Ni aibu kwa Serikali kwa Mashirika ya Umma karibu yote kupata hasara

Tunachoweza ni kuongea mpira, ngono, muziki na kubishana siasa. Other than that kuna kipi hasa tunaweza kama taifa?
Naungo mkono hoja

Yaan tanzania hakuna tunachokijua zaid ya kununua magor kwenye mipira

Nje ya hapo ni upuuzi mtupu hii nchi inapoelekea itakuwa kama alivyosema job ndugai

State failure
 
Mimi nadhani mashirika ya umma yangeweza kuendeshwa na makampuni binafsi.
 
TTCL walipaswa kuwa mbele ya muda na wangekuwa mbali sana hasa kwenye hudum ya Internet kiukweli kwasasa Internet sio anasa tena bali huduma ya muhimu kama sio lazima wangejikita kuboresha huduma zao kila mtu angependa kuunganishwa nao.

Tatizo linaanza mpka wakupatie huduma hiyo lazima usote zaidi ya miezi 6 sasa zama hizi usumbulie hivyo wakati kuna kampuni unalipia leo unalterable huduma siku hiyo hiyo nashindwa kuelewa utashi wa watumishi wa TTCL uko wapi yani kama wanakupa huduma bure wakati unalipia ajabu sana, niliomba kuunganishiwa na home Internet leo yapata mwezi wa 8 unaenda hata survey hawajafanya halafu wanalalamika hasara wakati wateja wapo lukuki mtaani.
 
waniuzie mm kwa bei ya punguzo kuliko mahasara yote hayo, bilioni...bilioni...bilioni, ndo nn sasa hyo
 
Just imagine yaani TTCL kutoka Kupata faida Hadi Kuzalisha Hasara yet bodi zipo na CEO yupo harafu Serikali Inatumika Kodi za Maskini kwenda kuwalipa mishahar...
Yaani mashirika yanashindana kutengeneza hasara. Nashauri ianzishwe tuzo ya mashirika yenye kuleta hasara ili mwaka kesho Rais atoe tuzo hizo kuanzia hasara kubwa hadi ndogo! AIBU YAO...!!
Akikabidhi ripoti iliyokaguliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, siku ya Alhamisi asubuhi, CAG Charles Kichere alisema ofisi yake inaelewa juhudi za serikali za kuboresha utendaji wa taasisi zake zinazopata faida lakini alisisitiza kuwa dhana ya utawala bora inapaswa kufuatwa...
 
Umeongea point 100% maana nilitaka kusema haya ndio nikapitia comment yako. Swali la kujiuliza hasara inatokea wapi mfano watuambia ATCL hasara kwa maana...
Wakuchukua hatua nan hapo mkuu wakati utamaduni wa hii nchi unaujua

Hii nchi kila aliyekuwa kwenye system ni mwizi, sasa unawezaje kumuwajibisha mwenzio wakati wewe mwenyewe ni mwizi?

Kuna mdau 1 alisema dawa ni katiba mpya tu, kuwe na kifungu ambacho kinasema mtu akiiba tu anyongwe

Huenda hapo watu wangeheshimu mali za umma
 
TTCL walipaswa kuwa mbele ya muda na wangekuwa mbali sana hasa kwenye hudum ya Internet kiukweli kwasasa Internet sio anasa tena bali huduma ya muhimu kama...
Sio ttcl tu mkuu, tatizo la ofis nyingi za umma sio wawajibikaji kabisa

Unaweza ukaenda kwenye ofis ya umma kuhitaji huduma unakuta wanakuangalia tu hata hawawajibik sasa unadhin hapo nchi itapataje faida?

Wao wamekaa kuangalia tu ifike tar 22 , au 23 waangalie kwenye acc zao kamzigo kamaingia

Na ndio maana miaka yote taasisi binafsi ndio zinapata faid sababu ili ulipwe inatakowa ufanyekazi kwel

Hii nchi kuendelea ni issue kwakwel ila all in all wakuwalaum ni hao hao viongoz vilaza tunaowachagua
 
Rais anahitaji vijana wachanga wenye uwezo na uthubutu wa juu kuyavusha mashirika ya Umma.
Tunahitaji katiba yenye kuweza kumuwajibisha rais endapo itabainika kashindwa kudhibiti na kuwasimamia watu wake wa chini kama vijana walikuwepo enzi za magufuli walicho fabya ninini kama sio kuemdekeza uzinzi na ubakaji na unyang'anyi,rais akijua kuna kuwajibishwa na yeye atawawajibisha walio chini yake ili yasije kumkuta ,lakini kwa hii katiba inayo mtakasa raisi hata kama mchafu tutaendelea kulalama tu kila mwaka
 
Wakuchukua hatua nan hapo mkuu wakati utamaduni wa hii nchi unaujua

Hii nchi kila aliyekuwa kwenye system ni mwizi, sasa unawezaje kumuwajibisha mwenzio wakati wewe mwenyewe ni mwizi?

Kuna mdau 1 alisema dawa ni katiba mpya tu, kuwe na kifungu ambacho kinasema mtu akiiba tu anyongwe

Huenda hapo watu wangeheshimu mali za umma
Nakuunga mkono lakini suala la katiba mpya halina uhusiano na haya madudu. Hii katiba iliyopo tu na uhakika hairuhusu haya madudu na sheria kali zipo tu. Tatizo tunataka katiba mpya hii ya zamani tu hatuijui, tunataka kujifariji kuwa shida sio sisi ni katiba mpya.

Hapana shida ni sisi uadilifu zero, wafanyakazi tu kwenye mashirika binafsi au kwa watu binafsi wakipata fursa tu wanaiba sasa hawa nao tuunde katiba?

Tanzania shida yetu kubwa tunaaminishwa kuiba ndio ujanja mtu anajenga nyumba la kifahari, gari za kifahari huyu ni mtumishi tu lakini sisi tuko busy kumsifu tu huyu ndio mwanamme sio yule yuko sehemu nzuri hata nyumba tu hana, hapo unategemea nini.

Dawa ni kama akithibitishwa kuiba ni mali zake zote kutaifishwa mpaka pesa aliyoiba irudi abaki zero mitaani hii ni adhabu tosha kuliko hata kumnyonga.
 
Sasa mawaziri hapo na wakuu wa hizo idara utawasikia kesho eti wanatoa maelekezo.
Yani wasipowajibika basi wawajibishwe. Au CAG aachetu kupata tabu maana nae anaongeza garama zaidi ambayo haina mrejesho chanya
 
Hawa hawa wanaoifisadi nchi ndiyo 2025 wataiba kura na kurudi tena kuendelea kuifisadi nchi. Hivi hatuna wanajeshi wenye kujielewa wakachukua nchi na kuvifuta vyama vyote vya siasa kwa miaka mitano,ikifika mwaka wa tano ndiyo viandikishwe vyama upya chini ya usimamizi wa jeshi ndiyo waitishe uchaguzi ambao utakuwa huru na haki ili tupate serikali halali.

Kwa CCM hii huu upuuzi hautakaa uishe na kwa jinsi walivyowekeza kwenye wizi wa kura unaoratibiwa na tiss na polisi ni vigumu chama kingine kuingia madarakani. Solution ni Jeshi tu.
 
Hasara ya ATCL wanajitakia wenyewe, huwezi kuwa na ndege 14 ukaajiri marubani 124.

Huwezi kuwa shirika la ndege unakatidha safari kisa tu Waziri kachelewa au Ndege imeenda kumpeleka Rais Zanzibar.

Hilo shirika linalelewa ndo maana haliwezi pata faida, likiachwa lijitegemee kama Vodacom huwezi sikia hasara kamwe.
Mbona NMB wanafanya vizuri,kwanini serikali isiangalie uwekezaji wa namna ile au kama haiwezi bora iachana na hiyo biashara kichaa
Aisee , Marubani 124, kweli 124?
Du ngoja ninyamaze tu,
Kwa hiyo rubani akiirusha mruko mmoja tu leo alhamisi, anasubiri au anapumzika wiki nzima ndio anakuja kurudha tena,
Au wanalipwa kwa masaa kurusha, kama ni malipo ya mshara basi hapo faida wasahau.
 
Back
Top Bottom