Ni ipi miti bora ya kilimo cha mbao?

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,602
2,000
Kiongozi hiyo miaka 7-8 kwa pinus yawezekana kwa IMPROVED TREE SEEDS .... lakini kwa UNIMPROVED ONES muda huo bado ni IMMATURE TREES .... japo mtaiona imekomaa ....

Ukitaka uione pinus ilofika miaka 10 na zaidi nenda SAO HILL FOREST PLANTATION
Unaweza ukamwona mtoto bonge bonge ukadhani ni mtu mzima, unene wa mti (kipenyo) sio kwamba umekomaa. Tupekue vitabu na tafiti ili tujue mti uliokomaa unatambuliwa kwa vigezo vingapi. Ni sawa na kuku wa bloiler anavyotumika kutosheleza soko la nyama ya kuku, lakini madhara yake tunayajua.
 

mkulima92

Member
Jun 4, 2017
40
195
Mbao bora hutegemeana na matumizi uliyoyalenga pia. kama unahitaji kwaajili ya kuuza nje au mbao ngumu nakushauri upande mitiki.

Mtiki ni mti wenye thamani kubwa sana kwenye soko la dunia kwa sasa kutokana na ubora wake. Inakomaa kuanzia miaka 15 hadi 20.

miche inapatikana morogoro @400 kwa mche mmoja utaletwa ulipo

0757026958
0766006128
 

busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,251
2,000
Kaka asante kwa kusaidia kutoa elimu hii, wadau wengi wanapata taarifa toka vyanzo ambavyo si sahihi, matokeo tunapata mazao feki yasiyo na ubora.

Naomba niseme, ukitaka taarifa sahihi za miti pita TTSA Iringa, TTSA Lushoto, TTSA Morogoro na TTSA Arusha. Tusipoteze muda, wakati majibu sahihi yapo ktk taasisi hizo. Toa taarifa na habari za kisayansi kwa kutoa reference official. Kinyume na hivyo ujue unadanganya.
Tuko pamoja kiongozi. By the way thank you for both your COMPLIMENT and your GOOD EXPLANATION too. I'm quite sure the members especially the poster will definitely benefit from your KNOWLEDGE and EXPERIENCE as well.
 

TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Data za miaka 7 na mitiki miaka 15 umepata wapi?, mimi nimezitoa TTSA. Bila kutumia improved seeds/GMO huvuni miti ya mbao kwa ubora unaotakiwa chini ya miaka 20. Mitiki na Cyprus inakula miaka ya kutosha. Labda acrocarpus unaweza vuna baada ya miaka kumi.

Ila kama unavuna kwa kuibaka miti sawa, hata miaka miwili inawezekana.
Zipo modified GMO technology ya kupunguza umri wa miti Kwa kuharakisha ukuaji badala ya hio 15 au 20 ukavuna kuanzia miaka 8 hadi 10 ukapata ubora na ukubwa sawa tu na wa miaka 20,kuna dawa za kuchoma miti,ni kama booster za mazao vile
 

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,602
2,000
Zipo modified GMO technology ya kupunguza umri wa miti Kwa kuharakisha ukuaji badala ya hio 15 au 20 ukavuna kuanzia miaka 8 hadi 10 ukapata ubora na ukubwa sawa tu na wa miaka 20,kuna dawa za kuchoma miti,ni kama booster za mazao vile
FDT Iringa wanasambaza mbegu hizo, ila mwitikio umekuwa hafifu sbb ya mbegu zake kuwa ghari balaa. Wana shamba pale Kisolanza/Rungemba, kwa anayetaka ni vema akachapa lapa ili akajifunze kwa vitendo zaidi.
 

pelezicr

Member
Jun 30, 2016
24
45
Unaweza ukamwona mtoto bonge bonge ukadhani ni mtu mzima, unene wa mti (kipenyo) sio kwamba umekomaa. Tupekue vitabu na tafiti ili tujue mti uliokomaa unatambuliwa kwa vigezo vingapi. Ni sawa na kuku wa bloiler anavyotumika kutosheleza soko la nyama ya kuku, lakini madhara yake tunayajua.
Kitaalamu hicho kitu kipo ila kwa aina za Miti tunazozarisha hapa nchini bado hazijaanza kupandwa, kwani haziruhusiwi kutokana na matokeo yake yasiyo sahihi kwa mazao ya Miti yanayohitajika kwa sasa nchini. Hivyo tunaomba ukiona kuna mti au shamba lina utofauti katika mazao hasa ya Miti afadhali wasiliana na wataalamu wa utafiti yaani TAFORI, TTSA au afisa misitu aliye karibu nawe.
 

Jaslaws

JF-Expert Member
May 31, 2011
6,036
2,000
Nmepanda mi pyne huu huko bukoba..huu sasa ni mwaka Wa 4 miti bado midogo tu sasa nikisikia mtu anasema mi pine miaka 7 unavuna najua sielewi, unless kama udogo unatofautiana.
 

lukinga01

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
327
500
Nmepanda mi pyne huu huko bukoba..huu sasa ni mwaka Wa 4 miti bado midogo tu sasa nikisikia mtu anasema mi pine miaka 7 unavuna najua sielewi..unless kama udogo unatofautiana..
Ndio mkuu kuna utofauti wa udongo na hali ya hewa. Mm nina miti ya miaka kuanzia mwaka mmoja mpaka kumi katika wilaya ya Makete mkoani njombe ndg yangu miti inakua hiyo mpaka balaa. Kuna mwaka nilisikia huko kwenu ni moja ya sehemu ina mvua nyingi nikataka nije nifanye utafiti kama naweza pata ardhi nipande na huko. Lkn bahati mbaya ratiba ilinikaba nikashindwa. Vp bei za ardhi huko imekaaje?
 

lukinga01

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
327
500
Mi mwenyew nlidanganywa pyne ni miaka saba kumbe pyne hadi ikomae ni miaka 15
Wapi huko mkuu? Miaka hiyo 15 kwa Makete unapiga pesa ndefu sana. Kule watu ni kweli wanavuna miti ya miaka 7 na kuendelea mpaka hapo 15 inategemeana na ardhi ilipopandwa hiyo miti. Kama umepanda kwenye ardhi nzuri unaweza pata zaidi ya 150,000/= kwa mti mmoja kwa hiyo miti ya miaka 15. Karibu tuwekeze Makete mkuu.
 

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
1,719
2,000
Upo wapi? Kwa mkoani iringa wilaya ya mufindi. Miti aina ya mlingoti ndio bora zaidi. Kwanza inakua haraka. Pili mbao zake zinatumika katika uselemala. Ngoja tusubiri na wadau wengine wanasemaje kuhusu hilo.

Sent using samsung galaxy grand prime pro
 

pelezicr

Member
Jun 30, 2016
24
45
Nmepanda mi pyne huu huko bukoba..huu sasa ni mwaka Wa 4 miti bado midogo tu sasa nikisikia mtu anasema mi pine miaka 7 unavuna najua sielewi..unless kama udogo unatofautiana..
Hongera sana na pole kwa mkasa uliokupata.

Ila kwa ushauri wangu ni vyema kabla ya kupanda kuhakikisha ni aina gani ya Miti inaweza kustawi katika eneo husika ili kupunguza hasara zinazoweza kuzuirika.

Pia sina hakika kama ulifuata taratibu zote za njia bora na na sahihi kwa upandaji wa Miti.

Kuanzia kwenye ukuaji wa miche ya Miti, kuchimba mashimo pamoja na upandaji wa Miti kwenye shamba.
Ingia hapa kwa msaada zaidi; Uwekezaji Bora na Mazao Bora ya MitiBiashara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom