Ni biashara ipi ndogo sana uliifanya ikakufikisha kwenye mafanikio makubwa?

Kuna biashara uchwara nimeifugua Zanzibar mtaji laki 2 na nusu, lakini hadi sasa Nimetengeneza zaidi ya milion tatu kwa siku kadhaa tu na kila siku nalaza faida ya laki Kama net profit.

Hela hata sipeleki benki natunza chini ya kapeti tu. Leo ndo napeleka benki milion 2.

I'm happy


 
Hii idea nilikuwa nayo jana tu hapa. Nilitaka kuweka laki 6 kwenye kakibanda ka chips baada ya kufatilia nikaona miyeyusho kwanza vibanda vingi na chips zina usumbufu. Nikafikiri nikiweka pungufu ya hiyo kwenye kibanda cha mamantilie si napata hela ingawa siwezi kamwe kufanya hiyo kazi mpaka niweke wadada.

Bado niko dilemma.
 
Biashara yoyote ile nisiyo na ufahamu nayo kimtindo na isio na usimamizi wangu siwezi kuifanya kamwe.
 
Uzi unakuomba utaje jina la biashara. Au unaogopa copyright issues
 
Biashara yoyote ile nisiyo na ufahamu nayo kimtindo na isio na usimamizi wangu siwezi kuifanya kamwe.
Niko chuo sina muda mwingi wa kukaa mtaani. Kila biashara ninayofikiria inataka muda wangu mwingi. Nina options mbili, either nimuamini mtu nimkabidhi biashara badala yangu, au nisimamie kazi ila operations zote ziwe mikononi mwa anayefanya kazi.

Nishapoteza hela nyingi kula bata kwa sababu ya kufeli katika uchaguzi wa options hizi nikapata hasara na kukata tamaa ya kuwekeza.
 
Sasa hivi unaenda kubadilisha tu namna hela yako inavyoenda kupoteza badala ya kuipoteza kwenye bata unaenda kuipoteza kwny kupeleka pesa kwny kitu usicho na usimamizi nacho.
 
Hv ujasiri wa kuwekaga wadada mnaupata wapi? Au la awe my wife wako...ww unakaz zingine?..hizi mishe piga mwenyewe saidiana na wenzako muwe 3..kwisha habari..yaan msichana awe wa kuosha vyombo na kupika greens
 
Chakula cha hvo kinakuaga very tastey
 
Kumbe milioni 3 ni mtaji mdogo? biashara kama ya kuuza mihogo, viazi kwa mafungu haizidi laki 2 au hata kuku wa kienyeji haizidi laki tano, wewe unaleta biashara za mamilion.
 
Sasa hivi unaenda kubadilisha tu namna hela yako inavyoenda kupoteza badala ya kuipoteza kwny bata unaenda kuipoteza kwny kupeleka pesa kwny kiti usicho na usimamizi nacho.
Basi bora nile maisha na manzi yangu as long as nakusanya elimu ya mazingira nikiwa free nitafanya. Sio kuwa ndio naenda kupoteza, nishapoteza 1.2M kwa kutosimamia. Niliambulia kuokoa laki 5 kasoro

Kwa kiasi flani nimeibukia kwenye savings, tatizo hela nayoweka ni ndogo naona bora niiwekeze ikue ila ndio vitasa napokea. Nikisema nisikate tamaa nazidi kupoteza hela
 
Biashara yangu ina copyright issues hivyo samahani jamani sitaitaja maana naifanya mwenyewe tu huku Zanzibar watu wengine bado hawajapata mechanism ya kucopy.

Na soon baada ya wao kucopy nahamia kwenye phase 2.

Mtanisamehe!
Najaribu kuitafakari iyo biashara akili inagoma kabisa. Kibaya zaid sijapata biashara nzuri ya mtaji mdogo niifanye toka mwaka uanze,eeh Mungu nisaidie !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hv ujasiri wa kuwekaga wadada mnaupata wapi? Au la awe my wife wako...ww unakaz zingine?..hizi mishe piga mwenyewe saidiana na wenzako muwe 3..kwisha habari..yaan msichana awe wa kuosha vyombo na kupika greens
Kuoa mimi sio leo wala kesho. Ndo kwanza niko chuo nina ghetto hasahasa namiliki jeans na raba hakuna kingine. Muda wa kufanya kazi sitopata, kusimamia sawa ila sio kukaa.
Hapa yenyewe nina UE jioni niko nazima moto
 

Attachments

  • IMG20210311112410.jpg
    76.4 KB · Views: 105
Usimamizi ni kila kitu mkuu, hakuna mtu anae enda kukutengenezea pesa huku wewe ukiwa kwny mishe zako nyingine mzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…