Ustaadh
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 413
- 19
Kuna baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya ambao huvaa nguo zinazoshabihiana na rangi za bendera ya chama tawala wakati wa kuwapokea viongozi wa kichama. Hivi ni halali wao kufanya hivyo na hasa ukizingatia wao ni wanaongoza wananchi wote bila kujali itikadi za vyama? Picha kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya akiwa na Bw. Kinana na picha kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tabora akiwa na Bw. Nape Nnauye.