FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 37,890
- 43,782
Kituo cha Mawasiliano kilichochukua nafasi ya kituo cha ubungo ni moja ya vituo bora kabisa vya daladala afrika mashariki na kati. Lakini cha kushangaza na kutia aibu ni kwamba barabara inayoiunganisha barabara ya Sam Nujoma na kituo hicho iko katika hali mbaya ya mashimo mashimo kama mahandaki, ina vumbi kama kiwanda cha cement na wakati wa mvua ni mabwawa na matope kwa kwenda mbele. Urefu wa hii barabara ukiunganisha na kile kipande kinachoenda hadi Sinza ni chini ya 1km. Sasa je, ni nini hasa kinachosababisha miaka yote hii kipande hiki kisiwekwe lami..?!
=======================================
UPDATE: (20/03/2017) Baada ya kuleta malalamiko hapa jf takriban wiki moja iliyopita, leo mkuu wa mkoa wa Dar mh.Paul Makonda, katika sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa ubungo flyover, amesema bajeti kwa ajili ya barabara ya kituo cha mawasiliano imeshatengwa na ujenzi utaanza muda wowote kuanzia sasa. Kweli jf inamkono mrefu.