Shoo Gap
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 246
- 71
Wahenga wanasema sarafu ni pande mbili, usipojua upande wa pili wa sarafu kwamba uko je, huwezi kutoa hukumu. Lakini mimi leo niseme kuwa dadu(die) ni pande sita mmoja ukiangalia juu, mmoja utaangalia chini na pande nne zitaangalia pembeni. Swala hili la Jairo huwezi kuliangalia kama shilingi kwani halina pande mbili tu, ni zaidi ya mbili.
Nilipomsikia Mb Nimrodi Mkono nilielewa kuwa, wapo wanaomchumkia Jairo kutokana na kuhitilafiana alipokuwa Katibu wa Mkulu pale Mjengoni, lakini huyu huyu anayechukiwa anapendwa na baadhi ya watendaji walioko chini yake kiasi cha kumpokea aliporudi ofisini haswa wale wa kada za chini. Lakini hii haitoshi, wachunguzi wa mambo wanasema pia jimboni mwake alishaombwa agombee u-MP, na hili linaweza likatokea baadae, hivi navyo ni vita haswa kwa wale waliohodhi majimbo.
Wapo wanaopiga chapuo kuwa alitazamiwa kumrithi KKM aliyepo kwani muda wake nasikia umefika ukingoni, hivi navyo ni vita vingine. Wapo aliowazibia ulaji katika Sekta za Madini, Umeme na Mafuta, hivi navyo ni vita vingine, kwani nani asiyejua kuwa wadau wengi wa sekta hizi ni wanasiasa? Kutokana na siasa 'uchwara' zinazoendelea za makundi na kuchafuana wapo wanaopambana kumdhoofisha yeyote aliyekaribu na mkuu wa kaya, hivyo naye kaangukia katika uchwara huu.
Hamaki ya PM siku ile aliposema JK yuko angani lakini angalikuwa na mamlaka angalifanya maamuzi hima, linagubikwa na tetesi kuwa wapo watu ambao wako close na mkuu wa nyumba kuliko yeye mwenyewe, hivyo kauli ile ilitokana na gundu. Lakini pia kauli ile ilitokana na pressure aliyopewa kwenye kikao cha wabunge wa chama tawala. Kwa hiyo akashindwa kui-accomodate, si mmnamjua huyu mtoto wa mkulima feki ni mtu wa kuonyesha hisia zisizoeleweka? Angeweza kulia pale!
Wananchi wengi wamemwona Jairo kama fisadi wa kutupwa kwa kukusanya pesa na kuwahonga wabunge, ingawa swala la hongo limekosa mshiko kwa kutothibitika according to KMK report+CAG. Hapa kuna maswali pia mbona kashikiwa bango huyu bwana, waliopokea hizo hongo mbona hawatajwi, mbona hawachunguzwi. Wapo wengine waliotuhumiwa kupokea rushwa katika kamati fulani ya bunge mbona hawaundiwi tume? Watafutwe waliotoa na waliopokea rushwa.
Lakini hili la kuchangisha idara na taasisi, ni Wizara hii iliyofanya hivyo tu, mbona hizi nyingine hazichunguzwi? Lakini tujiulize, hata kama alichangisha kuwezesha upitishwaji wa bajeti wakati fungu la maandalizi ya bajeti yake ilitengwa katika bajeti iliyopita. Tujiulize fedha za Wizara husika zilizoombwa na kupitishwa katika bajeti iliyopita 201/11 walipewa zote?
Najua constructive critism huwa zinajenga, nazisubiri ili tuendelee kufahamu undani wa issue hii.