Ni haki kufunga mitaa ya umma kwa ibada binafsi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,052
40,715
Hivi kuna logic gani watu kuwa na haki ya kufunga barabara za umma zilizopigwa lami kwa kodi za umma ili kufanya shughuli binafsi za ibada? Kwani viwanja si vinauzwa...

Kwanini mtumie barabara muhimu na kuzifunga? Kama nyumba yenu ya ibada haitoshi, basi changishaneni pesa mumnunue jirani yenu ili mtanue eneo lenu...

Mbona wengine huenda kuanzisha nyumba za ibada kwenye mapori, na eventually miji hudevelop kuwafuata kutokana na huduma za kijamii zinazotolewa sambamba na huduma kiimani? Hebu tubadilike bwana.
 
sasa ukienda Zenji si ndio utashangaa!!?maana mpaka Shein mwenyewe anashiriki kufunga barabara!hata mimi kwa upande mwingine siliafiki hili suala.

Kwanini wasiazime hata viwanja vya shule au vya mipira??mimi pia nakerekwa sana na hili!!
 
Hivi kweli mtu anaweza kuwa anafanya ibada peke yake na barabara ikafungwa? Ama nini maana neno binafsi, kama walikuwa ndiyo uma unaongelea huo au neno uma kwako wewe linamaana gani? punguzeni chuki hazijengi bali zinabomoa.
 
Jaim Siku moja nilikuwa naenda kwa jamaa yangu mwananyamala kwa kopa, naingia barabara kuelekea nakuta jamaa wamefunga turubai kukatiza barabara na wamejaza mawe na magogo pande zote kuzuia magari.
Hawa binadam wabinafsi kuvuka mipaka
 
Last edited by a moderator:
Pwani ndo waanzilishi wa hayo mambo watu washazoea na ni kawaida ukiona hivyo angalia njia iliyonyeupe upite ila ingekuwa kila siku ingekuwa si vizur kwa kuwa kwa wik mala moja halafu kwa muda mfup haina shida pia ukuaji wa miji huenda hao wenye hizo shughuli toka muda mrefu wapo hilo eneo inabid wahamiaj mjipange.
 
Ibada zifanyike ila si kwa kufunga barabara, maeneo yapo mengi tu ya wazi, unakuta mtu umeingia kwenye hiyo barabara umbali mrefu mara unakuta maturubai tayari barabara ishafungwa inabidi ugeuze utafute njia nyingine
 
Siku moja nilikuwa naenda kwa jamaa yangu mwananyamala kwa kopa, naingia barabara kuelekea nakuta jamaa wamefunga turubai kukatiza barabara na wamejaza mawe na magogo pande zote kuzuia magari.
Hawa binadam wabinafsi kuvuka mipaka

kumbe kwa kopa ilifanyika siku moja bas shida haipo ila ingekuwa endelevu tungesema kuna tatizo
 
usitoe kauli usizokuwa unaupeo wa kutatua jambo zaid ya kutangaza chuk na ghiriba angalia pia ufinyu wa maeneo nani anapenda kufunga barabara? kwani hizo mambo mikoani zipo? kama zipo ni chache kutokana na eneo husika lilivyofinyu sasa kila mtu anawaza kwenda dar hayo maeneo ya shughuli yanapatikana wap?

Nimetoa mfano wa Mwananyamala kwa kopa ambapo nikiwa naelekea nikakuta turubai katikati ya barabara. Mita zisizozidi MIA pana uwanja kwa nini sherehe isifanywe uwanjani ?

Wameweka turubai na kuziba barabara wakati waliokaa kwenye mikeka ndani ya turubai watu watatu tu.
 
Nimetoa mfano wa Mwananyamala kwa kopa ambapo nikiwa naelekea nikakuta turubai katikati ya barabara. Mita zisizozidi MIA pana uwanja kwa nini sherehe isifanywe uwanjani?

Wamewaka turubai na kuziba barabara wakati waliokaa kwenye mikeka ndani ya turubai watu watatu tu.

Muda ulikuwa bado huenda ulipowakuta hao watatu kwani ulikesha nao? Na umejuaje kama hawakuongezeka? Vp na wachezaj kama wangetaka kucheza ktk huo uwanja? Pia hapo na ww hekima ikowapi kwa jambo uliliona siku moja umekuja kusemelea huku?
 
Nkwesa Makambo

Mkuu kuna siku nusura tupoteze mama na mtoto!mjamzito ameshikwa na uchungu wa ghafla!kufika njiani barabara imefungwa!!aargh!!mi sikubaliani na hili swala banah!!

Makanisa yalivyokuwa mengi nchini hapa wakisema watoke na wao wakasalie barabarani hali itakuwaje??tutapata hata sehemu ya kupita kweli??ni nini maana ya kujenga nyumba za ibada?

Mbona viwanja vya shule na mipira vipo jamani!?katika hili suala watu tumegawanyika!!
 
Last edited by a moderator:
Yaani watanzania kwa kushabikia dini walizoletewa hadi mnashangaza! Hats logic mnaweka pembeni. Sio ibada tu kuna watu wanafunga mtaa kumtoa mwali na upuuzi Kama huo!

Mnaleta usumbufu kwa wengine kisa mambo yenu binafsi si mfanyie uwani kwenu?!! Sijali muislamu au mkristo hizo ibada zenu msitufungie barabara fanyieni makanisani au misikitini kwenu sio kufunga mitaa.
 
Back
Top Bottom