Ni jairo au mfumo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni jairo au mfumo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shoo Gap, Aug 26, 2011.

1. Shoo Gap

Shoo Gap JF-Expert Member

#1
Aug 26, 2011
Joined: Mar 11, 2009
Messages: 236
Likes Received: 5
Trophy Points: 35
Wahenga wanasema sarafu ni pande mbili, usipojua upande wa pili wa sarafu kwamba uko je, huwezi kutoa hukumu. Lakini mimi leo niseme kuwa dadu(die) ni pande sita mmoja ukiangalia juu, mmoja utaangalia chini na pande nne zitaangalia pembeni. Swala hili la Jairo huwezi kuliangalia kama shilingi kwani halina pande mbili tu, ni zaidi ya mbili.

Nilipomsikia Mb Nimrodi Mkono nilielewa kuwa, wapo wanaomchumkia Jairo kutokana na kuhitilafiana alipokuwa Katibu wa Mkulu pale Mjengoni, lakini huyu huyu anayechukiwa anapendwa na baadhi ya watendaji walioko chini yake kiasi cha kumpokea aliporudi ofisini haswa wale wa kada za chini. Lakini hii haitoshi, wachunguzi wa mambo wanasema pia jimboni mwake alishaombwa agombee u-MP, na hili linaweza likatokea baadae, hivi navyo ni vita haswa kwa wale waliohodhi majimbo.

Wapo wanaopiga chapuo kuwa alitazamiwa kumrithi KKM aliyepo kwani muda wake nasikia umefika ukingoni, hivi navyo ni vita vingine. Wapo aliowazibia ulaji katika Sekta za Madini, Umeme na Mafuta, hivi navyo ni vita vingine, kwani nani asiyejua kuwa wadau wengi wa sekta hizi ni wanasiasa? Kutokana na siasa 'uchwara' zinazoendelea za makundi na kuchafuana wapo wanaopambana kumdhoofisha yeyote aliyekaribu na mkuu wa kaya, hivyo naye kaangukia katika uchwara huu.

Hamaki ya PM siku ile aliposema JK yuko angani lakini angalikuwa na mamlaka angalifanya maamuzi hima, linagubikwa na tetesi kuwa wapo watu ambao wako close na mkuu wa nyumba kuliko yeye mwenyewe, hivyo kauli ile ilitokana na gundu. Lakini pia kauli ile ilitokana na pressure aliyopewa kwenye kikao cha wabunge wa chama tawala. Kwa hiyo akashindwa kui-accomodate, si mmnamjua huyu mtoto wa mkulima feki ni mtu wa kuonyesha hisia zisizoeleweka? Angeweza kulia pale!

Wananchi wengi wamemwona Jairo kama fisadi wa kutupwa kwa kukusanya pesa na kuwahonga wabunge, ingawa swala la hongo limekosa mshiko kwa kutothibitika according to KMK report+CAG. Hapa kuna maswali pia mbona kashikiwa bango huyu bwana, waliopokea hizo hongo mbona hawatajwi, mbona hawachunguzwi. Wapo wengine waliotuhumiwa kupokea rushwa katika kamati fulani ya bunge mbona hawaundiwi tume? Watafutwe waliotoa na waliopokea rushwa.

Lakini hili la kuchangisha idara na taasisi, ni Wizara hii iliyofanya hivyo tu, mbona hizi nyingine hazichunguzwi? Lakini tujiulize, hata kama alichangisha kuwezesha upitishwaji wa bajeti wakati fungu la maandalizi ya bajeti yake ilitengwa katika bajeti iliyopita. Tujiulize fedha za Wizara husika zilizoombwa na kupitishwa katika bajeti iliyopita 201/11 walipewa zote?

Najua constructive critism huwa zinajenga, nazisubiri ili tuendelee kufahamu undani wa issue hii.

2. olele

olele JF-Expert Member

#2
Aug 26, 2011
Joined: Dec 2, 2010
Messages: 814
Likes Received: 339
Trophy Points: 80
umesema hili suala lina pande zaidi ya mbili lakini wewe umeliangalia kwa upande umoja tu ambao unautaka wewe, labda swali la msingi ni kwa nini umechagua huo upande?

3. U

Ulimakafu JF-Expert Member

#3
Aug 26, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 18,015
Likes Received: 743
Trophy Points: 280
Vyote kwa pamoja.

4. Shoo Gap

Shoo Gap JF-Expert Member

#4
Aug 26, 2011
Joined: Mar 11, 2009
Messages: 236
Likes Received: 5
Trophy Points: 35
nimeangalia zaidi ya pande mbili, soma kwa umakini zaidi.

5. The Mockingjay

The Mockingjay JF-Expert Member

#5
Aug 26, 2011
Joined: Jan 11, 2011
Messages: 380
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
Shoo Gap I second you.

There is something very fishy around this Jairo issue. Hata mie namchukia but I have questioned myself why. Na nimemchukia kwa sababu a friend said Jairo mbabe mwonevu ana roho mbaya. Ila sina evidence. In other words, I have been influenced to hate the guy.

Kama kweli wabunge wanataka tuwaone wa maana, wafanye kwenye uchunguzi kwenye wizara zote.
Wabunge waliopokea hiyo hongo wafunguliwe mashitaka na kuachia ubunge wao na majimbo yao yawe wazi kama Igunga.

Short of that, bunge letu tukufu litakuwa linatuchezea akili.

6. olele

olele JF-Expert Member

#6
Aug 26, 2011
Joined: Dec 2, 2010
Messages: 814
Likes Received: 339
Trophy Points: 80

unachojaribu kusema ni kua Jairo ameonewa na alikua sawa kuomba/kushnkza zile pesa kwa sababu pia wizara zngne zinafanyaga lkn haujasma kma ni halali au c halali, caus kosa linabaki kuwa kosa tu bila kujali mmefanya wangapi. Hv nani anaweza kujua mchanganuo wa matmiz yake, je tuna uhkika gani zilpoishia ndo maana ni rahsi kusema zilikua kwa ajili ya hongo ,

7. Shoo Gap

Shoo Gap JF-Expert Member

#7
Aug 26, 2011
Joined: Mar 11, 2009
Messages: 236
Likes Received: 5
Trophy Points: 35

Thank you umenielewa kiasi. Tatizo la watu wengi wanashawishiwa kuchukia watu bila kujua undani wao na tuhuma wanazopewa. Ni lazima kufikiria critically kabla hujamchukia mtu binafsi. Mfumo wetu ndo wa kuchukia kwa kuacha mianya ya watu waovu kufanya uovu wao na kuachwa.

8. Shoo Gap

Shoo Gap JF-Expert Member

#8
Aug 26, 2011
Joined: Mar 11, 2009
Messages: 236
Likes Received: 5
Trophy Points: 35
Huo ni mtizamo wako kwamba ninaona Jairo kaonewa ingawa huo sio mtizamo wangu, lengo langu lilikuwa kuzidi kufikirisha watu, kabla ya kufanya hitimisho. Kama Wizara iliomba hazina fedha za maandalizi ya bajeti na hizo fedha wakapewa zote, atakuwa na la kujibu. Ila kama waliomba fedha na hawakupewa zote, tunapaswa kumsifu Jairo kwa kuwa creative kutafuta fedha za kuwezesha bajeti. Hatuwezi kufanya conclusion pasipo kufanya uchunguzi kwamba alikusanya fedha za rushwa.

9. Mtz-halisi

Mtz-halisi Member

#9
Aug 26, 2011
Joined: Nov 28, 2009
Messages: 47
Likes Received: 0
Trophy Points: 13
Naunga mkono, Tume ingeundwa kuwachunguza wabunge kwanza. Kama hakuna mbunge aliyehongwa utasemaje ni pesa za hongo!!!!!! Wabunge ndio wezi wetu hapa.

10. M

MWAMWAJA Member

#10
Aug 26, 2011
Joined: Aug 24, 2011
Messages: 12
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Asilimia 100%ni mfumo.ila MCHAKATO WA KATIBA MPYA itaaakuwa ndio mwisho wa mfumo huu.

Loading...