Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,271
- 2,401
Kuna usemi mpya unasema “Heri walimkavu kuliko walimwengu.” Penye walimwengu pana pana mengi. Nasema hivi kwa nini. Kiuhalisia tuliletewa hii fursa na kijana mwenzetu ambaye naweza sema si mhangaikaji tu, bali anajua anachokihangaikia. Si mwingine ni Sirjeff, almaarufu kama Ontario. Sina sababu ya kurudia kile alichowahi kuandika kuhusu namna gani aliweza kuileta na kuitangaza forex hapa nchini.
Kabla sijaenda sana napenda kutangaza maslahi kuwa name ni mmojawapo wa wanufaika wa fursa hii ya forex. Tangu batch ya kwanza kabisa pale mwaka jana mwezi wa tisa hadi leo miezi sita naendelea na forex huku nikiendelea kujifunza mengi kila siku maana forex ni forest kweli. Baada tu ya ujio wa forex nchini ni mengi yamefanyika ikiwa ni pamoja na kusemwa, kuandikwa, na kutendwa.
Kwa kipindi chote hiki cha kuandikwa na kuzungumziwa kwa forex kwa mema na mabaya, nimewahi kuchangia tu mara chache. Aghalabu huwa nasoma kila kinachoandikwa. Walianza kuandika kuhusu forex kuwa ni utapeli. Ni DECI mpya. Ni pyramid scheme, na kwamba siku itafika watu wataficha nyuso zao na kwa kuwa yaliyosemwa yametimia. Haitokaa itokee. Bado wako watu wengi sana wanaamini kuwa forex ni kama ile michezo ya kubahatisha. Well, ukiamua kwenda kwa staili hiyo haujakatazwa. Wapo pia wanaoendelea kuamini kuwa forex ni DECI. Ni ponzi scheme. Well, wako wajanja wanaoitumia forex kuendesha hizo DECI. Hivyo forex ni kama kisu ulichonunulia kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Sasa akaja mtu akakitumia kumuumiza mwenzie haimaanishi kisu kibaya bali matumizi hayakuwa sahihi, hivyo aliefanya matumizi yasiyo sahihi ndiye mwenye matatizo.
Baada ya baadhi ya wale wadau wa mwanzo kupata elimu ya forex (basic knowledge) kupitia kampuni ya The Million Team (TMT) chini ya JP Markets ambaye ndiye broker tunayemtumia hadi sasa, kelele zilianza. Ukweli ni kuwa kila kitu kipya kina changamoto zake. Yawezekana malalamiko yao yalikuwa yana ukweli ila wakakosa staha na uvumilivu katika kuwasilisha na kuona wanachokitaka kinachelewa.
Yaani u introduce forex mwezi wa tisa, na baada ya miezi mitano kila kitu kiwe kama wateja wanavyotaka? Ni ngumu. Wako waliokuja humu jukwaani kukiri kuwa hakika forex ni mkombozi. Wanatengeneza pesa ambayo walikuwa hawajafikiri kutengeneza hapo awali. Kwamba forex sio imekuja wakati mwafaka, bali imechelewa sana. Forex haikuchelewa. Kutokana na ukwasi uliopo kwenye hii biashara, wako watu hapa nchini waliijua mapema na wakawa wanafanya yao kimya kimya bila kutaka wengi wajue haya. Wapo watu binafsi pamoja na taasisi za kifedha. Sasa kati ya hao ambao wameona maslahi yao yanaingiliwa na TMT basi rafu nazo zikaanza.
Sasa turudi kwa wale wafaidika wa forex ya TMT. Ni hulka ya binadamu kutaka zaidi ya kiasi, na kuwa mdadisi na kutaka kujiongeza. Sasa baada ya hawa wenzetu kuona kasi wanayoitaka na mambo wanayoyataka hayaji kwa kasi waliyojipangia, wakaanza kunena mabaya kuhusu TMT pamoja na broker husika.
Kiukweli mabaya mengi yameandikwa kuhusu TMT pamoja na JP Markets. Kwa mtu asiyependa kutafakari atasema basi tena, pale hamna kitu. Lakini sisi ambao bado tupo tunajua nini tunataka, nini tunapata, na tufanye nini panapotokea changamoto kadhaa. Matatizo yalianzia na broker, kisha TMT. Mbaya zaidi ikashuka hadi kwa CEO wa TMT – Ontario. Yote hii ikiwa ni harakati za kuvuruga na kuona jamaa wanakufa kibiashara na kupotea. Si rahisi hivyo. Nitaeleza kwa nini.
Broker
Suala la broker ni suala tete sana, watu hawajui tu. Wengi wa brokers tunaowatumia, nje ya huyu ambaye wawakilishi wake wapo hapa nchini, tunafanya nao miamala kwa ile tunaita mutual trust. Lolote laweza kutokea na hela yako ikapotelea huko nje. Kwenye forex kuna brokers wengi sana! Inatakiwa upembuzi wa kutosha kujua unafanya biashara yako na broker wa aina gani. Wengi wamepoteza hela zao huko nje bila kujua wanafanya biashara na broker wa aina gani. Wengi wa waliokuwa wanakuja hapa jukwaani kuiponda TMT, CEO wake, pamoja na JP Markets walikuwa/wanatoa mbadala wa brokers wao ambao kwa namna moja ama nyingine wana maslahi nao.
Hatukatai kuna ushindani. Waswahili wanasema usiache mbachao kwa msala upitao. Tena wakasema usitukane mamba ungali hujavuka mto. Singependa sana kuwazungumzia brokers hao ambao wamekuwa sababu ya huyu waliyekuwa naye mwanzo kunenewa mabaya. TMT walituletea JP Markets. Tunawajua TMT na ofisi zao tunazijua. Kwa tatizo lolote ofisi zao ziko wazi, hivyo hakuna namna yoyote unaweza kufanya miamala yako na broker akashindwa kukulipa halali yako wakati TMT tuko nao.
Tuko na JP kwa kuwa waliingia makubaliano na TMT, na kwa lolote wako tayari kushughulikia. Yako mambo kadhaa ambayo kati ya hayo ndiyo yalipelekea wadau kufitini na kuja huku na kuanza kumwaga ugali na mboga. Mambo waliyoona kwao ni kero sasa yapo ambayo yameshafanyiwa kazi, ikiwa ni pamoja na spreads kupunguzwa. Kama si mdau wa forex itakusumbua kujua baadhi ya masuala. Wapo ambao waliona urahisi wa kufanya miamala yao kwa njia ya mobile money kama mpesa, tigopesa na airtel money kupitia kwa hao broker wengine. Uzuri ni kuwa wakati sio mwingi huduma hiyo itaanza kufanya kazi kupitia JP Markets. Hata hivyo kwa sasa ukihitaji kuwithdraw cash yako toka JP Markets inakuchukua saa kadhaa tu.
TMT
The Million Team ambao ndio wanaoiwakilisha JP Markets uzuri tunawajua. Tunakutana nao na kuwasiliana nao wakati wowote. Wao kama kampuni wana wajibu wa kuhakikisha kuwa sie wateja wao tunapata kile tunachohitaji, ikiwa ni pamoja na urahisi wa huduma ya uwekaji na utoaji pesa toka kwa broker. Kingine kupata elimu ya forex na mafunzo endelevu hadi hapo mtu atakapoona anaweza kujisimamia.
Kama kuna tatizo limetokea, suluhu si kutoka na kwenda pembeni kutukana na kuleta ujuaji. Mtu mzima, tena mwanaume unakuja kupandisha uzi humu kuwasema watu wengine, kisa hujulikani, ni uzezeta tu. Mtu anakuvusha mto kwa kukubeba mgongoni unafika ng’ambo unasema, ‘limgongo lake linanuka…!’ Si watu hao. Zikitokea kasoro tunapeana ukweli humo humo kwenye grupu zetu na kwa uwazi na mwisho wa siku zile kasoro zinaondoka.
Yapo mengi tuliyowashauri TMT kama kampuni. Nao kwa uchanga wao wanaendelea kujifunza mengi. Nao siku na wakati ukifika kulingana na malengo yao wamepanga kuwa broker hapa nchini. Kama wamekuwa wa kwanza kutuletea elimu hii kwa uwazi, tuwatakie heri pia wafanikiwe kuwa broker wa forex hapa nchini ili hii huduma iwe rahisi zaidi nay a uhakika zaidi na karibu zaidi.
HITIMISHO
Forex ipo na itaendelea kuwepo. Kama hatuwezi nasi kuwa hao broker, sembuse kuleta elimu hii kwa wengi na kwa uwazi, tuwaunge TMT mkono katika kufanikisha haya. Tuone kuwa forex inakuwa sehemu ya ajira kwa vijana wengi ambao ajira imekuwa changamoto. La msingi ambalo TMT wakishirikiana na wadau wengine wanapaswa kufanya ni kutoa elimu sahihi kuhusu forex. Kwamba forex sio a get rich quick scheme. Kwamba forex sio bahati na sibu. Kwamba forex ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine. Forex inahitaji muda kujifunza kama zilivyo taaluma zingine.
Tumpe moyo kijana mwenzetu, mtanzania mwenzetu Sirjeff ambaye ameiona fursa ilipo akaona sio vibaya kuwapa na wengine fursa hii. Tukiweka nidhamu katika kuifanya forex kulingana na misingi na taratibu zetu, basi lengo na kusudi la mwenzetu huyu litatimia – kuwezesha wengi kujiajiri. Lakini tukianza pupa na kutaka kutajirika na kuwa na ulafi na mwisho kujenga chuki na kuchafuana, forex itaonekana ni blah blah (kitu ambacho si sahihi kabisa) na mwisho lengo la mleta fursa halitatimia.
Tena wahenga wakaendelea, usidharau nazi. Embe tunda la msimu. Uzuri itafika siku na wale wote waliokuwa na nia mbaya na hawa jamaa (TMT) watarudi kuwa sehemu ya TMT. Wako watakaorudi kimya kimya na wako watakaokiri hawakuwa sahihi kutupa jongoo na mti wake. Hivyo basi natoa wito kwa wale ambao kwa namna moja au nyingine walikatishwa tamaa na hoja nyingi mfu zilizoletwa humu jukwaani waone tena sababu ya kujitafakati tena na kuichangamkia fursa hii. Kwa wale ambao hawaijui TMT na mahali ilipo, ni Oyaterbay karibu na kituo cha mbuyuni barabara ya Ali Hassani Mwinyi. Jingo linaitwa Jangid Plaza.