Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,348
- 5,978
Usiingilie mamlaka ya Allah ktk kutoa hukumu..
Tunaambiwa kwamba Dua ya aliyedhurumiwa huwa apigi kona,ukiomba inanyooka moja kwa moja mpaka kwa Allah.
Hutakiwi kumuombea mabaya,but mshitakie kwa muumba kwamba amekudhulumu haki yako na yeye Allah atakurejeshea kwa njia nyingine,kisha huyo mdhulumaji wako msubiri siku ya kiyama ili akusaidie mzigo utakakua nao kichwani maana siku hiyo hatokua na pesa ya kukulipa.
Nakupa mfano1..wakati naanza maisha nilikua nikiuza maji kwenye mkokoteni,sikua na acc bank so kuna kakangu nikawa nampa anitunzie maana nilikua nakaa kwake huku nikifanya na kazi za nyumbani kwake za kuhudumia mifugo na kuwapeleka watoto shule,baada ya miaka miwili nikawa nimepata 780,000/= na my bro akakili yes ndiyo pesa aliyonayo na yupo tayari kunipa hiyo pesa,nikamwambia poa ngoja niende mjini kuangalia bei ya mahitaji yangu ili ukinipa pesa nikanunue nirudi kwa wazazi.Nikaenda mjini kuulizia jembe la kukokotwa na ng'ombe lilikua 75,000/=,baiskel mpya 70,000/=,Godoro kubwa dodoma 28,000/=,na bahadhi ya mahitaji mengine ikiwamo vitenge na nguo za mzee na wadogo zangu.Ilikuja kama 300,000/= for shopping.Then nyingine ningeenda kununua ng'ombe home ili nianze maisha ya kujitegemea.
Niliporudi nikamwambie nipe kesho asbh hiyo pesa ili nifanye manunuzi yangu......sikuamini aliposema tupige mahesabu nilikua nakula bei gani kwa siku ili anikate kabisa then change itakayobaki ndio haki yangu,baada ya mahesabu kupigwa nikakuta nadaiwa 30,000/= na kaka yangu huyo wa mama mkubwa...nikamwambia basi nikopeshe elfu10 ili nitumie kurudi nyumbani nikifika home ntapiga vibarua ntamtumia pesa yake..jamaa akakataa..ikanibidi nikae tena mwaka mzima bila kazi...lakini nikakumbuka kuna mungu,mungu ambaye hajui kumuonea mtu..nikamlilia mungu..haikupita wiki1 moja nikapata kibarua cha ulinzi ambacho ndicho kilichonipelekea leo hii mimi Wonderful mambo yangu yakawa supa na kupitia mlango huo huo wa kazi za ulinzi niliweza kujikuta siku moja nikiwa Europe huku familia yangu ikiishi vzr home.Now days yule aliyenidhulumu ni masikini na biashara zote zilikufa,magari yakafa and now days anafanya vibarua huko maeneo ya Dodoma na elimu yake ya fm6..mie wa darasa la7 nakula good life.
Wasalaam!