Ni ipi Logic ya kumpeleka mtoto wa miaka 5 Bording School?

Leo kama kawaida ndio wanafunzi wanajiandaa kurudi shule kwa ajili ya kesho kuanza Masomo.

Sasa kwenye pitapita zangu nikakutana na vitoto nadhani vina miaka Minne hadi Mitano viko na wazazi wao na vimevalishwa uniform. Nadhani ile ndo point ya wao kukutania ili watoto wabebwe kwenda shule.

Wale watoto ni wadogo mno mno muda kama ule na baridi la Arusha walitakiwa wawe wamelala.

Sijajua tunakwama wapi aisee, mbona hata kuku au hata Wanyama wanatuzidi akili inapokuja swala la kutunza watoto?

Ni ubize wa kiwango kipi unaofanya mzazi kupeleka mtoto wake wa miaka minne Bording?

Hivi linapokuja swala la mtoto kweli kuna Optional? Kwamba watu wanachagua pesa badala ya watoto?

Kwa sababu kupeleka mtoto mdogo Bording ni kwamba Mzazi yeye pesa ndo kila kitu na sio mtoto.

Then utasikia Mzazi anasifia shule kwamba ile shule ina Matron mzuri sana ina Mazingira mazuri sana, wanakula chakula kizuri sana, wana Vitanda vizuri na kadhalika, Huu ni ujinga wa kiwango cha kutisha.

Mimi nililelewa kijijini nilikuwa nakunywa uji bila sukari make hakukuwa na pesa ya sukari lakini nilitunzwa na wazazi na nilikuwa na furaha.Tulikuwa tunalalia ngozi za Ng'ombe ila tulikuwa na furaha na amani.

Swala sio mazingira sijui mandhari bali malezi.

Malezi na Mandhari ni vitu viwili tofauti kabisa.

Mnaweza ishi kwenye nyumba ya maturubai na bado mtoto akapata malezi bora kabisa, hata wakimbizi wanaishi kwenye mahema ila wanawapatia watoto wao malezi bora.
Naunga mkono hoja. Wazazi wa kisasa wengi tumekuwa maboya sana
 
Back
Top Bottom