Ni John Okelo au Amri Abeid: mapinduzi

Ni John Okelo au Amri Abeid: mapinduzi

Heko FM J.G.Okello kwa kuwa mwanamapinduzi uliyefanikisha mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Nimesikitishwa na Rais wa Zanzibar kumtaja Amri Abeid Karume kama muasisi wa mapinduzi hayo wakati alikuwa Tanganyika pindi mapinduzi hayo yanafanyika!

Kwa kweli nimesikitishwa sana na upotoshaji huu wa hali ya juu!

Hakuna Amri Abeid Karume kwenye Mapinduzi ya Zanzibar ni Aman Abeid Karume!
 
Tukirudi kwenye mada, lililo wazi ni kwamba role ya Karume kwenye mapinduzi ilikuwa ndogo sana!

Architects wakubwa wa Mapinduzi ya Zanzibar ni Umma Party chini ya Abdulrahman Babu. Ni hawa Umma Party ndio walipeleka vijana wao Cuba kuchukua mafunzo ya kijeshi na waliporudi Zanzibar walikuwa tayari wamekwiva kwa mapinduzi!

Si tu kwamba walirudi wakiwa wamekwiva kwelikweli kimapinduzi bali pia walikuwa wamekwiva na itikadi ya ukomunist!

REMEMBER, hii ilikuwa ni takribani miaka 5 tangu kutokea kwa mapinduzi ya Cuba na vugu vugu la ukomunist lilikuwa juu huko Cuba na ndio maana haikushangaza vijana wa Babu walirudi wakiwa ni wakomunist waliokwiva!!

Hata hivyo, Karume alikuwa na mtaji mkubwa zaidi wa watu kuliko Babu kwa sababu Karume alikuwa anaongoza ASP ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa sana Unguja ambako ndiko kwenye population kubwa. Kutokana na ukweli huo, hapakuwa na njia ya mkato zaidi ya Karume na Babu ku-team up ingawaje inasemekana Karume alifichwa suala zima la mapinduzi na kama alifahamu, basi alifahmu kinagaubaga tu!!!

To make story short, katika kufikia mapinduzi palitakiwa awepo kiongozi wa mapinduzi! Kwavile hapakuwa na uhakika wa kufanikiwa, ikaonekana Babu au hata Karume (kama alifahamu) wasiwe mstari wa mbele! Hii ni kwavile, endapo mapinduzi yange-fail na endapo mmoja wao au wote hao wangekuwa ndio viongozi wa mapinduzi; ambacho kingefuata hapo kila mmoja anafahamu na bila shaka harakati zote zingepunguzwa nguvu! Hapa ndipo alipoingia Okello.

Okello akapelekwa mstari wa mbele... ama kwa kufahamu au kutofahamu ili endapo mapinduzi yangeshidwa; jumba bovu lingemdondokea yeye na kuwaacha akina Babu, at least kwa muda!!

Hivyo basi, ambae aliongoza mapinduzi practically ni John Okello raia wa Uganda. Wakati haya yanatokea; si Abdulrahman Babu wala Karume walikuwa Zanzibar bila shaka kwa sababu ile ile kwamba endapo yangeshindwa; wasiweze kuhusishwa na kama wangehusishwa basi ingewawea rahisi kukwepa mkono wa serikali ya akina Shamte!!!!
"Kinagaubaga" limetumika Ndivyo sivyo...
Muktadha wa neno hilo hurejelea "maelezo ya upana na marefu "maelezo ya ndani
 
"Kinagaubaga" limetumika Ndivyo sivyo...
Muktadha wa neno hilo hurejelea "maelezo ya upana na marefu "maelezo ya ndani
Ahsante... sina shaka utakuwa sahihi manake hata wakati nalitumia hilo neno nlilikuwa najisikia ukakasi kweli kweli lakini kwavile nilikuwa na haraka nikaona taabu kuli-verify!!!

Nilijisikia ukakasi manake huwa nakwazika sana ninaposoma kipande chochote cha maneno kilichobabeba Kiswahili kibovu ikiwa ni pamoja na matumizi ya maneno yasiyo sahihi bila kusahau ugonjwa wa "r" na "l" !!
 
kiongozi wa zanzibar alikuwa anaitwa Abeid Amani Karume siyo Amri Abeid huyu Amri Abeid ni mtu mwingine kabisa jina lake kamili ni Amri Abeid Kaluta,tujifunze kwa makini tunapo soma kuepuka makosa kama haya.
 
Kama nilivyojifunza kwa makini History of Colonialism and Nationalism Zanzibar aliemobilize na kukamilisha mapinduzi kamili ya Zanzibar ni mganda John Okelo na sio Amri Abeid sasa inakuwaje hata kumtambua hatajwi wala kuthaminiwa kama Icon ya Nationalism kwa Zanzibar.

Kwanza nikusahihishe. Yule wa Zanzibar hakuwa anaitwa Amri Abeid bali jina lake lilikie Amani Abeid Karume.....Amri Abeid ni mtu mwingine ambae alikuwa Meya wa Kwanza Muafrica wa Jiji la Dar es salaam, waziri wa kwanza wa Sheria baada ya Uhuru, Mbunge wa Kigoma Magharibi, Muandishi wa Kitabu maarufu cha Kanuni za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Jina la uwanja wa Mpira wa Arusha limetokana nae
Kwa bahati mbaya Watu wengi wanachanganya Kati ya Amani Abeid(Karume) na Amri Abeid (Kaluta) ni vyema ieleweke kuwa walikuwa ni watu wasili tofauti.
 
Kama nilivyojifunza kwa makini History of Colonialism and Nationalism Zanzibar aliemobilize na kukamilisha mapinduzi kamili ya Zanzibar ni mganda John Okelo na sio Amri Abeid sasa inakuwaje hata kumtambua hatajwi wala kuthaminiwa kama Icon ya Nationalism kwa Zanzibar.
Mkuu ni kweli kwamba John Okelo alifanya kazi kubwa Ila Huyo mwingine ni Abeid Aman Karume Siyo Amri Abeid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nilivyojifunza kwa makini History of Colonialism and Nationalism Zanzibar aliemobilize na kukamilisha mapinduzi kamili ya Zanzibar ni mganda John Okelo na sio Amri Abeid sasa inakuwaje hata kumtambua hatajwi wala kuthaminiwa kama Icon ya Nationalism kwa Zanzibar.
Anatambuliwa ila kishingo upande. Leo nlikuwa napitia vitabu vya grade III. NIMEKUTA WAMEANDIKA KUWA JOHN OKELLO NA ABEID AMANI KARUME NDIO VINARA WA MAPINDUZI HAYO
 
Someni kwaheri ukoloni,kwaheri uhuru.kina madini ya kutosha kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom