Ni akili kubwa kwa mwanaume kutokuoa mapema

Ni akili kubwa kwa mwanaume kutokuoa mapema

Mimi huwa najiuliza hivi wanaume kinachowafanya waogope kuingia kwenye ndoa ni nini? After all wao ndiyo watawala na ndiyo vichwa vya familia, wana maamuzi ya mwisho na hakuna wa kuwapangia cha kufanya, wana uhuru wa kutosha, na wanaweza kufanya chochote wanachojisikia kwenye ndoa, tofauti na wanawake ambao kwao ni kinyume chake!

Mimi nilidhani wanawake ndiyo wanatakiwa waogope kuingia kwenye ndoa na siyo wanaume. Lakini nashangaa eti wanaume ndiyo wanaoongoza kwa kulalamika kuhusu ndoa.

Mara nyingi, hakuna faida anayopata mwanaume pindi akioa, ila mara nyingi nyie wanawake mkiolewa ndo mnafaidika ndo maana nyie wadada mnakomaa muolewe Zoë
 
Wewe na wadada wengine wa jf mtamponda mtoa Mada kwasababu mnajua ndoa inawafaidisha nyie wanawake kwa kiasi kikubwa sana, ilhali mwanaume atafaidika kwa kiasi kidogo mno na ndoa mama D
Hicho unachosema wanawake wanafaidi toka kwa wanaume ni haki yao na ni wajibu wa mwanaume kukifanya.
Hakuna mto unaoanzia baharini ukayabeba maji ya bahari kuyapeleka nchi kavu, asili yetu na imani zetu zinaweza kupindishwa lakini matokeo yake ndio hayo wanaume kuogopa wanawake😂😂😂😂
 
Mimi nakushauri ukitaka kuoa akikisha kwanza una kazi ya kukuingizia kipato cha kila siku kwa uhakika ukioa bila hivyo lazima umuone huyo mwanamke kama shida kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa mkuu tena ni vizuri kutafakari uwezo wa familia ya huyo dada mfano baba na mama yake km wanafanya kazi, uwezo wa ndugu zake km kaka na dada na pia wako wangapi. Kisha angalia uwezo wa huyo dada mwenyewe km ana kazi au buz ya kumuingizia kipato. Kisha tazama kipato chako na gharama kadhaa za maisha km kodi ya nyumba, matumizi ya mwezi pamoja na mipango yako ya maisha like unataka kupata nn kwny maisha. Kisha jitafakari wewe mwenyewe je family yako inakutegemea kwa kiwango gani. Baada ya hapo utapata jibu km uendelee na wazo la kuoa kwa haraka au usubiri. There is another day always.
 
Mimi huwa najiuliza hivi wanaume kinachowafanya waogope kuingia kwenye ndoa ni nini? After all wao ndiyo watawala na ndiyo vichwa vya familia, wana maamuzi ya mwisho na hakuna wa kuwapangia cha kufanya, wana uhuru wa kutosha, na wanaweza kufanya chochote wanachojisikia kwenye ndoa, tofauti na wanawake ambao kwao ni kinyume chake!

Mimi nilidhani wanawake ndiyo wanatakiwa waogope kuingia kwenye ndoa na siyo wanaume. Lakini nashangaa eti wanaume ndiyo wanaoongoza kwa kulalamika kuhusu ndoa.

Tehtehtehteh.... Zoë kuna mwanamke wa kumfanya hivyo ulivyoandika mdogo wangu?

Hata la saba uliyemtoa kijijini atakudindishia usimjue kama ni yule.
 
Mimi nakushauri ukitaka kuoa akikisha kwanza una kazi ya kukuingizia kipato cha kila siku kwa uhakika ukioa bila hivyo lazima umuone huyo mwanamke kama shida kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
Unachosema ni ukweli kabisa ukiwa kijana uelewe kabisa mwanamke unaetaka kumuoa yeye anaangalia ni kwa namna gani wewe utaweza kuendesha maisha yake yaani future so akiona ipo lazima akukomalie umuoe. Hapo kijana itakupasa ujitafakari je unao uwezo wa kudili na matumizi ya huyo mwanamke kwa ujumla kwa wakati huo na near future? ukiona huwezi kausha tu usijiingize huko as utafanya maendeleo yako yachelewe sana na pia kuleta mtafaruku kwny hiyo ndoa. Hivyo ni vizuri kutokuwahi kukimbilia kuoa hadi pale kijana utakapokua na uwezo sawa sawa.
 
Hili suala la kukurupukia kuoa silitofautishi sana na hili la dada zetu kubeba ujauzito.....unazaa,unaoa/kuolewa kwa sababu tu kuna mtu kazaa,kaoa au kaolewa.,wazazi wazazi,ndugu,jamaa au rafiki wanataka mtoto,wanataka uoe au kuolewa...si sahihi hii maana mwisho wa yote huwa ni majuto...hivi vitu vinahitaji utayari wa mhusika/wahusika wenyewe.

Nb; Watoto wengi siku hizi wanatelekezwa kwa sababu hizi,ndoa nyingi hazidumu na baadhi zinadumu ila kwa nusura za vikao vya familia maana migogoro ni mingi mno kwa sababu vijana wengi hufanya haya mambo kwa kufuata mkumbo...ndoa ni zaidi ya taasisi ukiingia kichwa kichwa unakula za uso
 
Back
Top Bottom