Kwa hili NHIF watanzania tunawapongeza sana kudhibiti wizi kupitia Bima za Afya

Fyafyafya

Member
Nov 30, 2017
53
187
Kwa kipindi hiki watumiaji wa Bima za Afya wamekuwa wakipokea moja kwa moja ujumbe kwenye simu zao za mkononi kutoka NHIF kuwajisha kuwa Kadi zao za bima zimetumika. Kwa kutaja Tarehe; siku; muda na kituo cha afya au Hospital kadi hiyo ilikotumika.

Huu ni Mfano mojawapo:
"Card# 101500923816 Noella C Mtemi imetumika St. Joseph Soweto 12/12/2017 12:26 PM Ref# 521710414389. Piga 0800110063 iwapo hutambui muamala huu."

Huu ni utaratibu mpya na mzuri. Wamefata nyao za mabenk kama NMB ambapo mwamala ukifanyika tu hujulishwa kw simu.

Hata hivyo NHIF wamefanya hivyo kwa kuchelewa sana. Maana wamiliki wa vituo vya Afya ama mahospitali walikuwa wanaiba sana tena sanaaaaa kupitia hizo Bima.

Wizi ulikuwa unatokea hivi.

1. Kuongezea dawa nyingine ambazo mgonjwa hakupewa pale kwenye list ya dawa. Maana mgonjwa yeye kapewa ile form ya blue itaonesha dawa alizopewa na ile form ambayo hospita wanabaki nayo ndo huongeza dawa nyingine kadri wao wanavyoona inapendeza. Na mwisho wa siku hujumlisha katika kudai claim toka NHIF makao makuu.

2. Kuandaa Claim ( Madai) hewa.
Vituo ama mahospitali mengi walikuwa na taratibu za kuandaa wagonjwa hewa. Ilikuwa inakiw hivi.
Suppose mgonjwa ameenda kutibiwa leo tar 12. 12. 2017 ktk hospital flani basi hoslitali au kituo hicho walikuwa wanapika form ya mgonjwa huyo huyo kwa kuendeleza ugonjwa wa awali ama mwingine pia baada ya siku kam nne au tano. Maana ni kawaida mgonjwa kwenda kutibiwa leo hosp na akarudi tena kutibiwa pale pale baada ya siku 3 au 4 kwa kuwa anakuwa amezidiwa au dawa alopewa haikumsaidia. Hiyo ni kawaida sana.
Walikuwa wanaandika jina lile lile la mgonjwa; namba ya simu ile ile na sahihi yake ilikuwa inaigiziwa. Taarifa zote walikwa qanazichukuwa toka kwenye ile form ya mwanzoni.

Wamiliki wa hosp walikuwa wanapiga pesa ndefu baada ya mwezi kupitia huu ujanja. Sasa kwa utaratibu huu watakoma. Maana kama sijaenda hosp au sijaumwa halafu mala paaa napokea ujumbe kama huu "Card# 101500923816 Fadhili R Kassim imetumika St. Joseph Soweto 12/12/2017 12:26 PM Ref# 521710414389. Piga 0800110063 iwapo hutambui muamala huu" nitashikwa na butwaa kwanza na baadae kutoa taarifa polisi ili hatua nyingine zifatwe.

Hapa kweli ni kazu tu!!
 
Nadhani hili haliwasaidii sana. Hii notification ni ya kuonesha tu kadi yako inatumika. Kuna situation kama tatu ambazo zinaonesha NHIF hawanufaiki;

Scenario ya kwanza; endapo mwenye kadi akishirikiana na mtumiaji wa kadi yake ambae sie yeye hapo haiwasaidii chochote

Scenario ya pili; taarifa wanayokupa haioneshi dawa na gharama gani zimetumika ili kuona je, gharama gani halisi ulizotumia. Kwahiyo mfuko haunufaiki na haka kahuduma wakikuchakachua hats dawa wao hawawezi jua

Scenario ya tatu, kanotification haka hakana reliable feedback. Yaani MTU aseme kweli natumia au hapana sio mimi funga muamala instantly kama M-pesa au fast responses nyingine.

Mwisho, huu utaratibu umetubana wateja, iliwahi kunitokea September nimeenda kuzipa jino nikaanzia ubungo kibangu wakaniambia hawafanyi root canal wakanielekeza niende Madona hospital nafika tu naambiwa chini ya utaratibu huo kadi hutumika Mara moja tu kwa Siku.

Hawa jamaa huwa wana mambo ya ajabu sana wanufaika wa bima wamepunguzwa vigezo kibao masharti yameongezwa malipo yanaongezeka in relation to salary ila Huduma baaadhi zimeondolewa na wameweka limitation ya huduma. Mmh yangeongezwa mashirika tuwe tunajichagulia has a sisi tuliopo serikali za mitaa (walimu)
 
Wezi walikuwa ni Hospital ya Aga Khan. Kama Regency ungetozwa laki kwa kutumia Bima ya Afya, basi Aga Khan ingekuwa million 3 bila aibu
Naona umetoka usingizini mkuu,

Kama aga khan hospital wangekua wanapokea bima ya afya si tungejazana pale..

Aga khan hospital hawapokei hizo bima za NHIF..
 
Naona umetoka usingizini mkuu,

Kama aga khan hospital wangekua wanapokea bima ya afya si tungejazana pale..

Aga khan hospital hawapokei hizo bima za NHIF..
Aga khan Mbeya na Dodoma wanapokea,,
 
Naona umetoka usingizini mkuu,

Kama aga khan hospital wangekua wanapokea bima ya afya si tungejazana pale..

Aga khan hospital hawapokei hizo bima za NHIF..
Aga khan Mbeya na Dodoma wanapokea,,
 
Mwanangu alikazwa ili afanyiwe operation ya hernia! Eti nikaambiwa nitoe 20 ya Dr sasa sijui imekaaje hii na ana Bima.
 
Scenario ya pili; taarifa wanayokupa haioneshi dawa na gharama gani zimetumika ili kuona je, gharama gani halisi ulizotumia. Kwahiyo mfuko haunufaiki na haka kahuduma wakikuchakachua hats dawa wao hawawezi jua
Kazi hufanywa na Nhif ku reconcile,wanaweza hata kuhitaji kadi ya mgonjwa,ni hatari sana ukigundulika,yanaweza kukuta ya acacia na jela juu
 
Back
Top Bottom