Ni hasara gani kubwa ulishawahi kuipata ikakurudisha nyuma?

Dah pole sana mkuu,dunia ina mitihani sana.
Au wewe ndio yule wa Arusha aliyesema pesa za vicoba zimepotea kwa uchawi.
SIJUI HII YANGU NI KUPOTEZA AMA VIP!!
Nilikuwa mtunza fedha wa kikoba flani!
Fedha ambayo nna uhakika kwamba nilichota na kuwekeza ni around 4m(hii nayo haikurudi baada ya kutapeliwa na kupata hasara pia)
Kuna fedha nadhani nilishindwa kuipigua hesabu vizuri hivyo wakopaji walinifaidi ni around 1.5m
ILA MPAKA MWISHO NILIJIKUTA NINAPUNGUFU YA M.16.Mpaka leo nina kesi mahakamani.1.Nilifanya juhudi za kuwalipa kidogo kidogo(about 3M(sasa eti hawaitambui)
2.Nimehangaika sana na dhamana(pesa imetembea)400,000.Hii ilihitajika kwa ajili ya kufanya tathmini ya dhamana iliyotakiwa.
3.Nimetapeliwa na huyo huyo aliyeniwekea dhamana na ni mtu na heshima zake(usimwamini mtu hivihivi)500,00/-
Nimelipia gharama za mawakili.400,000/-.Huyu alinifanyia kwa kuwa ananijua
Mpaka leo naishi kama kiokote,heshima hamna tena.pesa napata za kuokoteza hivyo nafanya kazi za dharau sana!
Vitu vingi nishauza!!
Pesa inanitesa haswaaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee nilitaka nisiseme kitu ila nilipo soma visa vya wenzangu nimegundua kuna ya kujifunza hapa kupitia wengine

Kwanza nimpe pole yule alie wekeza Dada yake na shemeji waka mzima aisee huo ni ukatili pia una moyo ningekuwa mimi ninge wachoma moto nili kisoma jana lakini hadi leo roho ina niuma kama nime fanyiwa mimi pole sana!

Pia ulie tapeliwa mzigo wa stationary pole yote ni mapito ina uma sana ila hatuna budi kupambana

Niseme kisa kuhusu mimi hapa nilikuwa nakaa kwa sister nikapata kazi kinyerezi kwa mtu nyumbani kwake nika sema acha niende nika piga kazi fresh kwa uaminifu wa hali ya juu kama kawaida yangu mama yangu ame nilea vema nika leleka na ana niamini kuliko sote alivyo tuzaa basi baada ya kupiga kazi kwa muda mama yangu kuna siku ali nipigia simu kuwa kuna pesa ame pata nifikirie biashara ya kufanya kama Mil 5 hivi, ili niweze kusaidia familia na kumsomesha mdogo wangu alikuwa kaanza form 5 Tabora (W) Kaliua

kwa haraka kwa sababu mimi ni dereva nika sema hapa ni nunue bajaji maana kwa gharama za uendeshaji sio kama gari

Siku zika fika Mother akanipa Mil 6.5 kuna rafiki yangu nika muagiza aka enda Bank aka pewa maana nilishindwa kutoka kwa sababu ya kazi nilio kuwa nafanya rafiki yangu aka niletea nika zihifadhi ila ndugu zangu wali kasirika sana,nika piga hesabu nikaona nyumbani hakuna umeme nika kata kama Milioni 1 nika enda kariakoo na rafiki yangu nika nunua vifaa vya umeme na fundi nika mlipa kazi ika isha ikabaki kulipia 321,000/= Tanesco umeme uwekwe nika sema nikisha anza kazi nita weka nika chukua tena laki 5 yule mdogo wangu alie kuwa ana soma Tabora alivyo sikia mama kanipa pesa aka anza kulalamika kuwa kule shule haifundishi ata feli uki zingatia kasoma shule ya kata O'level tuka mtafutia nafasi Minaki aka anza kusoma huu uhamisho pamoja na michango uli gharimu kama laki 5 hivi

Sasa hapa ilibidi niombe kuacha kazi kwa Boss wangu ili nika endeshe bajaji aka nikubalia ila aliniomba niongeze mwezi mmoja ili atafute kijana mwingine nika sema hapa ninunue bajaji mapema maana pesa za masikini hazikai ili bidi ile bajaji nimpe dereva aanze wakati nasubiria kuacha kazi nilipo acha kazi nika chukua bajaji nika i park kwa yule dada yangu jirani yake ni askari ili kuifanyia service maana haikuwa katika hali nzuri basi Tarehe 04/06/2017 Asubuhi naona simu ina ita yule jirani wa dada yangu ana nipigia simu Uncle njoo Bajaji ime ibiwa aisee nili iona dunia nime ibeba ghafla nika chukua boda faster nika fika kweli bajaji haikuwepo ime ibiwa kufuli la geti lime vunjwa basi tuka enda polisi kufungua kesi lakini hakuna kilichojiri mwisho wa siku nili shukuru mungu nika enda nika mueleza mama ali nielewa lkn kwa ndugu hawaku amini wanajua pesa nime tumia na rafiki zangu japo Doc's zote zilikuwepo hadi leo nikiona bajaji nazichukia sana sito kuja kumshauri mtu wa karibu yangu anunue bajaji au pikipiki lakini maisha yangu yame haribika hadi nilijuta kuacha kazi lakini napitia wakati mgumu sana hadi nime pata vidonda vya tumbo pia roho huwa huwa ina niuma nikienda nyumbani kuona nyumba haina umeme mama yangu bado ana lala gizani In all Mungu hakupi mtihani ambao huuwezi kupambana tuu!
Pole sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2018 nilitumia kampuni ya rafiki yangu kufanya mradi tukakubaliana yeye asiingize pesa yoyote lakini nitampa mil 21, Nikapambana nikamaliza kazi alafu nikawa nimeacha ajira yangu hivyo nikaomba malipo ya mwisho.
Jamaa alivyoona nimeacha kazi alidhulumu mil 23 maana alikata mil 44.
Nilimwambia kitu kimoja tu, Ukipambacho ndicho utakachokivuna, unatamani nisiinuke lakini nitainuka tu.
Leo hii nina kampuni 2 na hivyo nina miradi kumzidi.
Katika maisha yangu sijawahi kuwa na msamiati wa kushindwa toka nikiwa mdogo hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
ASANTEEEEEEEEE..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nantombe umeuliza swali fikirishi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona kujua ni rahisi sana,ukiwa unafuga kibiashara lazima kunakuwa na wafanyabiashara kama wewe na mnakuwa mnawasiliana hivyo kama wao waliendelea kufuga labda kwa kuwa na mitaji mikubwa walimwambia ugonjwa umepotea. Mimi nilishalima nyanya ugonjwa ukaingia dawa ikawa ghali na inatoka Kenya nililikimbia shamba kwa kuwa sikuwa na mtaji ila jirani yangu alikomaa na zile dawa kwa kuwa alikuwa na nguvu na siku si nyingi ugonjwa uliondoka
 
Hongera mkuu. Sema ulizingua mwanzo kinoma dah!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha tu mkuu,nilipokua siingizi hata mia niliiona dunia chungu kuliko muarobaini,kila unayejaribu kumuomba hata buku mbili anakujibu sina kitu yani unajikuta unalala njaa hivi hivi.Mimi ilikua kununua mkate wa buku geto kula siku mbili na maji ya bomba ni kawaida ila nashukuru Mola now nakula nachotaka.Yani hali ilibana hadi nikaanza kuelewa kwanini mabasi ya mwendokasi hayapiti Tandale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalia nilivyopalilia...
Umeona hivyo visani?
Moto hata ukiingizwa utagusaje mti na hakuna majani?

Weeding management kwa wakulima wa kibongo ni janga.

#YNWA
Mkuu pruning na fire lines ndio zinasaidia sana, ila miti ikiwa mikubwa ni tatizo sababu ya matawi kule juu, unless iwe mbali mbali sana,
Na usiombee miti iwe ya kundi la Conifer kama pines ilivyo na turpentine(mafuta), ndani ya Nusu saa shamba zima umesimamisha magogo tuu...
 
Mkuu naomba msaada kwenye hii biashara,nikitaka kufungua minimum capital ni kiasi gani? Location inatakiwa iweje kwa experience yako mkuu?
Minimun capital 700k kwa sehemu ambayo kodi nafuu na umeme pia,hapo unaweza ukaanza na mashine moja ya ps2@150k +Tv flat @300k,kodi@100k,Viti meza feni vifaa vingine@150k...Location sehemu yoyote yenye msongamano hasa karibu na shule ama maeneo yenye vijana wengi iwe upenyoni sio sehemu ya wazi.Ukiwa serious Pesa yako itarudi ndani ya muda mfupi na utapanua zaidi biashara yako utaacha fikra ya kuajiriwa ukiwa na matawi mawili au matatu tofuati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Minimun capital 700k kwa sehemu ambayo kodi nafuu na umeme pia,hapo unaweza ukaanza na mashine moja ya ps2@150k +Tv flat @300k,kodi@100k,Viti meza feni vifaa vingine@150k...Location sehemu yoyote yenye msongamano hasa karibu na shule ama maeneo yenye vijana wengi iwe upenyoni sio sehemu ya wazi.Ukiwa serious Pesa yako itarudi ndani ya muda mfupi na utapanua zaidi biashara yako utaacha fikra ya kuajiriwa ukiwa na matawi mawili au matatu tofuati

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani mkuu,ngoja hili janga la korona likipita na Mungu akatuweka hai nitaifanyia kazi hii idea
 
Back
Top Bottom