Ni halali kwa wakuu wa Mikoa na wilaya kuvaa nguo za CCM?

Kwanini walipwe na fedha za Umma wakati wanafanya kazi za chama?

Siasa kwa ujumla wake inahudumiwa na serikali ileile kwakodi ya wananchi. Hivi unafahamu kwamba vyama vya upinzani vinalipwa ruzuku(kodi ya wananchi). Malipo ya viongozi wa vyama yanatokana na hiyo ruzukuambayo ni kodi kupitia serikalini. Wabunge wanawakilisha vyama nao wanalipwakupitia kodi za umma.
Jaribu kufuatiliakila chama kinakamata ruzuku kiasi gani? zote hizo ni fedha za umma

 
Hawa ni viongozi wakisiasa wanaomuwakilisha raisi,wanahaki ya kuvaa sare za CCM
Kwa hiyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye yeye hakuvaa nguo zinazoshabihiana na rangi za chama hamuwakilishi Rais? Kumwakilisha Rais sharti uvae kichama-chama?
 
Acha hizo.hawana haki ya kuvaa nguo hizo maana mishahara yao hawagharamiwi na ccm bali kodi za wananchi wenye vyama na wasio na vyama.

Na hivi vyeo havina haja ya kuwepo maana hawana kazi mikoani na wilayani zaidi ya kuvuja jasho la walalahoi bure.

Ndugu yangu unabisha bure!Hao ni makada wa CCM na nafasi zao ni za kisiasa na sikuwatumikia watanzania wote.Na ndiyo maana ni wapingaji wazuri wa vyama vya upinzani.Ukinikatalia basi haujui kazi zao na wako hapo kwa niaba ya nani.Kulipwa mishahara kwa kutumia kodi zetu hilo nalo suala lingine ndiyo maana tunataka katiba itakayowaondoa hawa watu.
 
ni halali kabisa mana vyeo vyao ni vya kisiasa ndo mana mmoja ni mjumbe wa ccm wilaya na mwingine mkoa
 
Serikali ijayo ya TANGANYIKA ITAVIFUTILIA MBALI VYEO HIVYO AMBAVYO IMEFAHAMIKA SASA KWAMBA NI SEHEMU YA ULAJI TU NA WALA HAVINA UMUHIMU WOWOTE .
 
Mbowe analipwa fedha za UMMA pia lakini anafanya kazi za UKAWA.

Sasa nimeamini kuwa wewe ni ...... Na kuanzia sasa siwezi kukujibu mahali popote. Kuna msemo wa kiingereza unasema "never urgue with a fool people might not ..........."
Sasa nami nahofia kunipata hayo! Maana ulichoandika ni eitha uko kwenye kundi nililotaja au umelewa.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Serikali ijayo ya TANGANYIKA ITAVIFUTILIA MBALI VYEO HIVYO AMBAVYO IMEFAHAMIKA SASA KWAMBA NI SEHEMU YA ULAJI TU NA WALA HAVINA UMUHIMU WOWOTE .

Lakini wanyewe CCM kwa vile wameiwezesha katiba ya sasa kuwapa madaraka makubwa sana hao ma RC na DC ya kuweza kuweka watu ndani bila kuhojiwa basi wanawatukuza sana. Nafikiri umeshasikia mara nyingi madiwani wa vyama vya upinzani wale wenye usubutu wanavyo fanyiwa mara kwa mara na watu hawa.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Old habits die hard. Hawajitambui wala hawajui wajibu wao kwenye mazingira ya siasa ya yvama vingi.
 
Mbowe analipwa fedha za UMMA pia lakini anafanya kazi za UKAWA.
Umeelewa kweli wewe bulumunda?au unaropoka na hujaelewa hoja ya muuliza swali?tafsiri yake ni kuwa wakuu wa mikoa na wilaya walitakiwa kulipwa na ccm kama chama na sio serikali kama watumishi wa umma wakati wanatumikia chama.uwe muelewa sio juha.
 
Umeelewa kweli wewe bulumunda?au unaropoka na hujaelewa hoja ya muuliza swali?tafsiri yake ni kuwa wakuu wa mikoa na wilaya walitakiwa kulipwa na ccm kama chama na sio serikali kama watumishi wa umma wakati wanatumikia chama.uwe muelewa sio juha.

Mbowe analipwa nani?
 
Back
Top Bottom