Ni CCM Gani Hasa Ilioleta Rekodi Mpy ya Kuchakachua Uchaguzi Mkuu 2010???

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,191
Wan-JF, malalamiko yako kila kona ya nchi yetu kuhusu uchakachuaji wa uchaguzi kwa njia ya aibu sana usoni mwa ulimwengu, laki mchakachuaji bado, ambaye mpaka sasa anadaiwa kuwa ni CCM, hatujaweza kumchambua vilivyo, jinsi gani alivyofanya, na kwa kuegemea udhaifu upi hasa.

Kuna rafiki yangu alikua akinifahamisha kwamba kuna CCM nyingi sana siku hizi. Kwa kutofautisha akataja aina mbalimbali za CCM kama ifuatavyo:

1. CCM Nyerere (Uadilifu / Masikini)

Akasema kwamba hii CCM ni ile yenye rangi ya Kijani ya mgomba na kwamba Timu yake inaundwa na Wachezaji Maarufu kama vile

(1) Namba Tisa Joseph Sinde Warioba, Namba Kumi Salim Ahmed Salim, Job Lusinde, Mzee Butiku, Mama Maria Nyerere, Mama Karume, Mzindakaya, Mzee Kisumo, Prof Shivji, Prof Mwandosya, Dr Mwakyembe, Ole Sendeka, Mzee Malecela, Mnauye Junior, Hussein Bashe, Ben Mkapa, Mwakalebela, Sitta, Getrude Mongela, Magufuli, Pinda, Prof Luhanga, Joseph Rwegasira, Mjeshi Shirima, Kilango, Mzee Bomani, Prof Sarungi, na wengine wa aina yao ... then akazungumzia;

2. CCM Academia (Wachacharikaji / Mamilionea)

Wakiongozwa namba tisa wao Mhe Rostam Aziz, Namba Kumi Edwardi Lowassa, Ridhiwani Kikwete, January Makamba, Lau Masha, Mhe Diallo Anthony, Mshambuliaji Machachari Makamba, Mchezaji wa Kuvizia Kpt Chiligati, John Komba, Mzee Mwinyi, Gachuma, Lameck Airo, Prof Mukandala, Dr Benson Bana, Owino Maina, Pesambili Mramba, na wengine kama wao .... tena akaongeza ya kwamba kuna;

3. CCM Liberals (Yatima / Vuguvugu)

Prof Magembe, Dr Kigoda, Mornica Mbega, Komanya, Banduka, Ole Njolay, Lukuvi, Dr Mwinyi, Aisha Kigoda, Lewis Makame, Odunga, Mudhihir, Hawa Ngulume, Felix Mosha, Kamara, Mwapachu, Ndolanga, Mengi, Nagu, Kimiti, Kileo, na wengine wengi

Sasa, je kati ya CCM hizo hapo juu nanyinginezo ambazo huenda bado hatuzifahamu, ni CCM ipi hasa ambayo huenda wanahusika na kilio cha taifa kuporwa haki ya kujichagulia viongozi wa kuwawakilisha kidemokrasia??

Je, ni haki kuwalaumu wana-CCM wote kwa kosa la kikundi kimojawapo tu ndani mle??

Je, CCM ikifa leo au kesho ni kundi gani hapo juu ambayo ndio wa kulaumiwa??
 
Unawezaje kumweka BWM na kina Warioba- CCM UADILIFU? Au Magufuli na Nyerere, unasahau alivyojipendelea na kupeleka lami kwake ambayo ilibidi kuifikia upite kwenye mashimo ya ajabu? L Makame kama Liberal, acha utani, huyu ni CCM WACHACHARIAJI!
 
hii topic ilitakiwa kuwa hapa kweli?
hii ni sehemu ya utambulisho muheshimiwa....
 
Back
Top Bottom