Ni aibu: Kituo cha Taifa cha Radio

leipzig

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
2,766
1,707
Ni aibu na fedheha kubwa kuona mashimo na madimbwi mfano wa bwawa mbele ya kituo TBC Radio pale Pugu Rd.

Yaani unapolikaribia geti inabidi utafute namna ya kuvuka hayo mabwawa yenye maji machafu yanayonuka kiasi kwamba unajiuliza wenye ofisi hiyo wanayaona?je harufu mbaya haiwakeri?halafu ndio wanatoa elimu ya kukabiliana na mbu waenezao malaria.

Jamani ni aibu kusubiri kila kitu Rais aingilie kati wakati tuna wasomi wenye PHD,ni aibu.
 
Back
Top Bottom