NHIF fuatilieni hili

NHIF fuatilieni hili

Dazzle

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
214
Reaction score
56
Kuna tabia ya kuliibia shirika inayoendelea pale Regency hospital hasa kwa upande wa pharmacy. Utakuta mgonjwa ameandikiwa dawa za wiki mbili ukienda pale pharmacy yao wanakubill dawa za mwezi mmoja ukiwauliza wanakujibu jeuri eti kwani unalipa wewe.

Hapa siandiki hadithi bali ni jambo ambalo limenitokea. Pamoja na kuhoji sana na kuwauliza hizo nyingine mnataka nizipeleke wapi?wanakujibu kazitupe.Baada ya kuwagomea sana wakaniandikia dawa za siku 20 badala ya siku 14.

Ombi langu kwa NHIF ni kuwa wafuatilie maana huu ni wizi wa mchana kama sio kuwasaidia wenzenu wauze stock kubwa ya dawa kila siku kiulaini
 
NHIF nao mbona wanatuibia pia mkuu?

Ngoma droo hapo.
 
Ukute kuna mkono wa mkubwa hapo.

Yani kila shida unayokutana nayo tanzania, jua kuna mkubwa ana mkono wake hapo
 
Makampuni yote ya bima za afya yanaibiwa sana.
Wakibaki na zile karatasi huwa wanabadilisha.
 
Pole sana ndugu! Vipi unaweza kutupia hako kadozi ulikoandikiwa na Dr wako? Yani aina ya dawa
 
Back
Top Bottom