezwa hayo mapinduzi hata baadhi ya vijana wa kiarabu walishiriki kivyao ,kilichopinduliwa si muarabu bali ni serikali huru iliyopokea uhuru ,japo Zanzibar haikuwahi kuwa koloni la Nchi yeyote ile,kwa ufupi pia napenda ufahamu ZANZIBAR haikuwahi kutawaliwa au kuwa koloni ,la muingereza,mreno mjerumani au mualabu ni tofauti na huo upande wa pili !
 
Heko FM J.G.Okello kwa kuwa mwanamapinduzi uliyefanikisha mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Nimesikitishwa na Rais wa Zanzibar kumtaja Amri Abeid Karume kama muasisi wa mapinduzi hayo wakati alikuwa Tanganyika pindi mapinduzi hayo yanafanyika!

Kwa kweli nimesikitishwa sana na upotoshaji huu wa hali ya juu!
 
Haujui historia, najua hukuwepo ila unapaswa usome historia

Zanzibar ilipewa Muingereza katika mkutano wa Berlin mwaka 1884 - 1885
 
Mkuu JOASH MUSSA yaelekea wewe ndiye hujui chochote,ni J.Okelo ndiye aliyefanya mapinduzi haya,na wakati mapinduzi yanafanyika Mzee Karume alikua ndani ya maji akikimbilia Dar kuyanusuru maisha yake punde akapigiwa simu/radio call kwamba arudi znz maana kazi imekwisha,na wakati huo mwalimu nyerere alikua Nairobi katika kupigania uanzishwaji wa jumuia ya A.mashariki.Na kenya na uganda ziliitambua serikali mpya ndani ya masaa 24 tuu,wakati mwalimu nyerere ilimlazimu kusubili mpaka siku3-5kuyakubali mapinduzi hayo lakini kwa masharti.Na moja ya masharti ni kumtimua John Okelo kule zenji ili arudi kwao Uganda.
Na jee unafahamu kilichomkuta J.OKELO baada ya kutimliwa Zenji weye?
 
Last edited by a moderator:
Haujui historia, najua hukuwepo ila unapaswa usome historia

Zanzibar ilipewa Muingereza katika mkutano wa Berlin mwaka 1884 - 1885

J.Okello alikuwa anapiigania nini?
 
Joni ukelu si mganda ni Mkenya kama sikosei ,na hakuwa kitu chochote isipokuwa alivishwa kilemba cha ukoka na kutomezwa hayo mapinduzi hata baadhi ya vijana wa kiarabu walishiriki kivyao ,kilichopinduliwa si muarabu bali ni serikali huru iliyopokea uhuru ,japo Zanzibar haikuwahi kuwa koloni la Nchi yeyote ile,kwa ufupi pia napenda ufahamu ZANZIBAR haikuwahi kutawaliwa au kuwa koloni ,la muingereza,mreno mjerumani au mualabu ni tofauti na huo upande wa pili !

Ukiacha kufuturu kwa waarabu na kusikiliza zile story za kulazimishwa kusmile....utasema kweli.Hayo ndio matunda ya futari za bure kwa waarabu..wachoyo wanaojisifu hadi kwa kila kidogo wanachompa mtu.wanaopenda mtu chakula kwa njia mbaya ili awasifie na kuwashukuru na kuwachekea kila kitu ,kuwasifia kuwa wamesema kitu cha busara hata km hakina busara...

Ndio waliokupa hii story ya alfu lela ulela..na kwa vile usipojichekesha na kukubali basi unayo hatari kwa hasira ya mwarabu.

Waarabu ni wajinga sana pamoja na kwamba ujasiri na ukatili wao unawapa adavantage kwa waoga na wenye fikra za kitumwa.Waarabu kwa uchoyo waliwapa watu maziwa na kuwawekea mkojo ndani yake km kuwadhalilisha, na walipoona kuwa jamaa wamenenepa...waarabu wakaona wivu tena na kudai kuwa mkojo una tiba na Afya..

Okello ndio baba wa taifa la Zenj..
 
wazanzibar ni watu wasio na shukran na wamejaa ukaidi
 
Yadumu mapinduzi matukufu ya Zanzibar chini ya muasisi wa mapinduzi hayo F.M.John Gedion Okello!

Mapinduziiiiiii........Daimaaaaaaa........!!!!!
 
Ni Karume, Okello was just a way and the means, the essence ni Karume.

Tuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuenzi matokeo chanya ya Mapinduzi hayo ambao ni Muungano wetu adhimu ulituzalishia taifa moja tuu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kule Zanzibar wao wana msemo wao was
Mapinduzi Daima
Na sisi Watanzania katika umoja wetu tunasema kwa kauli moja
Tutaulinda Muungano kwa gharama yoyote, na hata kama gharama yenyewe ni kutengua demokrasia kama ilivyofanyika kwenye uchaguzi wa Zanzibar, for the sake of union, demokrasia na itenguliwe! .

Nawatakia mapumziko mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Ukienda Shelisheli hutasikua Jeneral Shimbo au Ngwilizi wakitajwa, Nenda Uganda hutasikia Msangi akitajwa na amekuwa Rais pale , sasa Okello alikuwa Mganda sasa Zanzibar waanze kumsifu Mamluki kwa kuwapigania.
 
J.Okello alikuwa anapiigania nini?

Okello alishajua watz ni kama tulivyo sasa, mtawala anaeza fanya lolote atakalo huku akisikia kelee kwa mbaaliii...

Kwa mujibu wa makala mbalimbali za Ahmedi Rajabu na Mihangwa, inaonyesha mapinduzi yalifanywa na makundi kama matatu, Vijana wa Himran Babu, Okello na kundi lingine ambalo karume alikuwa mwanachama, na ni vigumu kupima mchango wa moja kwa moja mchango wa kila kundi, lakini Karume hakuhusishwa moja kwa moja kny mipango ya uvamizi siku ya tukio, na alipewa madaraka kulingana na political situations ya kipindi hicho.....
 
Heko FM J.G.Okello kwa kuwa mwanamapinduzi uliyefanikisha mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Nimesikitishwa na Rais wa Zanzibar kumtaja Amri Abeid Karume kama muasisi wa mapinduzi hayo wakati alikuwa Tanganyika pindi mapinduzi hayo yanafanyika!

Kwa kweli nimesikitishwa sana na upotoshaji huu wa hali ya juu!
Kwani muasisi mpk ashike bunduki? Nyerere anaitwa mwanamapinduzi ameshika bunduki wp
 
Joni ukelu si mganda ni Mkenya kama sikosei ,na hakuwa kitu chochote isipokuwa alivishwa kilemba cha ukoka na kutomezwa hayo mapinduzi hata baadhi ya vijana wa kiarabu walishiriki kivyao ,kilichopinduliwa si muarabu bali ni serikali huru iliyopokea uhuru ,japo Zanzibar haikuwahi kuwa koloni la Nchi yeyote ile,kwa ufupi pia napenda ufahamu ZANZIBAR haikuwahi kutawaliwa au kuwa koloni ,la muingereza,mreno mjerumani au mualabu ni tofauti na huo upande wa pili !
John F. Okello si Mkenya ni kutoka Uganda.
 
Haujui historia, najua hukuwepo ila unapaswa usome historia

Zanzibar ilipewa Muingereza katika mkutano wa Berlin mwaka 1884 - 1885
Na wewe historia yako ina mapungufu vile vile! Uingereza haikupewa Zanzibar kwenye mkutano wa Berlin. Leo hii huu mtafaruku wa Ziwa Nyasa moja ya visababishi ni hiyo Zanzibar!

Baada ya Mkutano wa Berlin ambao Ujerumani alipewa Tanganyika na Uingereza kupewa Kenya; pale Zanzibar tayari kulikuwa na Sultan. Huyu Sultan alikuwa anatawala Zanzibar na Mombasa vile vile!

Baada ya Waingereza na Wajerumani kuja East Africa; Ujerumani wakadai Zanzibar ni yao na Uingereza wakadai Zanzibar ni yao. Baada ya kutofikia muafaka, pamoja na mambo mengine hapo ndipo ilizaliwa Heligoland-Zanzibar Treaty.

Heligoland ni kisiwa ambacho wakati huo kilikuwa kinakaliwa na Uingereza.

Kufuatia Heligoland-Zanzibar Treaty, Uingereza wakaiachia Heligoland kwa Ujerumani in exchange to Zanzibar & urekebishaji wa mpaka wa Ziwa Nyasa ambavyo vyote vikaenda kwa Uingereza!!!
 
Tukirudi kwenye mada, lililo wazi ni kwamba role ya Karume kwenye mapinduzi ilikuwa ndogo sana!

Architects wakubwa wa Mapinduzi ya Zanzibar ni Umma Party chini ya Abdulrahman Babu. Ni hawa Umma Party ndio walipeleka vijana wao Cuba kuchukua mafunzo ya kijeshi na waliporudi Zanzibar walikuwa tayari wamekwiva kwa mapinduzi!

Si tu kwamba walirudi wakiwa wamekwiva kwelikweli kimapinduzi bali pia walikuwa wamekwiva na itikadi ya ukomunist!

REMEMBER, hii ilikuwa ni takribani miaka 5 tangu kutokea kwa mapinduzi ya Cuba na vugu vugu la ukomunist lilikuwa juu huko Cuba na ndio maana haikushangaza vijana wa Babu walirudi wakiwa ni wakomunist waliokwiva!!

Hata hivyo, Karume alikuwa na mtaji mkubwa zaidi wa watu kuliko Babu kwa sababu Karume alikuwa anaongoza ASP ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa sana Unguja ambako ndiko kwenye population kubwa. Kutokana na ukweli huo, hapakuwa na njia ya mkato zaidi ya Karume na Babu ku-team up ingawaje inasemekana Karume alifichwa suala zima la mapinduzi na kama alifahamu, basi huenda alifahamu kwa juu juu tu!!!

To make story short, katika kufikia mapinduzi palitakiwa awepo kiongozi wa mapinduzi! Kwavile hapakuwa na uhakika wa kufanikiwa, ikaonekana Babu au hata Karume (kama alifahamu) wasiwe mstari wa mbele! Hii ni kwavile, endapo mapinduzi yange-fail na endapo mmoja wao au wote hao wangekuwa ndio viongozi wa mapinduzi; ambacho kingefuata hapo kila mmoja anafahamu na bila shaka harakati zote zingepunguzwa nguvu! Hapa ndipo alipoingia Okello.

Okello akapelekwa mstari wa mbele... ama kwa kufahamu au kutofahamu ili endapo mapinduzi yangeshidwa; jumba bovu lingemdondokea yeye na kuwaacha akina Babu, at least kwa muda!!

Hivyo basi, ambae aliongoza mapinduzi practically ni John Okello raia wa Uganda. Wakati haya yanatokea; si Abdulrahman Babu wala Karume walikuwa Zanzibar bila shaka kwa sababu ile ile kwamba endapo yangeshindwa; wasiweze kuhusishwa na kama wangehusishwa basi ingewawea rahisi kukwepa mkono wa serikali ya akina Shamte!!!!
 
Ukitaka kupata historia sahihi ya zanzibar kuna kitabu kinaitwa short history of Tanganyika kwa tuliosoma zamani kuanzia book five, six,seven na eight utayapata yote
 
Ukitaka kupata historia sahihi ya zanzibar kuna kitabu kinaitwa short history of Tanganyika kwa tuliosoma zamani kuanzia book five, six,seven na eight utayapata yote
Kama ni vitabu vya shuleni basi ni historia ya kupika hiyo!!! Official history ya Tanzania imepikwa sana hadi inatia kichefuchefu!!!
 
Back
Top Bottom