Ni dhahiri Tanesco wanaelekea kufilisika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni dhahiri Tanesco wanaelekea kufilisika!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ibrah, Sep 22, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mdau mmoja hivi karibuni alilalamika kuwa TAnesco Ilala hawajamuunganisjhaia umeme na siku 90 zimeshapita tangu alipie huduma hiyo ati hawana waya. Nimebaisni kuwa tatizo hilo haliko Dar es salaam pekee bali mikoa ya Arusha, Iringa, na Ruvuma. Tanesco Iringa mwezi wa nane walipewa nyaya hizo na Tanesco Ruvuma ambao nao sasa wameishiwa.

  Kwa sasa Tanesco hawapokei tena pesa kutoka kwa Wateja kwa madai kuwa hawana nyaya hadi hapo watakapopata nyaya tena. Tutafakari hili; Tanesco ni moja na kama Mkoa wa Iringa umeishiwa vifaa unaweza kupata kutoka TAwi la Ruvuma, vivyo Arusha wanaweza kupewa kutoka Kilimanjaro au Manyara, na Tanesco Dar wanaweza kupewa na Tanesco Pwani au Morogoro.

  Kama mikoa ya Arusha, Ruvuma, Dar na Iringa hawana nyaya hizo basi ni wazi kuwa mikoa yote ya jirani na mikoa hiyo hawana nyaya hizo. Sasa unaenda mwezi wa kumi bado Tanesco hawajaanza kupokea malipo ya kuunganisha umeme hadi watakapotujulisha! Nijuavyo mimi shirka kama TAnesco halinunui vifaa kwa pesa taslimu bali mgavi huleta bidhaa na baada ya muda Shirika linalipa, hii inatoa p[icha kuwa Tanesco imezidiwa na madeni kiasi cha Wagavi kusitisha huduma kwa TAnesco na kwa bahati ni kuwa vifaa hivyo Tanesco hununua kwa niaba ya sisi Wateja ambao huwalipa Tanesco na Tanesco kuvinunua kwa niaba yetu.

  Hii ni ishara dhihiri kuwa Tanesco imezidiwa na madeni ambayo imeshindwa kuyalipa. Sasa hiyo maana yake nini? Inadhrisha kuwa ama kuna unadhirifu mkubwa ndani ya Tanesco au Shirka linajiendesha kwa hasara kwa mantiki ya kwamba pesa tunazolipia Tanesco kuunganishiwa umeme si halisi bali ni chini ya bei halisi -maana yake Tanesco inapokea ruzuku kutoka Serikalini ili kufidia gharama hali za ununuzi wa nyaya za kuunganishia umeme. Maana yake ni kuwa kwa sasa Serikali imesimamisha ruzuku hiyo ama kutokana na uchaguzi (ambao umekuja ghafula sana na serikali ilikuwa haijui ama haijajiandaa kwa gharama za uchaguzi) au kuna matumizi makubwa sana mengineyo kwa upande wa Serikali kiasi kwamba imeshindwa kupata pesa za kuwaruzuku Wateja wa Tanesco yaani sisi Wananchi.

  Kwa mtindo huu ni wazi Tanesco inahitaji wokovu, vinginevyo Wateja tulipie gharama halsi za kuunganishiwa umeme, kitu ambacho Serikali kupitia EWURA inachelea kuruhusu ongezeko hilo kwa sababu za kisiasa hadi uchaguzi upite na Tanescio wameshaomba EWURA kuongeza kupandiha gharama za umeme tangu miezi miwili ilopita lakini uamauzi haujatolewa bado (hadi baada ya uchaguzi). Watanzania tutadanganyika hadi lini? Maana ni dhahiri si EWURA wala Serikali zinaweza kuzuia ongezeko la gharama za kuunganisha umeme maana mbomoko wa shilingi ni mkubwa mno na Serikali imeshindwa kuuzuia mbomoko huo na hivyo Tanesco ambao huagiza vifaa toka nje (kwa fedha za kigeni) hawawezi kuepuka athari zake.

  Tujianda kulipia zaid umeme mara baada ya uchaguzi vinginevyo kura zetu ziwakatae Watawala hawa wa sasa. Tusema hatukubali na hatudanganyiki!

  MTU ANAYEKUBALI KUDANGANYWA, HANA MAONO JUU YA MAISHA YAKE MWENYE
   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Chagua Dr. uepukane na dhahama hizi zisizo na maana.
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nawajua Madakta watatu- Dk Kikwete, Dkt Slaa, na Prof Lipumba. Unamaanisha yupi?
   
 4. T

  Teko JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2010
  Joined: Jul 3, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Dk Slaa!
   
 5. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Shusheni fanancial statement ya Tanesco, wadau nadhani wanaweza kutoka sadaka ya ushauri. Sidhani kama na wao wapenda hali iliyopo. Just think about it, if Tanesco are having an operatioal issues in Dar, how about deep interior and over the montains and canyons of Tanzania. It's ok guys, ain't nothing to be ashemed. I think that's a reason for us to be in the JF.
   
Loading...