Ni halali mishahara minono kwa vongozi wa baadhi ya mashirika ya umma?

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Mkisema ni wivu, nitakubali ila kwa hili la baadhi ya viongozi wa mashirika ya umma, tena yasiyozalisha, kujilipa mishahara mikubwa (TZS 20m-40m kwa mwenzi)lazima nikiri linaniuma na si halali kabisa:

1) mashirika kama TCRA, TPDC, EWURA, na NSSF hayausiki kabisa na uzalishaji zaidi tozo za wanachama.
2) Ripoti ya CAG imeonesha ndiyo mashirika yenye madudu ya utendaji.

Je kuna vigezo vyovyote vya kuhararisha mishahara minono hiyo? Wanajamvi msaada.
 
hizo ni taacc nyeti zinazohitaji wataalamu wa hali ya juu na wenye uzoefu wa pekee na hata wa Kimataifa. jamii ya kimataifa imekuwa ikilipa mishahara minono watu wa hizo fani. kuwapunguzia mishahara ni kuwafukuza hapa nchini wakati tunawahitaji. pia kumbuka mishahara midogo ni kichocheo cha rushwa. yanaonekana kufanya vibaya kwa sababu JK hakuwa makini nao. sasa ni Dk. Magu akiwalipa vizuri hawataiba na wakiiba bac wafungwe! walipwe mishahara minono. wakurugenzi wakuu wapewe hadi 40M.
 
hizo ni taacc nyeti zinazohitaji wataalamu wa hali ya juu na wenye uzoefu wa pekee na ...kuwapunguzia mishahara ni kuwafukuza hapa nchini wakati tunawahitaji.
..pia kumbuka mishahara midogo ni kichocheo cha rushwa.
...yanaonekana kufanya vibaya kwa sababu JK hakuwa makini nao.
1) Kuna taasisi nyeti kuliko zinahusika na elimu (walimu na wahadhiri)!
2) kama mishahara midogo ni kichocheo cha rushwa inakuwaje hizo taasisi ndo zinaongoza kwa ubadhirifu 3) inakuaje taasisi wanazozuongoza hao wataalamu ndizo zineripotiwa na CAG kuwa na utendaji mbovu!
 
1) Kuna taasisi nyeti kuliko zinahusika na elimu (walimu na wahadhiri)!
2) kama mishahara midogo ni kichocheo cha rushwa inakuwaje hizo taasisi ndo zinaongoza kwa ubadhirifu 3) inakuaje taasisi wanazozuongoza hao wataalamu ndizo zineripotiwa na CAG kuwa na utendaji mbovu!
nishasema ndugu kuwa hapo nyuma JK aliharibu
 
Back
Top Bottom