Ni busara kukubali urafiki wa fb toka kwa mtarajiwa?

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Nimepata friend request ya mtarajiwa nimeshindwa kuijibu, nataka nichote ushauri kwanza.

Binafsi najijua sina break kwenye kupost issue na comments kwenye post na mipicha sasa najiuliza akikwazika na michango yangu humo fb nahisi itakuwa mwanzo wa chokochoko.Mwenye uzoefu atoe ushauri kama huna pita mbele.

NB. Kipindi cha nyuma niliwahi kuwa na mdada mwingine hatukuwa na malengo ya maisha ya baadae alikuwa rafiki yangu fb nilikuwa naona joto la uwepo wake alikuwa ana pay attention to details mpaka kero.

Binafsi napenda uhuru wangu wa kujieleza na kujichanganya.

Karibu.
 
Mkuu nakumbuka siku nilipoiacha account yangu FB ni siku nilipoona friend request toka kwa wife....Si tu sikurespond ila na hiyo account hadi password yake nimeshaisahau...Nilikuwa na sababu 2 tu..Kwanza sikuhitaji sana kujua kwenye ulimwengu huo yeye huwa ana-behave vp 2.Sikutaka na yeye ajue ulimwengu wangu huko huwa nabehave vp...Kuna comment zingine unaandikiwa na classmate wa kike kimasihara tu ila nyumbani hapataka lika siku hiyo....
 
Back
Top Bottom