Cha kushangaza wanaoponda kununua gari wao ndio wa kwanza kuwasumbua wenye magari kwa kuomba lift,ndio wa kwanza kukusubiri getini mda wa kutoka,ukichelewa kidogo kashapiga simu vp leo bado umalizia kazi? Huyo huyo anayesema bora ujenge nyumba,hiyo nyumba yenyewe kaijenga nje ya mji mapinga,mwasonga,gezaulole au chanika,kazi anafanya posta,k/koo au mwenge na hiyo nyumba si nyumba bali ni pagale,nahita pagale kwa sababu haina hata ceilin board,haina hata plasta,dirishani umeweka nyavu,kwakua nyumba ipo mbali hawezi kukaa huko itambidi apange,sasa una pagale halafu umepanga si bora mie nilieamua kununua mkoko kusave mda maana naamka saa kumi na mbili unusu mpaka saa moja natoka kazini ndani ya dkk 45 nishafika kimbembe wewe lazima kwanza uamke saa kumi na moja kuwahi lifti au kurusha mkuki(kupanda dala dala).