NHIF sometimes inalipia huduma hewa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NHIF sometimes inalipia huduma hewa!

Discussion in 'JF Doctor' started by Amakulu, Jan 20, 2012.

 1. A

  Amakulu New Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF, utaratibu wa kupata huduma ya afya kwa wenye bima ya NHIF, sijui bima zingine inakuwaje, huwa huduma na dawa zote ulizopewa katika hospitali fulani zianandikwa na doctor kwenye fomu ya NHIF alafu wewe mgonjwa au ndugu anasaini kuonyesha kuwa kweli ulipewa huduma hizo na fomu hizo baadae hupelekwa NHIF ili walipie huduma uliyopata. Imenitokea mara kadhaa nikieenda hospital hasa za private na doctor anaprescribe dawa mbili au tatu lakini nikienda pharmacy kuchukua dawa pharmacist ananipa dawa pungufu na kuniambia kuwa dawa fulani niliyoandikiwa imeisha lakini wakati huo tayari nimesaini fomu ya bima na kusaini inamaanisha kuwa huduma na dawa zote zilizoorodheshwa kwenye fomu ile nimepewa! NHIF wakipelekewa fomu ile wanalipia hata dawa ile niliyoambiwa imeisha. Sasa huwa najiuliza, je kweli dawa hiyo inakuwa imeisha? Je haiwezekani kuwa huu ni ujanja tu unaofanywa na private health providers kujipatia free money? Je wadau mmewahi pia kukutana na hali kama hii? Kama ndiyo, je nini kifanyike kurekebisha hali hii?
   
 2. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeshakutana nayo Aga khan
   
 3. K

  KVM JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180

  Nadhani hapa NHIF wnatakiwa wasisitize kutolipa kama issue note ya hizo dawa haijasainiwa na mchukuaji.
   
 4. A

  Amakulu New Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KVM, tatizo ni kwamba ile fomu inasainiwa kwa signature moja tu na sio kwamba unasaini against kila huduma/dawa uliyopewa. Hivyo ukisaini tu NHIF hawawezijua zipi ulipewa zipi uliambiwa zimeisha.
   
 5. K

  KVM JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Hilo ni tatizo kubwa. Kwenye Health Insurance ninayoijuwa mimi mambo ni kama ifuatavyo:
  1. Ninapomwona daktari nasaini form ya insurance ya kumwona daktari. Yeye atapeleka madai ya kulipwa consultation fee pamoja na huduma nyingine alizotoa kama kupima damu n.k.
  2. Prescription ya dawa za kununua natembea nayo kwenda pharmacies mabalimbali kutafuta data. Nikipata dawa zote mahali pamoja basi ni nzuri, nasaini form ya insurance na wao hutoa issue note na vilevile wanatoa photocopy ya "doctor's prescription" ambavyo wanaambatanisha kudai malipo. Kama hawana dawa zote "issue note" itaonyesha ni dawa zipi nilipewa. Naendelea kusaka dawa ambazo sikuzipata kwenye pharmacies nyingine ambako nako nitasaini form nyingine za insurance na wao tatoa issue notes ya dawa walizonipa pamoja na kutoa photocopy ya doctor's prescription.

  Kwa kifupi basi, " One doctor'sprescription wil have many insurance forms signed by me".
   
 6. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye Helth Centre nyingi fomu zinasainiwa kabla ya kupata huduma, mgonjwa anaelekezwa asaini pale mapokezi, halafu copy ya mgonjwa hapewi. Ni full kuchakachua, mfano mzuri ni Helth Center ya Anglican Buguruni Malapa.
  Mi nilishakataa upuuzi huu, husaini baada ya kujazwa fomu yote na nadai nakala yangu.
   
 7. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Soma hapa:
  PATIENT CERTIFICATION:


  I certify that I received the above named services.
  Name...........................
  Signature..................
  Tel. No:........................
  Employer's Name and Address.............


  HIVI NDIVYO TZ INAVYOLIWA NA WENYE AKILI MUKICHWA.SIZUNGUMZII YA NHIF PEKEE.NI HATA KWENYE MIKATABA AMBAYO NCHI YETU INAINGIA + ZILE NYARAKA ANAZOSAINIGI MKUU WA KAYA BILA KUZISOMA VIZURI.
  Back to topic:


  Hapo juu ndivyo inavyosomeka na tunavyopitisha
  ( sijui kwa woga au mazoea?!) Maandishi yanaonyesha unasaini baada ya kupewa huduma lakini tunasaini kabla hatujajua tutapata dawa gani!
  NHIF INAIBIWA KWA UZEMBE WETU ! Ova.
   
 8. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ...excellent!
  Na zile form ziko 3:
  Moja inabaki kituo cha tiba,
  moja inaenda nhif
  na ingine anaondoka nayo patient.
   
 9. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Acheni uongo,ulizeni kama hamjui,
  Ni hivii,ukienda hospitali kutibiwa kwa NHIF kuna mambo mawili kuhusu dawa.
  Daktari anaweza kuandika dawa nne lakini wewe pale pharmacy ya hospitali wakakupa mbili na wakakuambia nyingine hamna.
  Isikupe tabu kwa NHIF wana form nyingine ambazo utajaziwa kutafuta dawa kwenye pharmacy nyingine za nje ya hospitali zilizoruhusiwa na bima pale utachukua dawa mbili na utasaini pia
  Kwa hiyo kama hujapewa zote dai hizo fomu sikumbuki mpangilio lakini ni NHIF 2b au A
   
Loading...