Jinsi smartphone used ilivyonipeleka polisi

contask

JF-Expert Member
Jan 3, 2021
257
438
Habari wanajukwaa,

Leo nimeona niwaelezee smartphone ilivyonipeleka polisi katika kituo ca msimbazi then njkahamishwa hadi kituo cha Mbweni kilichopo Bagamoyo Road, nisiwachoshe ngoja niende moja kwa moja kwenye kichwa cha uzi wetu.

Mimi ni kijana nipo chuo fulani nikiwa najihusisha kuuza simu plae Kariakoo. Sasa siku moja kuna rafiki yangu naye anapiga mishe za uwinga pale Karikaoo kuuza hizi smartphone hasa used from Dubai aliniunganisha na jamaa mmoja yupo pale Navy Kigamboni, alitupigia simu siku moja akiwa anauza simu ya siku moja na kutuambia kwamba ana simu yake Samsung Note 10 Plus anaitoa kwa laki mbili tu (200000) kutokana na sababu zake binafsi.

Alituchek, tulitafuta hela tuinunue then tuje tuize katika price yake ambayo inarange 450k hadi 400k ikashindikana maana tulikosa pesa. Sasa ilipita kama mwezi hizi asubuhI akanipigia, akaniambia kuwa anasimu nyingine kama ile maana alinunua mbili yake na ya mke wake anaiuza laki mbili tu. Nilifurahi sana na kuona dili la hela limekuja lenyewe bila nguvu na wakati huo kwenye account yangu kulikuwa na ela kama 430k.

Nikaona sio kesi nitoe 200k ninunue simu the nije kutengeneza faida, kweli nikampigia simu nikafika hadi pale kambi ya Jeshi Navy Kigamboni akatoka akaniletea simu nikaiona kwa hakika ilikua ipo clean no dot na krek kwenye kioo, ila kreki kidogo kwenye back glass ila ilikuwa sio tatizo, nikanunua nikaondoka nayo nikafika home kisiwani ambako nayo ipo Kigamboni ni wastan wa dakika 10 hadi kufika Navy Ferry nikachukua nguo niende nyumbani Kisarawe kama ilivyokuwa kawaida yangu kila Ijumaa naenda Kisarawe narudi Jumapili.

Niliondoka na ile simu usiku yule jaama yangu ananipigia kuwa amapata mteja wa ile Samsung Note 10 Plus alikuwa anaitaka kwa 360000 kesho yake jioni nikapanda gari haraka Kisarawe to Gongo la Mboto then nikapanda gari za Temeke nikashuka Sudan ni sehemu ambayo tulipanga tukutane baada ya nusu saa jamaa kafika na mteja biashara haikuachukua muda mrefu ndani ya dakika 10 tu mteja kalipia ile simu 360000 nikachukua 50 nikampa jamaa yangu ambae aliniletea mteja then nikaendelea na safari hadi nyumbani Kigamboni maeneo ya Kisiwan nikawa nimetulia napanga matumizi ya profit ambayo nimeipata.

Wakat huo yule jamaa yangu kampeleka jamaa yangu Kariakoo kubadilisha mfuniko wa nyuma, picha ndio lilianzia hapo!
 
Sikuhizi simu hasa hizi zilizo nje ya maboks, hata kama ni dukani usiingie kichwa kichwa...

1. Ukinunua simu nenda kwenye Phone status hakikisha ni Official sio Custom, hizo ni za mbio wanazibadilisha imei, ndio Kwa kupitia imei UNAWEZA usikamatwe ila siku uka restore tuu, kwisha habari yako., haitashika network, ukilazimisha kuirudisha upo nyavuni..
Screenshot_20240514_104931_Settings.jpg


2. Hakikisha pamoja na kupewa Risiti ya ki electronic (hizi mimi hua sizikubali kabisa, hua hazioneshi model, imei n.k) omba risiti ya mkono, model ya simu iandikwe,
Imei number iandikwe, hii imei ifanane na ya kwenye boksi, ndani ya simu/software na oia i match na ya kwenye hardware yasimu, namaanisha nyuma ya simu(kama ipo)

3. Piga picha pale pale dukani,
4. Haikisha unapata mhuri na risiti ni ya duka lao,
5. Hakikisha unauziwa ndani ya duka lao(kuna mawinga wanajisogeza na fremu ya mtu anajifanya ni yake, kumbe umesetiwa, mkimaliza biashara anasepa, siku umepata la kupata, unaenda unakuta mawingu.

Simu ya Mkononi..

1. Hakikisha namba Mnayotumia kuwasiliana na muuzaji ni yake, imesajiliwa kwa ID yake..
2. Omba kitambulisho, kipige picha kikiwa na simu, na pesa unayompa.
20221212_123606.jpg

3. Piga naye Selfie/record video akiwa ameshika ID yake na makubaliano ya mauziamo..
Screenshot_20240514_103552_Gallery.jpg


4. Fanya biashara hio nyumbani/ofisini au basi uchukue namba ya mtu wake wa karibu, huyo mtu umtafte wewe..

Shtuka ukiona haya.
1. Muuzaji wa simu anasema ni yake lakini haitumii inasoma imergence.
2. Phone status inasoma Custom.
3. Muuzaji anakuambia exchange allowed lakini haweki conditions zozote na ukiangalia simu ni ya gharama.
4. Muuzaji ana namba za simu nyingi kupitiliza,
5. Muuzaji kaweka tangazo, hajaweka namba ya simu anakumbia weka yako, au nenda PM
Nimepiga sana u winga, Nina scenario nyingi sana ambazo ziliniokoa.

YOTE HAYA YANAWEZA KUA MATESO,
NENDA SHOP YA KUELEWEKA ZAMA MFUKONI VIZURI, NUNUA KITU SEALED.
NOTE : SEALED na FULLBOX ni vitu viwili tofauti.
 
Baada ya kama dakika 40 hivi nilimuona yule jamaa yangu akiwa na jamaa mwingine simfahamua alikuja nae ambae alionekana ni kama rika letu.

Akaanza kunihoji kuhusu simu nimenunua wapi na anahitaji kumpata mtu amabe amenunua maana walishindwa aliwatoka na mbaya zaidi kitu ambacho kinaniuma ni kwamba mwenye simu aliifananisha ile simu kupitia mvunjiko wa kioo cha nyuma cha ile simu.

Tulianza kubishana na yule askari mwisho nikamwambia atoe kitambulisho akatoa ila bado niliendelea kumbishia kwa point ya kwamba huwezi tafuta simu kupitia muonekano tafuta kwa kutumia vielelezo.

Askari akachukua simu yangu ilikuwa Samsung s20 utra anataka nitoe lock nikamkatalia maana nilijua ni matapeli kwanini nimpe wasiliano ili akutane na yule jamaa ambae nimemuuzia ili akutane nae amtapeli acopy imei akatengeneze warranty na risiti apate vithibitisho.

Niliendelea kumkatalia kuwa namba ya niniyemuuzia simu sina. Wakati huo nilikuwa na jamaa yangu ambae aliniletea yule mteja mwishowe polisi akasema nipande boda yeye atalipa, simu yangu nikaichukue kituoni Msimbazi tukaendelea kubishana nae tena kama askari kwanini unipeleke Msimbazi wakati kituo cha Kigamboni kipo?

Mwisho nikaona sio kesi tukapanda pikipiki mimi na jamaa yangu yeye alipanda bajaji na mtu ambae anasema simu ni yake akiwa na rafiki yake tukafika hadi Msimbazi kituo cha polisi halafu yule askari akaishia zake wakati ashanipa simu yangu tayari tukawa tuko pale mapokezi tukahojiwa.

Nikaonekana mimi ndio niko na fact huwezi tafuta simu kwa muonekano bali kwa vielelezo askari akamwambia kila mtu atume vielelezo ali ahakiki akiona tofauti simu so yake kweli mtu ambaye aliniuzia alipigiwa simu akasema apewe muda kidogo aitafute atamtumia yule polisi wa pale msimbazi ahakiki, yule askari akaniambia tuondoke MWISHOE AKATOKEA ASKARI MWANAMKE AKASEMA "HUYO ASIONDOKE NI MWIZI AKAE NDANI"

Niliumia sana nikaacha vitu vyangu nikaingia mahaubusu na ilikuwa mara ya kwanza kuingia mahabusu pale Msimbazi bila kujua natoka lini na muda gani nilianza kuchanganyikiwa hali ya kuwa kuna mtu anakuambia hana kesi anasubiri dhamana ana kama wiki mbili hivi.

Mimi siku moja naona kama mwaka kwa ambao wameenda wataelewa hako kafeeling nilikaa mule ndani sielewi hali ya kuwa nilikuwa nimefunga hiyo siku na sikula chochote zaidi ya kipande cha mkate.

Kitu ambacho kilikuwa kiliniondoa wasi wasi nilifanikiwa kupiga simu kwa mama yangu kumuambia aje kunitoa niko polisi.
 
Back
Top Bottom