Wana JF,naomba kujua kutokana na uzoefu wako binafsi aina ya simu ambayo itakuwa ni ya kasi sana na ina uwezo wa kuangalia Youtube,download n.k. bila shida.Pia yenye uwezo ambayo unaweza ukaandika documents mbalimbali na kuziprint moja kwa moja kwenye printer.Yaani kwa ufupi ambayo unaweza ukafanya kazi nyingi bila kuhitajika kutumia Computer.Pia kwa anayejua gharama zake kwa makadirio.Napenda kutumia vitu ambavyo ni "Genuine",hivi fake vina usumbufu sana!.Asante kwa ushirikiano mwema na uwe na siku njema yenye baraka tele za Mungu aliye hai.Nawasilisha.